webnovel

chapter 32

Anaamka jasho likimtoka anakaa kitandani akihema "uko sawa" anaingia Nzagamba akiwa na kibatari " ndoto mbaya tu,nimeota ndoto mbaya" anamjibu mkono wake ukienda kifuani pake kuangalia kama moyo bado upo wakati mapigo yake hata mtu aliyepitia nje anayasikia lakini bado alitaka kuhakiki kama upo." pole,usiogope ilikuwa ni ndoto tu" anamwambia akiweka kibatari pembeni ya kitanda chake " najua lakini ilikuwa inatisha sana" anaongea akikumbuka ndoto ni ileile aliyoiota usiku uliopita lakini Leo kukiwa na utofauti kidogo.

" lala nina uhakika hutaota tena" Nzagamba anamwambia akimfunika kaniki vizuri " nenda tu ukalale niko sawa" " basi usizime taa itakusaidia" anamwambia akisimama " sawa" Nzagamba anaondoka na kumwacha."nilijua nitakufa kwenye ndoto,kwa nini niiote tena hii ndoto,itakuwa ni hadithi niliyoisikia mchana tena,kuanzia sasa itabidi niikimbia kwa miguu miwili" anajisemea akigeuka

Alfajiri na mapema anaamka,anavaa nguo zake na kutoka sebuleni akiwa na kibatari mkononi " umeamka"Nzagamba anamuuliza akikaa kitako mwayo ukimtoka mdomoni kwake " ndio samahani kwa kukusumbua,inabidi niwahi kumpitia mama Ili tuwahi kuondoka" anajibu akikusanya vifaa vyake alivyoandaa jana,kijembe kidogo na sonzo anachukua na kaniki anaitupia shingoni kwake "mbona bado mapema,jogoo la tatu ndio limewika,ungelala kidogo isitoshe usiku hujalala vizuri" " hapana,tunatakiwa kufika huko kabla jua halijachomoza ili tuwahi kurudi jua likiwaka itakuwa shida kutembea na mzigo" anasimama akijiuliza kama amuombe ampeleke mpaka nyumbani kwa mjomba wake maana nje panamtisha,lakini itakuwaje kama akisema anamsumbua ,baada ya kugombana na akili yake anaamua kujikakamua aondoke mwenyewe tu sababu hii kazi ni yake "endelea kulala,naondoka " anamwambia akielekea mlangoni.

" unaondoka peke yako saa hizi?" Nzagamba anamuuliza akimwangalia kwa mshangao " ndio,Sasa niende na nani?" anamjibu akisimama na kumgeukia kwa matumaini " huogopi huko nje kukimbizwa na fisi?" anamuuliza,Tulya anakaa kimya akimwangalia " yaani wewe waajabu kweli,unaogopa watoto wa mbwa na mbwa ambao ni walinzi,fisi unawafanya marafiki zako" anamwambia akisimama " sijasema siwaogopi" anamjibu macho yakienda chini " ila?" naye anamuuliza " ulikuwa na mpango wa kufanya nao kikao wasikudhuru endapo ungeonana nao"

" unaweza kunipeleka mpaka kwa mjomba,tafadhali" anaomba na kunyanyua uso wake kumwangalia Nzagamba aliyekuja kusimama karibu yake kabisa.

Tabasamu linatanda usoni kwa Nzagamba " kumbe ulishindwa nini kuniuliza tangu mwanzo" " nilikuwa sitaki kukusumbua na isitoshe utakuwa umechoka" " kwa hiyo ulikuwa unanifikiria mimi,ukaamua kujitoa kafara" anaongea akitabasamu kumuona Tulya katika hali asiyo na njia " unanipeleka hunipeleki,maana ninachelewa" anabadilisha sauti baada ya kuona Nzagamba anafurahia hali yake 'huyo karudi aliyeenda likizo' anawaza Nzagamba akitamani kucheka kwa nguvu " hivyo ndivyo watu huomba msaada" anamuuliza "naona unafurahia hali hii" anamuuliza akimwangalia usoni.

" ndio,kwani sio kila siku kumuona Tulya akiwa kwenye miguu ya mtu" " twende bwana ninachelewa mama ataenda kunigombeza nikichelewa " anaongea akianza kutoka Nzagamba naye anamfuata,anafungua mlango na wote wanatoka, Tulya anageuka na kufunga mlango,wakati huo macho ya Nzagamba yakienda angani na kukutana na nyota na mwezi mkubwa " kutakuwa na giza siku tatu zijazo mwezi umeanza kuchelewa" anaongea macho yake yakiwa bado angani.

" ndio,nadhani kesho utachelewa zaidi" Tulya anamjibu na yeye macho yake yakiangalia mwezi "twende" anaongezea. Wanaanza kuondoka.Ghafla Tulya anasimama nakuanza kumwangalia

" kuna nini?"

" ndio umetoka mikono mitupu" anamuuliza

" unamaanisha nini?"

"namaanisha hujabeba silaha yeyote ile "

"anaongea mtu aliyetoka usiku peke yake,haina haja we twende"

"Haina haja kivipi,tukikutana na wanyama wakali tutafanyaje?"

" utakuwa umesahau kama wanyama hawawezi kunisogelea "

" aaah,samahani nilisahau" anaongea akianza kutembea huku akihofia kama amemkwaza.

" usihofu itakuchukua muda kuzoea,ngoja nikuulize wewe ulivyokuwa unatoka mwenyewe ungekutana na wanyama ungefanyaje na hukubeba hata silaha" anamuuliza wakitembea

" unamaanisha nini,bila silaha" anaongea akinyanyua kijembe chake kidogo kwa mkono wake wa kulia juu.

" hii sio kwa ajili ya udongo tu,inakata kote kama msumeno" anaongea kwa msisitizo na kumfanya Nzagamba acheke kwa nguvu.

" kweli? hicho kijembe,kingeua kitu gani?" Nzagamba anaendelea kucheka pasipokujua kuwa walikuwa wamesimama na Tulya akimwangalia usoni.

" nini?" anamuuliza baada ya kumaliza kucheka.

" unacheka!"

"eeh?"

" unacheka,tangu nikujue sijawahi kukuona ukicheka wala kutabasamu,natamani ingekuwa mchana niione sura yako ukicheka inakuwaje,ni mbaya umecheka usiku" anaongea macho yake yakiwa bado usoni kwake akitamani apate hata kibatari ili alione tabasamu.Nzagamba anakohoa kidogo na kujiweka sawa kwani yeye mwenyewe hakujua kama amecheka anaangalia huku na kule " twende" anaongea nakuanza kutembea

" mwangalie anavyokimbia utadhani kafanya dhambi ya kuvunja sadaka ya mizimu" anaongea taratibu na kuanza kumfuata nyuma.

Nyumbani kwa Mzee Shana wanamkuta Runde na Sinde wakiwa nje " Umechelewa" Runde anaongea baada ya kuwaona "shikamoo,habari ya asubuhi Sinde" Nzagamba anasalimia " Marahaba mwanangu,siku nyingine jitahidi umwamshe mapema mkeo"

" nzuri" anaitikia Sinde akipiga mwayo.

" shikamoo mama" Tulya nae anamsalimia

" Marahaba jitahiti kuwahi kesho"

" sawa mama" anamjibu

"mbona bado mapema sana mama" Nzagamba anaingilia

" ndio,kwa wanoenda kuchota maji,ila tunaoenda porini tumechekewa,jua likiwaka sijui kama mkeo atarudi na udongo,tusizidi kuongea hapa tunapoteza mda twendeni" Wanaanza kuondoka .

" haya safari njema" Nzagamba anawaaga.

" asante" wanamwitikia wakifuata njia naye anachukua njia aliyokuja nayo kurudi nyumbani.

Siku zinasogea Tulya akiwa amefinyanga vyungu vingi vya kutosha lengo lake akavibadilishe na bidhaa zingine siku ya kubadilisha bidhaa ikifika au gulio.Uhusiano wake na Nzagamba ukiendelea vizuri isipokuwa mmoja analala chumbani mwingine sebuleni.Tulya hakutaka kumlazimisha Nzagamba ahamie chumbani na kuamua kumpa nafasi anayoitaka kwani ameridhika na jinsi uhusiano wao unavyoenda kwa sasa.kuhusu mbwa aliowaleta Nzagamba alimwambia asiwahamishie nyumba yao na sasa amewazoea hawaogopi tena na wao wamemjua sana na kumfanya rafiki yao kwani muda wote akiwa anafinyanga vyungu uani huwa anaongea nao.Na anashukuru ndoto za kutisha kuhusu Ndesha hazijamjia tena.

kwa upande wa Nzagamba akiwa amemzoea sana mke wake na kumjua kidogo kuwa ni mwanamke anayejali sana hasa pale anpomuona akimhudumia mama yake na yeye, pasipo kulalamikia hali yao ya kimaisha.

mwanzoni alidhani kuwa hataweza kuyazoea maisha ya nyumbani kwake ya kula ndega Kila siku lakini Tulya amemuonyesha ni jinsi gani alivyo watofauti na pasipokujua anajikuta amempa nafasi kubwa ndani ya moyo wake kwani siku akiwa hayuko nyumbani muda wote hufanya haraka kurudi muda wote akautumie na mke wake.wazo la kuhusu mtu akimfuatilia bado liko palepale lakini Kila akiangalia haoni kitu,anaamua kuachana nalo na kulipuuzia lakini mara kwa mara humjia nakujikuta akitafuta anayemwangalia.

Marafiki zake wamekuwa wakimkuta mtoni na anawasaidia kupata chochote kile kulisha familia.siku mbili baada ya kumsaidia kujenga uwaaa mbiu ya lombo ilipigwa na wawindaji wote walienda porini kuwinda,walirudi na nyama lakini iliwachukuwa siku tano kurudi kwani walienda umbali mrefu sana.Hata hivyo uhaba bado upo palepale kwani mbiu haiwezi kupigwa kila siku na wawindaji kuingia msituni kwani baada ya windo kubwa kama lile wanyama wengi hukimbia mbali wakiogopa kuuwawa hivyo inabidi wasubiri mda mrefu ili wanyama warudi na hapa Kijijini hali inazidi kuwa mbaya watu inabidi wajifunze kula mlo mmoja na wengine wakianza kutega ndege kama Nzagamba.

Leo ni siku ya kubadilisha bidhaa au gulio,Tulya akiwa amevipanga vyungu vyake gulioni baada ya kusaidiwa na Sinde kuvileta asubuhi na mapema na yeye akiwa pembeni tayari kwa biashara "unauhskika hutaki kurudi nyumbani" anamuuliza Sinde aliyeng'ang'ania kubaki naye tangu asubuhi na sasa ni mchana na Tulya akiwa ameshabadilisha nusu ya mzigo wake "ndio,nyumbani kwenyewe amna hata kazi isitoshe kuanzia kesho kutwa nitakuwa nashinda ndani tu" anaongea Sinde akinyanyua mabega yake.

" imekuwaje wamebadili mpango wa harusi"

Tulya anamuuliza baada ya Sinde kumwambia kuwa tarehe ya harusi yake imebadilika na anatakiwa kukaa mwali.

" hata sijui,wamesema siku Tinde anatoka lindo kesho yake ndio iwe harusi yetu"

" mmmh,atakuwa huyo Tinde hataki kuchelewa,jiandae atakuwa na njaa huyo"

wote wanacheka.

" vipi wewe na Nzagamba bado tu" anamuuliza kwani Tulya na Sinde hawafichani chochote hivyo anaujua vizuri uhusiano wa Tulya na Nzagamba.

" hatua kwa hatua mama,nadhani tunaelekea huko"

" kuwa makini,majuzi nilisikia habari mtaani"

" habari zipi hizo?"

" nilikutana na mama yake Nsio akaniuliza kama ndoa yako Iko vizuri"

" kwa nini huyo mama atake kujua maisha ya ndoa yangu"

" sijui,anasema eti alimuona Nzagamba akiwa na Lindiwe na walisimama kwa mda mrefu tu wakiongea na sio yeye tu aliyewaona Kuna mama mwingine aliwaona siku chache nyuma Nzagamba akimtwisha kibuyu Lindiwe"

Tulya anahisi mwili ukifa ngazi,sura inapoa na kupauka kama damu haipo mwilini mwake kabisa anafungua mdomo wake aseme kitu anakosa cha kusema na kuufunga habari ilikuwa ni ya kushtukiza sana hakutarajia kuisikia.

" usijali sana,unajua maneno ya watu,najua Nzagamba sio mtu wa hivyo na wewe unalijua hilo lakini ndoa ni mahusiano zaidi fanya bidiii mwenzangu, Nzagamba sio kijana ambaye hajaoa tena hilo linautofauti asipopata kitu ndani atakitafuta nje" Sinde anazidi kukandia.

" namwamini hawezi kunifanyia kitu kama hicho" baada ya muda anapata ujasiri wa kuongea lakini ndani imani yake ikitetereka.

" najua,hata mimi namwamini Nzagamba lakini simwamini yule kiumbe mwingine,ukilinganisha na uhusiano wao wa nyuma akijitegatega anaweza kumwangusha hata kama kaolewa kuna wanawake ambao hawachelewi kujishusha na nina uhakika atataka kukuumiza tu sababu mumewe anamfanyia vibaya kwa sababu yako"

" Sinde tafadhali ninamjua Nzagamba,hawezi kuanguka kwa yule mwanamke unakumbuka alimuacha tena katika wakati mgumu" anajaribu kumtetea.

" ndio hapo Sasa,fikiria tangu Lindiwe avunje uchumba na aolewe na Manumbu walikuwa hawaongei hata wakikutana njiani walikuwa wanapitana tu,hivi sasa wanasimama na kuongea tena kwa mda mrefu tena mara mbili watu walizowaona,itakuwaje kama kuna zingine ambazo hawajaonekana,ninachomaanisha fanya haraka umfanye awe wako mmeoana kwa mda mrefu sasa na umempa nafasi ya kutosha huwezi jua endapo utalala naye nakushiriki naye tendo anaweza kukupenda "

Tulya anabaki kimya hamu ya biashara ikimtoka,anaendelea kujikaza asije uvumilivu uliobakia ukavunjika na kumwaga machozi Mbele za watu.

" Tulya!?" anasikia sauti ya kiume ikimuita na kumtoa mawazoni na macho yake yanataka kuanguka kwa mtu aliyemuona.