webnovel

chapter 33

" Tulya,kweli ni wewe" anamsikia mwanaume akiongea huku akisogea pale walipo macho ya Sinde yanatoka kwa kijana mtanashati aliyekuja kusimama walipo uso ukiwa umemjaa furaha kama muwindaji aliyopata mshale wake wa mwisho aliouangusha dakika za mwisho za kupambana na Simba.Sura ya Tulya ikiwa bado imejawa na mshangao.

" sikutarajia kukuona" anazidi kuongea yule kijana akimpuuzia Sinde aliyekuwa amesimama pembeni kama hajamuona,kumbe kweli hakumuona kwenye eneo hili alikuwa anamuona Tulya tu watu wengine hakuwaona kabisa.

" Luila,unafanya nini hapa?" Baada ya muda Tulya anaongea na kufanya mdomo wa Sinde kuanguka ' hii ndio huitwa Dunia ndogo' anawaza Sinde.

" unamaanisha nini kufanya nini,nimekuja mnadani,naona na wewe unabiashara" anaongea akiangalia vyungu chini.

" ndio,umeleta nini?" anamuuliza

" nimekuja na mbuzi na ngozi ya ng'ombe,vilevile nimekuwa kiongozi wa kuleta watu gulioni"

" aaaah! hongera" anamwambia na kumsikia Sinde akikohoa pembeni wote wanageuka na kumwangalia " habari yako" Sinde anamsalimia

" nzuri tu" anaitikia akimwangalia Tulya akimuuliza kwa macho nani huyu.

" huyu ni binamu yangu anaitwa Sinde,na Sinde huyu ni Luila"

" nashukuru kukufahamu,nimekuwa nikikusikia sana" anaongea Sinde "ouch!" anagugumia baada ya Tulya kumkanyaga mguu.

" kweli,sidhani kama Tulya angenizungumzia,ila nashukuru kusikia alikuwa ananizungumzia"

" sio kwa mazuri lakini" Sinde anamjibu akijichekesha

" najua,na sijali kwani ninastahili,ila nashukuru tu kuwa ananikumbuaka"anaongea macho yake yakiwa yamejaa matamanio

" naona unanunua vyungu na kuuza" anamuuliza macho yake yakiangalia vyungu.

" hapana nimetengeneza mwenyewe"

" kweli?ni vizuri sikujua kama unajua kufinyanga?"

" nimejifunza huku huku, na wewe imekuwaje umekuwa kiongozi wa msafara wakati ulikuwa unachukia kuzunguka gulioni"

" kwa sababu yako "anaongea na kuwashtua wote Tulya na Sinde

" nikisema kwa sababu yako utaniamini?"

" Luila mimi nim.."

" najua,nilisikia kuwa umeolewa,nilianza Kuja gulioni ulivyoondoka tu nikiwa na matumaini ya kupata bahati ya kuonana na wewe nikumbembeleza unisamehe na urudi lakini sikufanikiwa hata siku moja kukuona,habari za mwisho nilizopokea kutoka kwa shangazi yako kuwa unaolewa zilinivunja moyo na maini,sina wa kumlaumu ni makosa yangu." amalizia sura ikiwa na huzuni lakini mdomo ukiwa na tabasamu.

" Tuachane na hayo Luila kila mtu anamaisha yake Sasa hivi" anamjibu kwani hajui amwambie mara ngapi ili aelewe.

" najua,na sasa ndio nimeamini kabisa kuwa Kila kitu kimekwisha ila jua siku zote utakuwa moyoni mwangu,nimefurahi kukuona tena,nadhani tutakuwa tunaonana mara kwa mara sasa" anamuaga nakuondoka.

Nzagamba alikuwa anakuja akiwa na kikapu chenye chakula mkononi baada ya mama yake kumwambia amletee chakula mkewe anafika na kumuona mwanaume akiongea na mkewe ambaye hajawahi kumuona kabala hajafika walipo mwanaume anaondoka na kupishana naye ' mteja gani kaondoka pasipokununua hata chungu kwanza tangu lini wanaume wakanunua vyungu' anapotezea mawazo yake na kupiga hatua walipo Tulya na Sinde.

" ooooh! ni mzuri sana,kibaya tu hamkuoana" anamsikia Sinde akimwambia Tulya na miguu yake inapata breki pasipo yeye kujua.

" sinde,acha hayo ni ya zamani huko kabla sijaja huku"

" zamani vipi wakati unamuona mwenzio hajakuacha kabisa na kasema hapa wazi umesikia,'kumbuka Tulya siku zote utakuwa moyoni mwangu' sauti yake sasa" anamalizia akimwegelezea sauti yake

" mwanamke yeyote lazima ampende mwenzangu,mtanashati na anasauti nzuri kwa sasa sikulaumu kwa nini unampenda" anaongea Sinde pasipokujua Kuna mtu anasikia maongezi yao.Nzagamba anageuka na kuondoka moyo wake ukiwa umechwanwa vipande elfu Moja.

" ongea vizuri Sinde mtu akikusikia ataelewa vibaya hiyo ilikuwa zamani"

" najua,mbona nilikuona umeshtuka ulipomwona"

" hiyo kawaida Sinde,unajua sikutarajia kumuona tena hapa"

" kweli ni mshtuko"

" Tulya habari yako"

mtu anawasalimia na wote wanamwangalia.

" njema shikamoo " wote wanaitikia

" karibu mama Ntula" anamkaribisha

" asante,naona biashara yako inaendelea vizuri mpaka jioni utakuwa umemaliza"

" hivyohivyo kidogo mama"

" vyungu vyako ni vizuri Kila mtu anavizungumzia Kijijini?"

" kweli mama"

" ndio,unabisha nini wakati Mimi mwenyewe nilichukua ninavyo"

" nashukuru umevipenda"

" sana,halafu nimekutana na Nzagamba kanipa mzigo huu nikuletee " anampa kikapu chenye chakula.

" Asante, mwenyewe yuko wapi?" anauliza akiangalia huku na kule

" nimekutana naye pale kasema kana mahali anaenda"

" alishafika si angeleta tu hapa" anaongea akiangalia chakula

" nilimuuliza hivyohivyo akasema nimsaidie ana haraka"

" haya,asante mama" anamjibu na mama Ntula anaondoka.

" njoo tule kwanza" anamsikia Sinde ambaye alishatoa chakula tayari.

" nakuja" anajibu akiendelea kutafuta katikati ya watu kama atamuona Nzagamba,baada ya kutokufanikiwa anakaa nakuanza kula mawazo yakimpeleka anaharaka ya kuonana na nani,anatikisa kichwa kuyapuuzia.

Nzagamba anatembea umbali mrefu pasipo kujua anajikuta juu ya mti karibu na mto,mti unaompatiaga faraja siku zote,sehemu ambayo amna mtu anayekuja kumsumbua,penye amani na utulivu.lakini leo hivyo vyote havioni,utulivu wala amani kichwa chake na moyo vyote vimevurugika,akili yake inapiga makelele na neno moja tu "hakupendi,ana mtu anayempenda"

lakini kwa nini alikuwa anajifanya kama anampenda kumbe ana mwanaume mwingine ndani ya moyo wake.

Anakumbuka usiku wa harusi yao alipomwambia atakuwa analala sebuleni kwa mda aliyaona maumivu machoni pake,lakini kumbe hata hakuumia,ndio maana mpaka sasa hajamshawishi ahamie chumbani kwa sababu karizika anaona ni sawa tu " Tulya we ni mwigizaji mzuri sana" anajikuta akiongea kwa nguvu.Anajua hakutegemea upendo kutoka kwake kwa sababu hata yeye mwenyewe hampendi lakini kwa nini inauma namna hii,roho yake inamuuma na inatamani Tulya angekuwa anampenda yeye,anatamani angekuwa na moyo wake " Amna atakaye kupenda hujioni na mkosi wako huo,ameolewa na wewe kwa sababu hakutaka kuolewa na Manumbu na anaishi na wewe kwa kukuonea huruma tu,imekuwaje umesahau mapema kama wewe umelaaniwa" akili yake inamkumbusha." najua,najua lakini hapa moyoni natamani angenipenda mimi" anaijibu " endelea kuota " nayo inamjibu " kwa nini usikubali tu kuwa hakuna atakayekupenda na uishi na ukweli huo siku zote utajiepusha na kuvunjwa moyo namna hii" akili yake inaendelea kumpa ushauri.

Alikuwa ni mtu aliyeweka mimpaka yake katikati ya watu lakini Tulya amekuja na kuivunja taratibu ngome imara aliyojijengea Ili asiumizwe na watu tena imeanguka pasipo yeye kujua na ndio anagundua sasa akiwa ameshaumia, kuwa ulinzi wa moyo wake ulishasambaratika siku nyingi na moyo wake umevamiwa na kupigwa na mishale elfu moja na sasa unavuja damu,asijue atautibu vipi" nilijua ni watofauti sana" anajisemea akikumbuka nyakati alizomfanya aamini kuwa ni wa tofauti sasa anaona ipo siku akimchoka atakimbia na kwenda kwa mwanaume anayempenda.wazo hilo linamfanya moyo uume zaidi kwani inamfanya agundue kuwa hataki kabisa kumuona Tulya akiwa na mwanaume mwingine tena akiwa ameolewa lakini hana namna ya kumzuia endapo akitaka kuondoka.

Anaamua kuyapotezea mawazo hayo,anachukua kalimba yake nakuanza kupiga nyimbo iliyozoeleka .anaijaribisha kuipiga na kuiona kama ni ya tofauti,hapo ndipo anakumbuka kuwa ni siku nyingi hajaupiga huu wimbo,anatoa kicheko kuwa haamini kama aliacha kuipiga hii nyimbo siku nyingi zilizopita pasipo kujitambua.Ndipo anagundua kuwa ni mambo mengi sana yalibadilika pasipo yeye kujua.Anaiweka vizuri mkononi mwake na kuanza kubonyeza tena lakini sauti ya mziki huo haikumpendeza masikioni tena wala kumfariji kama zamani,anaamua kuacha anairudishakiunoni pake na kuulaza mgongo wake juu ya tawi la mti nakufumba macho yake,hakujua ni mda gani ulipita akiwa pale juu ya mti alipokuja kuyafumbua macho yake anakutana na giza totoro anashuka taratibu na kuanza safari ya kurudi nyumbani.

Anaingia uani mwa nyumba yao na kukuta pako kimya ikionyesha watu wote wamelala,anatoa tabasamu la huzuni,amezoe kila akirudi amechewa humkuta Tulya nje akimsubiri,anamkaribisha na kumtengea chakula,Leo hii hakuwaza kumsubiri " atakusubiri vipi wakati hata hakukumbuki anamkumbuka mpenzi wake" akili yake inamwambia.Anazunguka uwaani na kuwafungulia mbwa " najua hata nyie wenyewe mkijua ukweli mtaona mmesalitiwa kama mimi hivyo ni vyema msijue kabisa" anawaambia mbwa waliokuwa wakitikisa mikia yao wakimlamba vidole.anasimama na kuelekea ndani mbwa nao wakimfuata nyumanyuma wakiendelea kutikisa mikia yao na kubweka.Anafungua mlango na kuingia ndani anakutana na giza moto kwenye mafiga ukiwaka kwa kufifia,anaenda na kuukoleza anawasha kibatari mwanga unaimulikia sebule,anaona ngozi ikiwa imetandikwa na chakula kikiwa kimefunikwa pembeni.anaamua kukipuzia chakula na kujitupa juu ya ngozi anazima kibatari na kufumba macho yake.Tulya naye aliyekuwa macho akimsubiri anafumba macho baada ya kuhakikisha amerudi nyumbani salama.myo wake ukimuuma na kuwaza,pengine alikuwa na Lindiwe mda wote huu na walikuwa wanafanya nini,mawazo yake yanapotea pale usingizi mzito ulipomchukua pasipo kuualika.

Imekuwa ni siku tatu tangu Kila mmoja apate habari ya kutawanya moyo,mazungumzo yao yamekuwa sio kama awali,Wanaongea kwa kifupi tena pale panapohitajika.Nzagamba amekuwa akiondoka asubuhi na kurudi usiku,na hii inamuumiza zaidi Tulya kwani Kila mara akili yake inamtuma kuwa atakuwa na Lindiwe na anaogopa kumuuliza asije akakubali kwani hilo litamvunja vibaya na hataweza kutengenezeka. Hivyo akaamua kuanza kumsubiri nje usije mdomo wake ukamsaliti na kumuuliza ametoka wapi.Anaamua awe anamsubiri ndani chumbani kwake pasipo Nzagamba kujua. Nzagamba akirudi kila siku anajua amelala.Bibi sumbo analiona hilo lakini hataki kuingilia ugomvi wa wanandoa tena unaoendelea kimya kimya anawaacha watatue wenyewe." chakua chakula umpelekee mumeo mtoni" Bibi Sumbo anamwambia Tulya aliyekuwa anafinyanga vyungu akiweka chakula chini karibu yake." lakini huwa hataki tumpelekee chakula" anamwambia mikono yake ikiachia udongo.

" Ndio,lakini kaondoka asubuhi sana na Sasa ni mchana atakuwa na njaa,we peleka" anasisitiza " Kuna tatizo?" anauliza baada ya kumuona akisita " Amna,nanawa mikono na kuondoka Sasa hivi" anamjibu akinyanyuka Bibi Sumbo anamwacha.Ananawa mikono yake na kuvaa viatu vyake anachukua kikapu cha chakula nakuanza kutembea,anapiga hatua chache na kusimama anajinusa mwili wake nakuona ananuka udongo,anakumbuka maneno ya Sinde " kwa nini usimfanye akutake"

" kivipi?"

" mfanye akose uvumilivu wa kulala sebuleni,mfanye ahamie chumbani mwenyewe,nadhani umenielewa"

Anarudi ndani haraka,anachukua kaniki na kwenda kuoga.Bibi Sumbo anamuona na kutoa tabasamu.Anaoga haraka na kutoka,anaingia ndani anajipaka mafuta na kutafuta sketi nzuri inayomwonyesha shepu yake vizuri na kitambaa Cha kufunga maziwa yake kilicholegea,anakivaa na kufunga maziwa yake pasipo kuyakaba,saa sita yake kifuani inasimama vizuri akitembea inatikisika " najua ni mbaya,lakini nafanya hivi kulinda ndoa yangu" anajisemea na kutoka,anachukua kikapu na kuondoka mapigo ya moyo yakiongeza mwendo kila hatua anayopiga " unaweza Tulya" anajisemea akikaribia mtoni.Lakini kabla hajafika anasikia watu wakiongea mwanaume na mwanamke " mbona sauti ya kiume kama naijua anajisemea na kusogea karibu na zinakotokea sauti.Miguu yake inakosa nguvu kwa anachokiona,Mbele yake amesimama Lindiwe na Nzagamba.