webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · 现实
分數不夠
245 Chs

UNAMFAHAMU?

Edrian alipoona Aretha kakubali, akamwangalia Allan kisha akapiga hatua kumsogelea Aretha

"Rian ninaomba ni____" Kabla hajamaliza Edrian akatikisa kichwa kumwambia asiendelee kuongea kisha akainama na kumwambia

"Endeleeni, ukimaliza niko nje nakusubiri kwenye gari"

Akatoka huku Allan akimfuata akijaribu kumuelewesha

"Bro sijui chochote nakwa_" Edrian akageuka

"Allan nakuamini, samahani kwa sababu sijisikii vyema kuendelea kukaa humu ndani. Niombee radhi pia kwa Renatha. Usihofu."

Allan alipomwangalia Edrian usoni hakuelewa aamini maneno yake au akubaliane na uso ambao ulikuwa kama mwali wa moto.

"Sawa bro. Nashukuru sana. Nisamehe kukuweka mazingira haya." Allan akaonesha kujutia

Edrian akamgusa bega,

"Hakuna kosa lolote bro." Alipomaliza akaelekea kwenye lifti,

Allan akarudi mahali alipoketi Renatha huku akiangaza kuona Aretha aliketi wapi.

Kwa upande wa Aretha bado hakuamini mambo yaliyomtokea, alipoingia hakuwaza kuwa angeonana na Edrian. Mara Edrian alipoondoka alibaki akiwa amesimama huku akishtuliwa na BM ambaye alinyoosha mkono kumuelekeza afuatane naye.

Miguu ya Aretha ilikuwa mizito lakini akajitahidi kumfuata BM, mawazo yake yalikuwa katika mkanganyiko mkubwa.

BM akamwangalia Aretha huku akijua ameshtushwa na uwepo wa Mr Simunge pale, akamwambia

"Aretha, samahani sijui ni kwa namna gani mnahusiana na Mr Simunge lakini sikujua kama angekuwepo hapa."

"Aaa Mr B____"

"Niite Bon" BM akamwambia

"Ahm...Mr Bon, tunaweza kuongea kwa wakati mwingine?" Aretha akaongea kwa wasi wasi huku akitazama alipoketi Allan akiwa na Renatha ambao walionekana wakiinuka kutaka kuondoka

"Aaah basi sawa, lakini ninaomba kujua kama ile kazi utaweza kuifanya?" BM akamuuliza

Aretha akaangalia simu yake akaona ujumbe umetoka kwa Edrian, akafungua

"Ukitoka nijulishe" akarudisha simu na kisha akamjibu BM, "Hiyo kazi inaweza kusubiri baada ya wiki mbili?"

"Mmmh, sawa, ila ni vizuri ukajua kile nakitaka." BM akamwambia kisha akatoa kifuko kidogo sana kilichofungwa akanyoosha kumuelekea Aretha akipokee

Aretha akatazama kisha akapokea huku akibaki anamtazama kama afungue

"Usifungue, hilo ni jiwe la 'Ruby' nataka picha ambayo utalificha lisionekane" akamaliza kumwambia huku akimtazama usoni.

Aretha akamrudishia kile kifuko, "Mr Bon samahani siwezi kukaa na kitu cha thamani hivi"

BM akatabasamu na kumwambia "Nakuamini sana Aretha. Tafadhali nakuomba unifanyie kazi yangu"

Aretha akaweka kile kifuko karibu na BM akainuka "samahani Mr Bon nafikiri itakuwa vyema tuongee kwa wakati mwingine. Naomba niende." Akaaga akionesha wazi alikuwa na haraka

BM akatabasamu huku akichukua kifuko kile akakirudisha kwenye mfuko wa koti "Sawa hamna shida Aretha. Nadhani kuna mengi yametokea. Asante kuitikia wito"

Aretha akaondoka kwa haraka kuelekea kwenye lifti.

Allan na Renatha walibaki wakitazamana baada ya Allan kurudi na kuketi,

"Allan kuna nini kinaendelea na yule dada aliyeingia?"

"Renatha samahani lakini bro Ed amepata dharura hatorudi. Naamini ulimwambia uliyotaka kumwambia" Allan akamwambia

"Sawa, nadhani amesikia nilichomwambia, lakini nataka kujua huyo dada ni nani?" Akauliza tena Renatha

Allan akamtazama Renatha "Renee kama humfahamu hakuna sababu ya kumfahamu. Nafikiri nikuache"

"Allan sikia yule dada ni kama namfahamu ila sijui nimemfananisha au la" kulikuwa na hisia mchanganyiko wakati Renatha akiongea hata kumfanya Allan kuhisi maumivu yake katikati ya maneno yale

"Renatha, unamfahamu?" Akauliza akimtazama usoni ambapo aliona huzuni kwenye macho yake lakini ghafla akatabasamu

"Haha basi. Tunaweza kuondoka wote?" Akauliza Renatha

Allan akakubali nao wakatoka, wakati huo akaangaza alipoketi Aretha akamuona yuko katika mazungumzo na yule mwenyeji wake.

**********

Alipofika kwenye gari, Edrian akachukua chupa ya maji iliyokuwa ndani ya gari akanywa. Alipomaliza akashusha pumzi kwa nguvu kisha akampigia Derrick na kumuuliza iwapo alijua chochote kuhusu BM kukutana na Aretha,

"Bro sijui chochote lakini nimekuta amenipigia jioni hii nami nilikuwa nimepumzika." Derrick akamjibu akishangaa