webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

TWENDE KWAKO

Edrian akakata simu mara tu alipoambiwa na Derrick kuwa Aretha alijaribu kumpigia.

"What are you trying to do Retha?" Akanong'ona kisha akaegama kwenye kiti. Akatafakari kama BM alimfanyia makusudi au ilitokea kama ajali kuwa wote wamekutana sehemu hiyo.

"Nahitaji kufahamu nini hasa wameongea" akawaza kisha akachukua simu na kumtumia ujumbe Aretha "Ukitoka nijulishe"

Akijaribu kupata utulivu lakini bado alihisi donge ambalo lilimkaba kwenye koo. Mapenzi ni jambo ambalo alilikwepa tangu mwanzo, sasa kwa namna ambavyo alihisi aliona ni kama moyo wake hauwezi kuwa sawa kama ulivyokuwa zamani.

Akiwa kwenye mawazo alimuona Allan akitoka na Renatha, akakumbuka maneno ya Renatha,

"Kuna kitu nataka uwe makini nacho lakini sitakwambia kwa namna gani, utakapo niamini na kuniambia kitu unachokificha ambacho hakuna mtu mwingine anajua zaidi yako, nami nitakwambia ufanye nini"

"Huyu mwanamke anamaanisha nini" akawaza..

Akawaangalia walipoingia garini, "au Allan anampenda huyu dada?" Akajiuliza kisha akashusha pumzi huku akitazama mlangoni kama Aretha angetoka.

Akiwa mawazoni alishtuliwa na simu iliyoita, akapokea kabla ya kusema chochote sauti ya Aretha ilisikika ikiwa na wasiwasi "Rian nashuka kwenye lifti uko wapi?"

"Nitakusubiri mlangoni" akajibu kisha akakata simu lakini usoni kulikuwa na tabasamu jepesi

Akasogeza gari karibu na mlango wa kutokea ambapo alimuona Aretha kupitia kwenye kioo akitembea kwa haraka kuelekea mlangoni. Akafungua mlango wa gari, Aretha akaingia na kufunga mlango. Edrian akauliza pasipo kumtazama usoni

"Nyumbani au kuna sehemu unaenda?" Swali lile lilimfanya Aretha asikie ukakasi uliokuwa kwenye sauti ya Ed. Akamgeukia,

"Rian, tafadhali usifikiri kitu king__" kabla ya Aretha kumaliza kuna mtu aligonga kwenye kioo cha upande wa Edrian.

Edrian akashusha kioo, alikuwa ni mlinzi ambaye alimuelekeza kusogeza gari mbele kwa kuwa mahali pale hapakutakiwa kusimama kwa muda mrefu.

"Sawa, samahani kamanda" Edrian akamwambia kisha akaondoa gari, walipokaribia kwenye geti akamuuliza tena Aretha

"Nyumbani au kuna mahali unaenda?"

Aretha akameza mate kisha akampa jibu ambalo lilimshtua Ed

"Naenda kwako." Sauti ya Aretha ilikuwa na dalili za kulia

"Retha" Edrian akashtuka na kumuita

"Endesha twende kwako nitakwambia ili uniamini" Aretha akamwambia huku sauti yake ikimezwa na huzuni ambayo kuna namna ilifanya moyo wa Edrian uyeyuke. Akakanyaga mafuta na kuondoa gari taratibu,

Edrian alibaki njia panda akiwaza kwa muda ule aende na Aretha nyumbani kwake au ampeleke nyumbani. Kabla hajauliza Aretha aliinua simu na kuweka sikioni

"Mama, niko salama!" Akaongea kwa unyonge kisha akaendelea

"Nitakutumia ujumbe sasa hivi mama" alipomaliza akakata simu kisha akaandika ujumbe.

Edrian hakujua nini ameandika akamuuliza huku akitupia jicho la wasi wasi kujua kama Aretha alimaanisha

"Retha najua ku___" lakini kabla ya kumaliza Aretha akainua uso wake

"Rian endesha twende kwako tafadhali" alipomaliza akaegemea kiti huku akitazama nje

Edrian akamwangalia kisha akafanya kama alivyosema, akakunja kushoto huku akiendesha taratibu akitafakari nini Aretha alikuwa akiwaza. Mawazo yake yakashtuliwa na mlio wa simu yake, alipotazama aliyepiga simu moyo wake ukadunda kwa mshtuko, akamwangalia Aretha ambaye hakuonesha kujali ile simu iliyoita kwa Ed

"Hello mama. Shikamoo" Edrian akapokea

"Mwanangu, marhabaa" akaitika mama kisha akaendelea..

"Mwenzio kaniambia atalala hapo kwenu leo, mwanangu ninakuamini sana nisaidie nakuomba" mama alionesha kutafuta maneno gani ya kufaa aweze kuongea lakini hakujua kwa kiasi gani Edrian alikuwa kwenye mshangao ambao alijaribu kuuficha huku akimtazama Aretha.

"Sawa mama, usihofu, nakuahidi kabisa. Kila kitu kitakuwa salama" Edrian akamjibu mama.

Walipomaliza kuongea hakuweza kuongea chochote kwa Aretha hakujua kwa nini maamuzi yale yalifanyika. Akamwangalia kila mara, lakini Aretha aliegama kwenye kiti macho yake akiwa ameyafumba huku akiweka mikono yake tumboni.

Wakafika nyumbani kwake, Edrian alipoegesha gari alidhani huenda Aretha alilala akamuita "Retha"