Annabella alishangazwa na ujio wa Reuben na Joy nyumbani kwake. Uwepo wao uliwakilisha jeshi kuu la taifa hivyo hakuwa na budi kuwakaribisha ndani. Sebuleni walikuta mabegi makubwa mawili yaliokwisha kupakiwa. Annabella aliwaalika kuketi.
"Nimesikia habari jana jioni.", alianza,
"So unajua kwa nini tupo hapa.", Reuben alisema,
"Najua kwanini.",
Reuben alinyoosha kidole chake kuelekea kwenye mabegi, "Kuna sehemu unakwenda?",
"Um, yeah, Cyprus.",
"Kwanini?",
"Kwanini? Because I need a breather.", alisema Annabella kwa msisitizo, "Haya yote yanayoendelea yananikosesha amani.",
"Ndio maana ukakata tiketi ya ndege masaa machache baada ya kujua kuwa upo miongoni mwa watuhumiwa.",
Annabella alishangaa, "Are you saying nataka kutoroka?",
"Ndivyo inavyoonekana.", Reuben alisema,
"Sina sababu ya kutoroka.",
"Annabella, umeshawahi kukutana na marehemu Montana?", Reuben aliuliza,
"I wish I did.",
"So hujawahi kukutana nae?",
"Sijawahi.",
"Kwa jinsi unavyoongea inaonesha kuwa ulikuwa unamchukia sana marehemu.",
"Sio nilikuwa, bado ninamchukia na nitaendelea kumchukia.",
"Kwanini?",
Hasira ya Annabella haikujificha, "Hakuwa na sababu ya kumtafuta mwanangu na kumuhoji. It was none of her fucking business. Whether nilimtelekeza mwanangu au la, haikumuhusu. Alijua kabisa mwanangu ni my weakness lakini bado alimtumia. Hivi unajua ni maumivu gani niliyoyasikia ile siku?",
"Naelewa. Wewe ni mama mwenye majuto mengi. Hakutakiwa kutonesha kidonda chako.",
"Exactly. I'm so sorry to say this but I'm glad she's dead.",
Joy alitupia macho ya wizi kukagua kucha za mikononi kwa Annabella. Kucha zake zilikuwa fupi na hakukuwa na dalili ya kucha za bandia.
"Annabella, naelewa uchungu wako. Najua haisaidii chochote but I'm sorry kwa kilichotokea.", Reuben aliomba msamaha,
"It's not your fault.",
"Kutokana na nature ya hii kesi, I'm afraid hautaruhusiwa kusafiri nje ya nchi mpaka kesi itakapoisha.",
Ingawa jambo hilo halikumfurahisha Annabella, ilibidi akubaliane nae.
Reuben alimgeukia Joy kumpa uhuru wa kuuliza swali kama analo. Joy alikuwa na swali;
"Miss Annabella, tumesikia stori yako, ila ushahidi wetu unaonesha kuwa mmoja wenu yupo guilty. Kwa haraka haraka unahisi ni nani?",
"Suzy au Janat. Hao wawili wamepoteza kila kitu; Suzy kapokonywa kampuni, Janat obviously ataenda jela. Muuaji ni mmoja wao. Ila hiyo ni opinion yangu.", Annabella alijibu.
Reuben na Joy walifunga mahojiano yale.
…
Suzy hakutegemea kuiona simu ya Janat. Mara yao ya mwisho kuzungumza ilikuwa siku siri ya Suzy ilipotobolewa, na maongezi yao hayakwenda vizuri. Suzy alijua urafiki wao umekwisha, ila sasa simu yake ilikuwa ikiita na namba ilikuwa ni ya Janat.
"Sema.", Suzy alitamka mara tu baada ya kupokea simu,
"Suzy, umesikia tetesi?", Janat aliuliza,
"Tetesi gani?",
"Annabella amehojiwa leo.",
"So?",
"One of us might be next.",
Suzy aliguna kwa dharau, "Hivi kumbe bado tu kesi yako haijaisha uende jela?",
"What?",
"Unakabiliwa na kesi ya mauaji. Unatakiwa uwe jela.",
"Wewe sio wa kuniambia mimi hivi. Wewe na mimi hatuna utofauti wowote. Ulimfanya binamu yako kichaa ukaiba business plan yake.",
"Embu usinichekeshe. Watu wapo wanafariki kwa cancer ulizowapatia kwa bidhaa zako mbovu. At least mimi sijaua mtu. Ila wewe una msululu wa maiti nyuma yako.",
"Watch your mouth, Suzy.",
"Yani nilivosikia habari zako nilitishwa. Siamini nilikuwa rafiki wa muuaji. Yani bila shaka hata Montana itakuwa wewe ndiye uliemuua.",
"OKAY ENOUGH!", Janat alipayuka kwenye simu, "Unavuka mipaka sasa. Nimepiga simu kwa nia nzuri, sio kukashifiwa na wewe. Alafu usijifanye mkamilifu. Wewe mwenyewe ni muuaji tu na dictator.",
Suzy alicheka, "Unajiona umeongea mwenyewe. Embu fanya hivi; futa namba yangu na usinitafute tena. Isije laana yako ikanifikia na mimi bure.",
Suzy alikata simu na kuirusha kwenye kochi. Alikuwa na hamu sana ya kumtamkia maneno yale Janat, na hatimaye maombi yake yalijibiwa. Alijihesabia kuwa hana rafiki na hakutaka tena kujali hisia za watu. Kwa sasa kitu pekee alichotambua ni kuwa kila mtu alimchukia, hivyo na yeye pia alifanya uamuzi wa kumchukia kila mtu.
…
Paul aliingia nyumbani kwa Leah kwa hasira na amshaamsha. Alikuwa akitweta, uso ukiwa umefunikwa na jasho.
"LEAH!", aliita kwa nguvu akiwa chini ya ngazi za sebuleni, "LEAH!",
Leah alitoka chumbani kwake na kufata sauti ya Paul. Hakuelewa ni kwanini vurugu iliingia kwenye nyumba yake. Yeye alipenda ukimya na utulivu. Akiwa kwenye ngazi aliweza kuona jinsi Paul alivyokuwa hajatulia. Mara alikuna kichwa, mara alitembea huku na kule. Alikuwa mtu aliekosa subira.
"Vipi kelele jioni yote hii?", Leah aliuliza huku akishuka ngazi,
Paul alimuangalia kwa jicho la ukali, "Ulikuwa wapi leo?", aliuliza,
"Eh, tumeanza kuulizana hayo maswali lini?",
"Leah, usinitanie! Ulikuwa wapi leo?",
"Naomba usinipayukie, wewe vipi? Alafu unataka ujue nilipokuwa ili iweje?",
"Ulienda kumuona Cecy?",
Leah alitabasamu kidogo. Sasa alijua sababu iliyomfanya Paul awe namna ile.
"Umemwambia nini?", Paul aliuliza,
"I just wanted to see my competition.", Leah alijibu kwa staha,
"Kwanini umeenda kumuona na ni kitu gani umemwambia?",
"Maongezi ya kike hayakuhusu _",
"HATAKI KUNIONA TENA!", Paul alitamka, "Cecy hataki kuniona tena.", sauti yake ilibeba uchungu. Ni kweli kwamba swala lile lilimuumiza sana. Kwa bahati mbaya hicho ndicho kitu Leah alichotaka.
"Hivi ni macho yangu au ni kweli kuwa unataka kulia?", Leah aliuliza,
Paul aliangalia pembeni. Ni kweli machozi yalikuwa yakimnyemelea.
"Are you seriously coming to complain about your mistress to your wife?",
"Nilishakwambia tuachane. Mbona unakuwa king'ang'anizi? Umemwambia nini Cecy mpaka amenichukia hivi?",
"Nimemwambia ukweli.",
"Ukweli gani?",
"Ukweli ambao wote tunaujua.",
"Leah _",
"Ukweli kuwa humpendi bali unataka kumtumia tu ili ujisikie vizuri.",
"WHAT!",
"Oh come on, Paul. Sababu ya wewe kutaka kuvunja ndoa yetu ni kwasababu I'm richer than you. Sasa hivi unahamu sana ya kuwa na mwanamke wa uchumi wa chini ili ujisikie powerful.",
"Leah hunijui!",
"Nakufahamu fika, nje na ndani, juu na chini. Nothing about you surprises me.",
"I love Cecy.",
"Maybe.",
"Unamaanisha nini 'maybe'? Unajua nampenda.",
"That's sad.", Leah alitazama saa ya ukutani, "Kama umemaliza unaweza kwenda. Huishi hapa tena.",
"Umemuofa nini Cecy? Niambie.",
"Nimemfungua macho yake tu.",
"Umemwambia nini?",
"Kamuulize mwenyewe.",
Leah alianza kupanda ngazi kurudi chumbani kwake,
"Leah, wewe ni demon!", Paul alitema sumu, "Unataka uwe na furaha peke yako!",
Leah alimgeukia kwa hasira, "Furaha?", aliuliza, "Furaha gani hiyo unayoiongelea? Mume wangu wa miaka kumi anataka kuniacha kisa mwanamke mwingine. Isitoshe I had to find out about it from the radio. Kwamba ulikuwa unanicheat miaka yote hii. I've wasted my love, energy and time on somebody who doesn't give a shit about me. Furaha? Unahisi nina furaha?",
Paul hakuweza kujibu.
"Wewe ndio ulikuwa familia yangu pekee, Paul. Sina ndugu. Sina uwezo wa kupata mtoto but it was okay kwa sababu bado nina wewe. Lakini unathubutu kunitelekeza bila hata huruma? Bila hata msamaha? Mama yako ananitamkia maneno ya kashfa na wewe hata hunitetei. Furaha? Furaha? Seriously?",
"Leah, you're rich. Una uwezo wa kupata mwanaume yoyote na kumove on.", Paul alijitetea,
"You're right. Naweza nikafanya chochote nachotaka. So, Paul, as long as mimi sina furaha, wewe pia hautakuwa na furaha. Case closed. Get out of my house.",
"Leah _",
"Toka!",
Ilibidi Paul aondoke taratibu maana moshi ulifuka kwenye kichwa cha kila mmoja wao. Wote wawili walikuwa na la kusema na hakuna aliyetaka kumsikiliza wala kumuelewa mwenzie.
***