webnovel

CHAPTER 15

Usiku, kama kawaida wakiwa ofisini, Joy aliendelea na upelelezi wake wa mtandaoni. Ingawa kesi ilipata watuhumiwa bado kuna maswali alikuwa nayo. Aliweka juhudi kwenye kusaka taarifa yoyote ambayo ingeweza kusukuma kesi iende lakini aliona anaelekea kukwama. 

"Labda nina usingizi.", Joy alisema kimoyomoyo.

Kikombe chake cha kawaha kilikuwa kitupu. Alinyanyuka na kuelekea mlangoni. Reuben alikuwa bize akisoma ripoti zilizokuwa juu ya meza yake. Kahawa yake ilikuwa haijaguswa.

"Detective, naenda jikoni kutengeneza kahawa.", Joy alisema akiwa mlangoni, "Kama yako imepoa naweza nikakupashia.",

"Amna shida. Kahawa yangu ipo sawa.", Reuben alijibu bila kunyanyua macho.

Joy alitikisa mabega na kuanza kutoka. Lakini ghafla kengele ya kompyuta yake ililia. Hii ilikuwa ishara ya kupatikana kwa taarifa. Haraka, Joy alirudi mezani kwake na kuisogeza kompyuta karibu. Alisoma taarifa ile kwa makini.

"Detective.", Joy aliita,

"Yes. Umepata chochote?", Reuben aliuliza,

"Ndiyo. Nimegundua kwanini tajiri alimtumia Montana kutoboa siri za kina Annabella.", alisema kwa tabasamu la auheni,

"Kwanini?",

"Montana alikuwa na dada; Angela Sabas.",

Reuben alinyanyua macho na kutazama upande wa Joy.

"Dada yake yupo wapi?", aliuliza,

"Angela Sabas alifariki dunia mwaka 2010 baada ya kutumia dawa za uzazi wa mpango kutoka JM Pharmacy.", Joy alijibu, "So, inamaanisha Angela alikuwa miongoni mwa mabinti waliofanyiwa the first trial na kampuni ya Janat.",

"Kwa mujibu wa ripoti, inasemekana kuwa wote walifariki.",

"Ndiyo, na Angela alikuwa miongoni mwao.",

"Okay.", Reuben alitikisa kichwa, "So, tajiri alimfata Montana na kumuofa hili deal kwasababu alijua tayari Montana alikwishabeba chuki juu ya Janat and possibly every rich person in the universe. Tajiri alijua kuwa Montana atakubali ombi lake hata kama litamtia hatarini.",

"Yes. But ukifikiria zaidi, kuna uwezekano mkubwa wa Janat kumfahamu Montana instead of others. Na kama alimfahamu, pia kuna uwezekano mkubwa alipajua alipoishi. And finally, anaweza akawa the killer.", Joy alitengeneza mtiririko,

Reuben alionesha kufurahishwa na muelekeo wa kesi. Hatimaye walipata jibu la swali 'Kwanini Montana?'. Maswali yaliobaki bila jibu ni jina la tajiri aliemuajiri Montana, na mtu aliemuua Montana na mama Zai. 

Janat alisindikizwa na askari mpaka kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam. Njia nzima alikuwa akiuma kucha na kujitahidi kutuliza moyo uliyokuwa ukidunda kama ngoma za jadi. Janat alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji na haikumpa matumaini. Sasa alikuwa akielekea kituoni kuhojiwa na bwana Reuben, mpelelezi mwenye akili na uzoefu kuliko wapelelezi wote nchini. Hii ilimaanisha uongo wowote atakaotamka utamtokea puani. 

Dunia yake iliingiwa na giza. Hata usingizi alikuwa hapati. Alikuwa akitegemea mvinyo umpatie usingizi lakini baada ya muda hata mvinyo haukuweza kumsaidia. Kila afumbapo macho aliona na kusikia sauti za vilio. Alikuwa na wakati mgumu sana.

Walipowasili kituoni, Janat alipelekwa kwenye chumba cha mahojiano. Alikuta Reuben na Joy tayari wameketi wakimsubiri. Janat alikaa kitako na kujitahidi kuweka sura ya kujiamini.

"Janat Marko; ulimfahamu vipi marehemu Montana?", Reuben aliuliza mara moja,

"Alikuwa ni _ alikuwa ni mtangazaji.", Janat alijibu kwa kukwama,

"Unamaanisha kabla ya hapo haukumfahamu na wala haukuwahi kukutana nae?",

Janat alimuangalia Reuben machoni na kuona kuwa kuna kitu tayari alifahamu. Alivuta pumzi,

"Nilikutana na Montana mwaka 2010, lakini mazungumzo yetu hayakuwa ya muda mrefu hivyo hata sura yake ilinipotea.",

"Mlipokutana mwaka 2010, mazungumzo yenu yalihusika na nini?",

Janat alisita kujibu maana jibu lake lilikuwa linaenda kumdidimiza zaidi. 

"Janat, naomba nisikie jibu lako tafadhali.", Reuben aliongea kwa mkazo,

Janat aliogopa, "Montana alikuja ofisini kwangu kudai kuwa dawa zetu zimesababisha kifo cha dada yake.",

"Baada ya hapo?",

"Niliita walinzi wamfukuze maana alikuwa akifanya vurugu.",

"Je, baada ya kusikia dai la Montana, ulifanya uchunguzi wowote kujua ni kwanini alisema hivyo?",

"Hapana, kwa sababu kila alichosema kilikuwa uongo.",

"Unataka kusema kuwa kampuni yako haijawahi kuua watu during medical trials?",

"Hap-hapana. I'm innocent.",

Reuben alibamiza meza kwa hasira, "Janat! Unathubutu kudanganya jeshi la polisi?",

Mikono ya Janat ilitetemeka. Joy alifungua faili na kutoa makaratasi yaliyobeba taarifa kamili kuhusu unyama uliofanyika mwaka 2010 hadi 2015. Zilimuacha Janat mdomo wazi. Miaka yote hii alijua kuwa taarifa hizo zilikwishateketezwa. 

"Janat, baada ya kujua kuwa kampuni yako ipo responsible na vifo vya binadamu, ulifanya uamuzi gani?", Reuben aliuliza kwa ukali,

"Nili-nili -",

"Ulifanya nini?", 

Janat hakuweza kujibu. Aliinamisha kichwa chini kwa aibu.

"Ulijua kuhusu vifo vya watu lakini hukutetereka. Badala ya kujifunza, ukatengeneza bidhaa za kike na kuziweka sokoni bila kuzifanyia utafiti. Mwishowe wanawake wanaangamia na saratani hospitalini.", Reuben aliongea kwa hasira, "Baada ya Montana kutangaza siri yako, ukaona umnyamazishe kimya milele, sio?",

"Hapana. Naapa kwa Mungu.", Janat alijibu kwa msisitizo, "Sijamuua Montana.",

"Taarifa zake zote ulikuwa nazo tokea siku nyingi. Na ulikuwa ukimfatilia kwa karibu kuhakikisha kuwa hatomwambia mtu yoyote kuhusu kilichotokea 2010. If anyone is guilty, it's you.",

Janat aliangukia magoti na kusugua mikono yake pamoja kama ishara ya kuomba msamaha, "Sikujua ni nani ametangaza na wala sikumfikiria Montana. Nilijua ni yeye baada ya waandishi wa habari kutangaza. Sijamuua Montana. I swear to God.",

"Janat, umeshatudhihirishia jinsi gani wewe ni muongo. Nitakuwa mjinga nikiamini maneno yote yanayotoka kinywani mwako.",

Reuben alimuachia uwanja Joy.

"Janat Marko.", Joy aliita,

Janat alielekezea macho kwa Joy,

"Montana aliweza kujua siri zenu wote wanne, tena siri za ndani kabisa. Tunahisi kuna mtu anayewafahamu vizuri na kumtumia Montana kama njia ya kuwaangamiza. Je, unahisi huyo mtu ni nani?", 

Janat alikaa kimya kwa muda huku akifikiria. Ghafla alikuza macho kutokana na wazo alilopata.

"Leah Shahidi.", Janat alitamka kwa uhakika,

"Leah?", Reuben na Joy waliuliza kwa wakati mmoja,

"Ndiyo, Leah. Kuanzia habari za kuwa na kipindi cha kufichua siri zetu, alikuwa na amani tele. Hata kwenye vikao tulivoitana ili kutafuta ufumbuzi, kwanza alikuwa anachelewa na hata akifika hakuonesha uoga wowote as if hakuwa na kitu cha kuficha.", Janat alielezea, "Think about it. Sisi wote tumefichuliwa siri zetu kubwa then her turn comes and Montana just reveals kuwa mume wake anamcheat? Like, who gives a shit? Tulitaka siri nzito, kila mtu ana siri nzito na Montana aliijua lakini hakuisema kwasababu Leah ndie muajiri wake.",

Reuben na Joy walitazamana kwa machale. Maelezo ya Janat ni kama yalikuwa yanaleta maana. 

***