webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

NILIWAZA NINI

Ed akasema taratibu huku mkono wake ulioshika kalamu ukizungushia duara sehemu za ripoti aliyokuwa akiisoma.

"Brother unafikiri anaweza kuwa mtu wa ndani ndie aliyefanya kazi hiyo?" Akauliza Allan

"Ninahisi hivyo, just check na Ganeteu if possible waangalie mikataba ya wafanyakazi, faili zao, na kabla ya hapa walikuwa wapi"

"Sawa, brother we will solve even this one... Hapa kuna shida moja tu ya vifaa, kuna delay sana. Na kwa Town S nimeona kuna ulazima wa kutuma timu ya The Base.. tunahitaji security measures sana"

"Mmmmmh" Ed akaguna

Allan akajua tayari bosi wake anajitahidi kutoridhishwa na mabadiliko ya ghafla ya operasheni

"Nina mawazo nayaweka vizuri... kesho tutayajadili tukifika" Allan akajaribu kuleta farijiko kwa bosi ambaye alionekana kusikia uchovu kutokana na mambo yalivyoenda

"Sawa bro. Tuonane kesho. Nitachelewa kidogo muda wa kuondoka umesogezwa dakika 40 mbele..."

"Sawa kaka, nitakusubiri..usiku mwema"

Alipokata simu, akaendelea na kupitia ripoti zile mpaka alipohisi kuchoka akinuka, mara baada ya kutoka bafuni haikuchukua muda akajitupia kitandani...

Akaangalia simu yake ambayo ilikuwa na simu kadhaa ambazo hakuweza kuzipokea ikiwemo ya Derrick mdogo wake. Bila kumsahau Joselyn...aaaah walikubaliana kuonana akakumbuka... usiku ulikuwa ushaenda sana. Nani angetaka kuamsha kelele za churaa...

Akatabasamu alipofikiria mazungumzo yake na mama yake Aretha..

"How i wish all these troubles could dissappear before our meeting on sunday" aliwaza Ed..

Siku iliyofuata asubuhi , Edrian akiwa amevalia mavazi safi ya kiofisi yaliyompa kuonekana mtanashati, aliketi kwenye mgahawa wa hoteli hii. Karatasi kadhaa zilikuwa mezani huku pembeni kukiwa na begi lililobeba kompyuta mpakato yake.

Mbele yake kulikuwa na kikombe cha maziwa kilichofuka mvuke kuonesha joto lake.., vipande viwili vya mkate, mayai yaliyokaangwa na tufaa la kijani lililokatwa kiustadi viliipamba meza... lakini kabla ya kuweka ladha tamu ya vyakula hivyo mdomoni....simu iliita..Alipoangalia, sura yake ikawa kama mtu anayekunywa dawa chungu....ni nani mwingine kama si Lyn

Baada ya salamu malalamiko ya Lyn yalianza

"Lyn....huwezi kuongea taratibu?" Ed akauliza

"Taratibu wakati hujali hata maisha yangu, wewe ni busy na kazi, umeondoka hata bila kuniambia unasafiri.. na simu uka-divert kwa Loy ndio ananitaarifu, who am I Ed?" Lyn alilalama

"Mmmmmm" Ed akaguna na kitendo hicho kikasababisha ghafla Lyn aliyekuwa akilalamika kuanza kuongea taratibu

"Babe, lakini mbona hujaniambia?"

"Lyn kama sijakwambia ni kwa sababu nilisahau, sikupokea simu zote sababu ya kazi kunikaba..ndio maana zilielekezwa kwa Loy" Edrian akaongea kwa taratibu ili kutovuta masikio ya wahudumu wachache waliokuwa wakiendelea na shughuli zao pale..

"Lakini. .." kabla Lyn hajaanza tena Ed akamkatisha...

"Lyn nitakupigia nikiwa Airport lakini kwa sasa siko mahali pazuri kusikiliza malalamiko yako"

"Oooh basi sawa Ed. Tuongee baadae.. love you"

"Okay" akakata simu. Akashusha pumzi, "ooh my God, hivi nilikuwa nawaza nini kuwa na huyu binti. Ni mwiba kwenye kidonda... nimevumilia vya kutosha" kasema Ed ambaye alihisi hamu yake ya kula imeharibiwa.... Lakini ilikuwa siku ya bahati kwake..

Alipoanza kula, meseji ikaingia kwenye simu yake ambayo ilibadilisha kabisa sura yake

"Habari ya asubuhi Rian, uko salama... sikukujulia hali, samahani.?"

What...ameniita Rian.. ametafuta namna yake ya kunirejea... I like it! Wait nawaza nini hapa... Ujumbe ulitoka kwa Aretha....

Akarudisha kipande cha mkate, akashuka simu yake na kujibu

"Salama Retha, samahani imepokelewa... niko nje ya mji lakini nitarudi leo!, umeamka kwenda chuo?"

Akaangalia simu kisha akaendelea na kifungua kinywa chake..

Mtetemo wa simu ukamshtua, tabasamu likaonekana usoni kwa Ed...

"Ndio, niko kwenye basi naelekea."

"Okay, unakumbuka jumapili?" Akaandika Ed

Huku akiendelea macho yake yaling'aa kwa matarajio ya kupokea mrejesho kutoka kwa Retha.. ooh hebu subiri sasa anamuita Retha sio Aretha na huyu Edrian amekuwa Rian ha ha ha mambo yanakimbia sana...

"Nakumbuka. Nitajitahidi...baadae Rian"