webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

NATULIA KUMUONA

Uwanja wa ndege wa A-Town ulikuwa nje kidogo ya mji, Edrian na Allan walipokelewa na dereva wa kampuni ya SGC, safari ya kuelekea Ashanti Tower iliendelea huku wawili hao wakizungumza namna mambo yalivyoendelea katika ziara ya dharura waliyofanya.

Baada ya kufika ofisini, waliendelea na majukumu huku wakisubiri wanasheria wa SGC kuwasili tayari kwa ajili ya kikao ambacho walikusudia kufanya. Wakati wa mchana simu ya Edrian iliita, alipoangalia mama yake ndie aliyempigia...akajisikia vibaya maana alimuahidi mama yake kuwa angeenda kumuona lakini majukumu yalimkamata...

"Mama nakuhakikishia nitapita leo, kuna mambo hayakukaa sawa mgodini lakini usiwe na hofu ninayaweka vyema"

"Ooohhh haya mwanangu, jitahidi umuone mama yako leo, ukishindwa zaidi kesho."

"Mama leo nitakuja, sitaahirisha, nataka pia kuongea nawe"

Edrian aliona vyema kumuona mama yake aongee nae, akatamani ajue mama yake amemkubali Aretha au la! Alipowaza hilo akakumbuka ujanja wa Lyn alipoingia chumbani kwa mama yake... "sijui alimwambia mama nini" akawaza Ed

*********************

"Mwanangu usijaribu kunificha maana niliona kwa macho yangu namna wewe na yule binti mlikuwa mnaibiana macho....nini kinaendelea maana huyo mchumba wako amenihakikishia unampenda kweli"

Edrian aliyekuwa amekaa kwenye kochi lililotazamana na mama yake, alikuna kidevu akamwangalia tena mama yake.....

"Ma, sijui nayawekaje haya mahusiano.... hebu nisaidie mama..! Lyn kwenye hisia zangu ni mtu nimekuwa nae na nimejaribu kuelewa kupenda kupitia yeye... lakini mama.... Aretha anafanya nihisi niko chuo cha kupenda.. hisia zangu kwake ni kama maji tulivu baharini mama. Natulia kwa kumuona tu, nataka nimsikie mara zote, sauti yake kama wimbo masikioni. Moyo wangu unacheza kufuata melody yake..."

Mama yake alimwangalia Edrian alivyoongea.. hakutaka kuamini aliyoyasikia kwa sababu kijana wake huyu hakuwahi kuwa mtu wa maneno yote haya. .."huyu Aretha kamfanyaje kijana wangu" aliwaza kabla ya kufikiria kwa namna gani amsaidie Edrian..

"Nyakati kama hizi namkumbuka sana baba yako....angekuwepo, mwanaume anaweza kuelewa zaidi yangu" mama akaongea huku akionekana kuyazuia macho yake yasilowane machozi....

Edrian akainuka na kukaa kochi alilokaa mama yake akapitisha mkono wake shingoni.... "Mama am sorry.....usiwaze sana, nitakuelewa tu. ..baba alikuamini wewe kuwa unaweza."

Mama yake akatabasamu na kumwambia.... "mimi sijui mlikutana wapi na Lyn.... na kama hutaki kuendelea naye uwe gentleman enough kuweka sababu ya msingi kwa nini unataka kumuacha"

Edrian akawaza sababu ya kumuacha Lyn... "mama inawezekekana sababu zangu zikawa zimeegamia kwenye tofauti yake na Aretha kitu ambacho sitaki kukifanya. ..lakini ninaamini ninavyojisikia kwa Aretha ni tofauti kabisa. Sijawahi kujisikia hivi."

Ed ambaye wakati huu alitoa mkono wake shingoni kwa mama aliangalia chini kwenye zuria huku mikono ikiwa kidevuni! Hakutaka kumwambia mama yake kuwa Lyn ni binti wa adui wa kampuni yao.. anamjua mama yake angeweza kumuuliza Lyn iwapo angekuja jumamosi na angeharibu mchakato wa 4D..

Mama hakujua anamsaidiaje mwanae. .. muda mrefu alitamani kumuona mwanae akiwa na uhusiano na mwanamke kama hatua za msingi kuelekea ndoa. Edrian amekuwa mtu wa kazi sana na hata kutojali uhusiano na mambo ya ndoa. Aliona walau apate ushawishi wa kuwa na familia yake.. sasa kaanza kuona hilo wazo linamuingiza mwanae kwenye wakati mgumu...

"Mwanangu, mimi siwezi kukupa njia iliyonyooka katika maamuzi ya nani anakufaa au nani hakufai... ila kama una sababu kidogo inayokuzinga kuwa na Lyn, mwambie" mama akaendelea

"Uhusiano mwanangu ni hatua ya kwanza kuelekea ndoa, haimaanishi kwa sababu umehusiana nae ndio awe mkeo hata kama umegundua mambo ambayo unajua huwezi yavumilia kwake!"

"Sasa kwa habari ya huyu Aretha, una muda gani unamfahamu?"

"Wiki tatu" akajibu Ed

"Haaaaaa kumbe, basi hujamfahamu Aretha. Hebu mpe muda umfahamu.... na kama una hakika yeye sio sababu ya kuvunja uhusiano wako na Lyn, mfahamu taratibu bila kumwambia malengo yako. .ukifanya hivyo utamlinda na mwenzie ambaye aweza mchukia kwa kudhani amemnyang'anya tonge lake"

Edrian aliyekuwa ameinama akashusha pumzi.....

****************

Unaposoma usisahau ku-like, ku-comment na ku-vote... tuwezeshe webnovel kuona lugha ya kiswahili ni lugha kubwa na inawatumiaji wengi