webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

MIMI NI NANI KWAKO?

Akameza mate Ed, akafikiri njia rahisi ya kumuelezea Aretha,

"Njia ya kukufikisha ni rahisi ikiwa tutaingia kwa njia hii ili nami niweze kufika nyumbani mapema" akaeleza Ed na kumfanya Aretha kukubaliana naye, "ooooh basi sawa, sijazoea barabara hii"

"Utazoea kama una gari" Joselyn aliyekuwa akiangalia simu yake akasema kwa sauti ya chini.

Aretha hakusikia vyema lakini sentesi hiyo ilisikika vyema kwa Edrian ambaye ghafla akaongeza mwendo na kufanya wanawake hawa wamuangalie kila mmoja akitafsiri kivyake.

Aretha aliangalia majumba ya kifahari waliyoyapita kwenye mtaa huu, mpaka gari lilipopunguza mwendo na kuingia mbele ya geti kubwa kisha akasimama. Joselyn alibaki amekaa akitarajia Ed amfungulie mlango. Ed alishuka na kuelekea upande wa pili wa gari, akafungua.

Joselyn akafurahi na kushuka kwa madaha akimuaga Aretha..

"Nimefurahi kukuona Anitha"

"Mmmmm" Ed aliguna na kufunga mlango, akashika mkono wa kushoto wa Joselyn kwa nguvu na kutembea kuelekea getini huku Lyn akijaribu kujinasua maana alisikia maumivu...

"Next time Lyn...if there will be, hautaonesha tabia kama hiyo kwa wageni wangu. Never!" Sauti ya Ed ilikuwa na mitetemo ya hasira. Na hakika tangu Joselyn aanze kuzungumza wakiwa kwenye sherehe Ed alijawa na hasira lakini hakutaka kuionesha mbele ya wageni na hasa mama yake.

"What? So what? Yaani unataka nikae kimya wakati uko na mwanamke wako eeeh? Au waniona mjinga"

Ed akauachia mkono aliposikia geti likifunguliwa, kisha akainama kwenye sikio la Lyn na kusema "Read well my profile, usinijaribu" akampa ishara ya asante mlinzi na kurudi kwenye gari.

Alipopanda akashusha pumzi, "Aretha samahani nimekuchelewesha kwa dakika chache, nitakupeleka sasa"

"Aamh...a..Sawa!"

"Moon Street, house number..?" Akauliza Ed ambaye alikuwa busy na usukani akigeuza gari..

"13 lakini..." akajibu Aretha..

"Hakuna lakini Aretha. Am taking you home" Ed akamkatisha kwa kujua anataka kumwambia si lazima afike nyumbani kwao..

Kimya kilipita huku gari ikikata mitaa ya watu maarufu hadi aliporudi barabara ya Avenue. A-Town iling'aa sana wakati huu wa usiku, taa katika majengo marefu ziliufanya mji kuonekana vyema.

"Aretha" Ed alivunja ukimya na kumuita binti huyu ambaye macho yake yaliangalia nje.

"Emmmm" akaitika. Edrian alitumia muda huu kuangalia kama anamwangalia na kwa ghafla macho yao yaligongana kwenye kioo cha ndani. Aretha akayarudisha pembeni haraka.

"Kwa kiasi gani unamfahamu Derrick?" Edrian aliuliza huku viganja vyake vikikamata usukani. Aliuliza swali ambalo majibu yake aliyahofia.

"Aaammmh.. namfahamu tu. I... mean aaah kama rafiki" Aretha alisita sita akifikiri aelezeje.

"Rafiki wa aina gani?" Hakuwa na uvumilivu tena, Ed alitaka kujua... mtetemo wa sauti yake ulibeba msisitizo mzito wa kutaka kujua..

"Kama... aaaah.. kama ulivyo wewe" Aretha akajibu huku akijitahidi kutoangalia kioo cha mbele alijua Edrian atakuwa anaibia kumuangalia..

Edrian akainua macho na kuangalia kwenye kioo "mimi ni nani kwako Aretha?"kisha akarudi kuangalia barabarani..

Aretha ambaye hakutarajia swali lile akapata kigugumizi.."wewe ni aaah..mh. .ni rafiki yangu...wa...."

Kabla ya kumalizia Ed akafunga breki kwa ghafla na kusababisha Aretha aliyekuwa nyuma, alinusurika kujigonga kwenye kiti kilichokuwa mbele yake, mkanda ndio ulimsaidia.

Gari ndogo iliingia ghafla mbele ya gari ya Ed kabla ya kishiria kumruhusu, hii ikapelekea Ed kufunga breki ya ghafla na kusababisha gari iliyokuwa nyuma yake kuigonga gari yake.

"Are you okay, Aretha?" Ed akauliza huku uso wake ukiwa na wasiwasi mwingi.

"Niko, sawa, sijui wewe? Ni nini kimetokea?" Akauliza Aretha huku akitaka kushuka...

"No no, subiri nije Aretha." Ed akashuka kwenye gari huku honi za magari mengine zilisikika wakitaka njia waendelee na safari zao. Akafungua mlango wa upande wa abiria na kuwasha taa akamkagua Aretha kama mama amkaguavyo mtoto akianguka.

"Ed, am okay, usiwe na wasi wasi" Aretha akasema kwa aibu baada ya kuona Ed akikagua hadi miguu.

Aliporidhika akamruhusu Aretha ashuke na wakati huo dereva wa gari iliyomgonga kwa nyuma alisogea alipokuwa..