webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

MIKONONI KWA ED

Kwa upande mwingine Joselyn alijua ni nafasi pekee ya kumuonesha Aretha, huyu Edrian ni nani kwake. Naye akasimama kuonesha kuwa tayari kuondoka. Hata kama asingesimama bado Ed angemsubiri maana alijua anawajibika kumrudisha nyumbani. Wageni wengine walikuwa katika mazungumzo na wachache walianza kuondoka..

"Mama, asante kwa jioni ya leo" Edrian alisema huku akimwangalia mama yake kisha akaendelea

"Nakutakia afya njema. Naomba niwahi ili nipumzike mapema. Nitakuja ndani ya siku mbili."

Akamgeukia Coletha, "Coletha asante kwa maandalizi mazuri, you are the best"

Coletha akaachia tabasamu

"Niwatakie usiku mwema" akasukuma kiti kwa nyuma na kuelekea alipo mama yake. Akambusu kichwani na kuondoka huku akimpa ishara Allan amuone..

Wakati huo Aretha naye alimshukuru mama na Coletha akainuka kuondoka,

"Jumamosi dia, usisahau nitasubiri" mama yake na Edrian alimkumbusha.

Derrick aliongozana na Aretha akimuomba amsamehe kwa kuwa hatoweza mrudisha. Aliendelea kumhakikishia kuwa atakuwa salama akienda na Ed na si kuchukua usafiri binafsi huku akimuonesha kuwa usiku umeenda. Alipoona Aretha hakubaliani na hilo, akatoa simu na kumpigia mama yake akimuomba amkubalie Aretha kuletwa na Edrian. Mrs Thomas alikubali huku akimpa onyo ikiwa lolote litampata binti yake yeye atalaumiwa.

"Mama, Retha yuko salama, na atakuwa salama mikononi mwa kaka yangu."

Aretha alimwangalia Derrick kisha akamwambia

"Najua kuna jambo unalificha Derrick lakini nikijua ukweli utakuwa adui yangu!" Akasema kwa sauti yake ya upole lakini alikuwa anajisikia vibaya kwa namna aliyoiona kati ya Derrick na Joselyn..

"Hakuna baya Retha" akaachia tabasamu na kumshika mkono kuelekea kwenye gari la Ed, ambapo alimuona Ed akiongea baadhi ya ndugu ambao walikuwa nje wakisubiri kuondoka.

Pembeni ya Edrian Joselyn alisimama akimsubiri amalize kuagana na ndugu zake. Alipomuona Aretha akafungua mlango wa gari na kuingia kiti cha mbele. Na kumfanya Edrian kugeuka na kumuona Aretha na Derrick. Akaelekea kwenye mlango wa abiria akafungua kumruhusu Aretha kuingia, akafunga mlango.

"Njoo mara moja" Ed akampa ishara Derrick na wakaelekea nyuma ya gari...

"Unafanya mambo haya kwa kusudi Derrick?" Akauliza akimwangalia usoni kwa kusaidiwa na taa za nje.

"Mambo gani Bro" akauliza Derrick akiwa na uso usiokuwa na mzaha..

"Okay, nitakupigia nikifika. Usizime simu"

"Sawa bro, mfikishe salama. Nimemhakikishia mama yake. Please" Derrick akamsihi Ed japokuwa alimjua kaka yake si mtu wa kupuuzia.

"Sawa." akajibu Ed na kupiga hatua kuingia kwenye gari.

Ndani ya gari Joselyn kama kawaida alitumia nafasi hiyo kumuonesha Aretha kuwa Edrian ni mchumba wake na atamvalisha pete hivi karibuni.

"Mmmmmh" mara zote Aretha alimuitikia Joselyn kitu ambacho kilimfanya ahisi atakuwa amefanikiwa kufikisha ujumbe..

Ed alipoingia kwenye gari aliangalia nyuma alipoketi Aretha ambaye kichwa chake kilitazama nje. Akafunga mkanda na kuwasha gari, kisha akaondoka huku akifunguliwa geti na mlinzi.

"Unaishi wapi tukupeleke kwanza...Anitha?"

Joselyn akauliza baada ya kuona Ed anafuata uelekeo wa barabara ambayo ingemfikisha yeye nyumbani. Hakutaka kuwaacha wawili yao kwenye gari.

Edrian aligeuza shingo kidogo na kumuangalia Lyn kwa hasira kisha akarudisha macho barabarani akisubiri jibu la Aretha.

"Moon Street, lakini mwaweza niacha Avenue nitafika kwa urahisi" alijibu Aretha.

"Ed umesikia" Lyn akamgeukia Ed ambaye hakuhangaika kumjibu bali mikono yake ilikamata usukani kiasi cha kufanya vifundo vya mkono kuwa kama mtu aliye ulingoni.

Edrian aliendesha huku akimthibitishia Lyn kuwa hapendi kutawaliwa akili. Maana ilikuwa wazi kuwa kituo cha kwanza kilikuwa nyumbani kwao Joselyn.

Joselyn alimwangalia Ed kwa hasira akafumbua mdomo kutaka kusema lakini alikatishwa na maneno ya Ed

"Not now Lyn, stop please"

Akashusha pumzi Lyn na kuchukua simu yake.. akatulia hapo. Aretha aliyekuwa nyuma akapatwa wasi wasi alipoona wameacha barabara kuu iliyoelekea Avenue

"Ammmh... tunapita wapi?" Akauliza

Ed akaangalia kioo cha ndani kumuona Aretha akisaidiwa na mwanga wa taa za barabarani...

********************