webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

DUDE NDANI YA EDRIAN

"Goodmorning Mr Simunge" sauti kutokea nyuma yake Edrian ilisikika na kumfanya ageuke

Akamwangalia Renatha ambaye alipiga hatua kwa haraka akionekana kujaribu kumsogelea, "Goodmorning" akajaribu kutabasamu kumuonesha ukarimu lakini tabasamu likakataa

"Mbona uko huku?" akauliza Ed kwa mashaka. Alijua eneo hili la maegesho ni kwa watu wachache ambao yeye ndie aliwapa kibali cha kuegesha magari yao. Ilikuwa ni sehemu muhimu kwa wasimamizi wakuu wa idara SGC na baadhi ya wamiliki wa ofisi zilizokodishwa sehemu ya mengi hili.

"Nimeshuka kuja huku jana niliona ni rahisi kutumia lifti ya huku kuliko zile za upande ule. Watu wanakuwa wengi asubuhi" Renatha akajibu akionesha kutokuwa na hatia kwa kile alichofanya

Edrian akageuka na kuelekea ilipokuwa lifti pasipo kusema neno, Renatha akamfuata kwa nyuma huku akitabasamu,

Lifti ilipofika akatangulia kuingia Edrian, Renatha naye akamfuata na kusimama pembeni. Hakukuwa na mtu mwingine kama ilivyo mara nyingi.

Edrian alifikiri ujasiri wa huyu dada huku akishangaa maana kwa kuwa ule muda alioingia mara nyingi ni wafanyakazi wachache wanakuwa wameshafika. Kuwahi kwa Renatha kulimshangaza.

Renatha akainua macho kumwangalia Ed ambaye macho yake yalikuwa kwenye kioo cha simu yake akisoma ripoti kwenye simu yake...

Walipofika kwenye ghorofa ya kumi na tatu, mlango wa lifti ukafunguka Edrian akainua macho kuelekea ilipo ofisi yake na kuanza kupiga hatua huku nyuma Renatha akitoka kwenye lifti.

Aliyesimama mbele yao alimfanya Ed kuganda huku akimwangalia kwa hasira.

Renatha nae akabaki nyuma ya Edrian huku tabasamu lake likiwa wazi la dhihaka

"Edrian, unatoka wapi na huyu malaya!" Joselyn aliyesimama karibu na mlango wa kuingia ofisini kwa Ed aliongea huku akishiria aliyekuwa akimzungumzia

"Joselyn" sauti ya Ed ilikuwa kama muungurumo wa radi akageuka na kumpa faili Renatha, dakika ile akapiga hatua za haraka akamshika mkono kwa nguvu Joselyn. Akamvuta na wakarudi kusimama kwenye lifti wakisubiri mlango ufunguke. Joselyn aliyekuwa akijaribu kujinasua kwenye mkono wa Ed hakuweza kutoka tena macho makali yalimfanya atulie

Mlango wa lifti ulipofunguka Ed alimsukuma Lyn ndani nae akaingia na kubonyeza kurudi kwenye maegesho. Hakusema chochote lakini kwa namna uso wake ulionekana ungeweza kuona mauti ikinukia..

Walipofika kwenye maegesho akatoa funguo na kubonyeza mlango wa gari ukafunguka na akamsukumia Lyn kwenye kiti cha nyuma. Akaingia kwenye gari na mwendo aliotoka nao pale hadi sehemu ya kuingiza kadi kutoka ungeweza kudhani alibeba mgonjwa!

Alipofika geti la nje walinzi waliokuwepo walielewa hali si shwari, akakanyaga Marita na kuondoka Ashante pasipo kuongea neno lolote. Asubuhi ile kulikuwa na foleni kidogo kwenye barabara ya Avenue, lakini kwa Ed ungeweza kudhani yuko kwenye mashindano ya "Formula One" kwa namna alipishana na magari. Asante kwa SUV maana mambo yangekuwa magumu.

Joselyn aliyeketi nyuma mikono yake ilikamata kiti alichokalia, alijua amefikia kwenye kikomo cha uchokozi wake. Kule kunyamaza kwa Ed ilikuwa ni ishara tosha kuwa Ed alikuwa ni dude kwa wakati huo. Aliooona muelekeo walau moyo wake ukatulia akijua anamrudisha nyumbani. Alipotaka kuongea Edrian akaongeza mwendo.

Walipofika makutano ya Avenue na Embassy Ed hakuangalia taa nyekundu iliyowaka na akaongeza mwendo nusura wagongane na gari nyingine

"Edrian enough!" Akapiga kelele Lyn, alichoambulia ni macho makali mekundu yaliyomwangalia na kisha kurudi barabarani.

Sasa waliingia barabara iliyowapeleka mpaka geti la nyumbani kwao Joselyn. Kwa namna gari ilivyosimama nje ya geti mlinzi alishtuka na kujiweka sawa kwa kudhani kuna shambulio la hatari!

Edrian akashuka na kufungua mlango wa nyuma, akamvuta Lyn kama afutaye mtoto mdogo

"Edrian unaniumiza tafadhali" Lyn akalalamika lakini Ed hakujali alisogea hadi getini.

Mlinzi alipoona hali ilivyo akafungua geti huku akijaribu kutaka kumsaidia Joselyn, lakini alimuona Ed kwa muonekano wake hakuwa mtu mbaya. Akahisi kuna kitu kinaendelea akasogea na kuwapisha huku akiambulia jicho kali la Joselyn ambaye hakufurahishwa na kutotoa kwake msaada