webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

ANGESEMA YEYE

Wakati Ed akijiuliza akae wapi mshereheshaji akawakaribisha wageni waweze kukaa ili sherehe iweze kuanza. Ed akaketi mkono wa kulia wa Aretha, na kumfanya Aretha kuwa kati yake na Derrick..

Akajaribu kupata utulivu haikuwa rahisi kwake, akageuka na kumsemesha kwa sauti ambayo ilikuwa ya chini ambayo kwa Li asingesikia chochote.....lakini kwa Derrick ambaye alifurahia kile alichokiona kwa kaka yake alihakikisha anasikia..

"Aretha, am sorry, nimeshtuka kukuona, forgive my manners, karibu nyumbani" alinong'ona Ed

Binti wa watu kwa aibu akamtazama Ed usoni kisha akarudisha macho pembeni, "hakuna shida Ed, hata mimi nimeshtuka"

Kabla ya kuendelea mshereheshaji aliwataarifu wageni kuwa mama alikuwa tayari mlangoni kutoka na kushiriki pamoja nao..

"Wakati mama akija ndugu zangu, tutamwimbia wimbo wa "happy birthday" na wakati huo nitawaomba msimame"

Wakasimama na kuanza kuimba, wakati huo Mrs Simunge aliingia akiongozana na Coletha pembeni yake, huku nyuma Joselyn alifuatana nao. Kitendo cha kumuona mwanamke mwingine pembeni ya Ed kilibadilisha mwelekeo wa Joselyn na akaelekea walipoketi. Pembeni ya Ed, kiti kimoja kilibaki wazi, Ed alipomuona Joselyn akija huku uso wake ukionesha kwa hakika ulikuwa na maswali juu ya ugeni uliokuwa pembeni yake, hakufanya jitihada zozote kusogea, akaendelea kusimama huku akiimba kumtakia heri mama yake.

Ed alijua kabisa kuwa jioni hiyo imebeba changamoto kubwa kwa kuingiliwa na uwepo wa Aretha. Alimjua Joselyn na king'ang'anizi chake, na wakati huo alikuwa njia panda kuwaza nini Lyn atakuwa ameongea na mama yake. Muda wote aliokaa chumbani kwa mama yake aliamini kuna jambo atakuwa amelifanya kumshawishi mama yake.

Baada ya mshereheshaji kuwaruhusu kuketi, wageni waliendelea kupata vinywaji vyao huku ratiba ikiendelea.

Ed mara kadhaa aliibia kumuangalia Aretha na kwa hakujua kuwa Lyn alimfatilia,

"Ed unafahamiana na huyo mgeni" hakuweza kuvumilia Lyn akaamua kuuliza.

"Ndio" jibu fupi akajibu Ed na kurudisha macho yake mbele..

"Ni nani?" Akauliza tena

"Sio muda wa maswali Lyn, mama's birthday" akamnong'oneza kisha akaendelea kufuatilia mazungumzo ya mshereheshaji.

Lyn akalazimika kunyamaza, lakini alipotupia jicho pembeni ya Aretha, alikutana na macho ya Derrick ambaye alionesha wazi kusikia yaliyoendelea na kwa tabasamu alilompa..

"Tunatoa dakika chache kwa wanaotaka kusema chochote kwa mama, kabla hatujampa nafasi aseme hekima zake jioni ya leo.. Naomba niwape nafasi watoto wake kwanza tukianza na mkubwa" yalikuwa maneno ya mshereheshaji ambayo yalimshtua Ed ambaye akili yake ilikuwa katika dimbwi la mawazo.

Akainuka pale alipokaa, akapokea kipaza sauti kwa mshereheshaji na kumuelekea mama yake ambaye mwonekano wa leo ulimfanya awe muongo kwa umri aliotimiza.

Mrs Simunge alimwangalia kijana wake huku macho yake yalionekana kupambana kuzuia machozi yaliyotishia kumwagika, alimfanya kumkumbuka marehemu mumewe. Ed alimfanania sana baba yake kwa muonekano..

"Mrs Simunge, mama yangu, heri ya siku hii ya kuzaliwa. Nakupenda na Mungu akupe miaka zaidi. Wewe ni nguzo yangu ya mafanikio. Live long mama" Alimaliza Ed na kurudisha kipaza sauti kwa mshereheshaji ambaye akimkabidhi Linus.

"Mama, happy birthday to you, Asante kujijali muda wote hata uko nasi leo. Miaka mingi kwako mama. Your boy loves you."

Walipomaliza na Coletha, mshereheshaji akawapa wengine waliotaka kusema heri zao kwa mama huyu.

Ed muda huu alikuwa akiomba Lyn asije akachukua kipaza sauti maana hakujua nini angesema. Mshereheshaji alipouliza mara ya mwisho kama mtu mwingine alitaka kusema chochote, maombi ya Ed yalishindikana, Lyn akachukua kipaza sauti na kwa utulivu akasema,

"Happy birthday mama, nafurahi kuwa tumefahamiana kwa muda mfupi lakini nimekupenda sana. Tuombe kijana wako Edrian afanye ukaribu wetu usiwe na mipaka. Miaka mingi kwako mama"

Kama bomu lililolipuka, Ed aliinua jicho kumuangalia Lyn ambaye alilirudisha kwa tabasamu laini kisha akaketi. Aretha aliyekuwa pembeni alikuwa moja ya watu waliopiga makofi kumpongeza Lyn, asijue kuwa Edrian alitamani yale maneno angeyasema yeye.