webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

MUONESHE UKARIMU

Sherehe iliendelea japokuwa msuguano ulikuwa wazi kwa machoni pa Edrian, Joselyn na Derrick. Kama mioyo yao ingaliwekwa wazi ukweli sherehe isingeweza kuendelea.

Mrs Simunge akapewa nafasi kusema machache kabla ya kushiriki chakula cha pamoja.

"Asanteni sana wanangu kwa maandalizi haya japokuwa yanachosha aisee ila nimefurahia kuwaona pamoja... Hata sijui itakuwaje nikitoa huu urembo asubuhi.....nisije nikaukimbia uso wangu mwenyewe.." ( watu wakacheka waliposikia hivyo)

Akaendelea "Raha ya umri huu ni kuonekana mshamba kwa teknolojia na maendeleo" (vicheko vikasikika tena)

"Kweli kabisa...mkifika mtaona, kila jambo linakuwa geni na hulielewi. Sasa binti yangu anaona kama mimi napitwa sana na wakati...wakati mie naona ni kupoteza wakati... utasikia 'mama acha ushamba'. Baba yenu hakuwahi kuniandalia sherehe lakini kila birthday yangu ilipofika tuliitumia tukibishana nani anazeeka zaidi kabla ya kukamua ng'ombe na kuuza maziwa.

"Haha hahaha" ,watu wakacheka. Akaendelea

"Sherehe ilitukuta mnadani tukiuza maziwa, atakayeuza maziwa haraka huyo bado kijana. Na wakati wote nilimshinda"

Akakaa kimya kwa sekunde, kitu ambacho kilikuwa wazi kwa wanawe, alimkumbuka baba yao. Akaendelea

"Asanteni sana wanangu, nimefurahishwa kuwaleta watu wa karibu yangu. Wale wageni mjisikie huru... nauza maziwa fresh hapa, karibuni sana kila siku jumla na reja reja. Washamba kama mie tunajua kutumia wakati."

Hahaha haahaaaa (wakacheka)

"Lakini kabla sijawakaribisha kwa chakula, ninapenda mjue kuwa nilikataa wazo la keki , mbadala wake niliomba wawaandalie chakula kizuri kiasi mkitoka hapa mtanikumbuka, hivyo karibuni sana."

Baada ya maneno nayo Mrs Simunge aliinuka, Edrian akainuka kuchukua nafasi ya baba yake kumuongoza kwenye chakula, akiwaacha Lyn na Aretha. Akamtupia jicho Derrick kumpa ishara amwangalie Aretha. Hakujua kuwa Lyn aliona.

Wageni wakaelekea kwenye eneo ambapo meza mbili kubwa za chakula ziliwekwa pamoja na viti. Ed alimsaidia mama yake kuweka chakula kwenye sahani na kisha akaweka cha kwake. Wakati huo wengine nao walijiunga pale mezani na bila hiyana Mrs Simunge alimuomba Lyn akae upande wake wa kushoto huku Ed akiwa upande wa kuume.

Linus alipofika akaketi pembeni ya Joselyn na wakati Coletha akielekea kukaa pembeni ya Ed, Derrick akamuita

"Coletha unaitwa huko" akamwambia

"Na nani D" akauliza Coletha

"Na hao wapishi" alipompa hili jibu akawa kampita na nyuma yake alifuatana na Aretha. Kitu ambacho Coletha hakujua ilikuwa ni mbinu ya kumzubaisha ili asikae pale...

"Retha kaa hapa" Derrick akamwambia Aretha huku akiweka chakula alichokibeba kwenye meza. Aretha ambaye alibaki amesimama asijue akae au la maana alishuhudia kile Derrick alimfanyia ndugu yake...

"Binti yangu kaa ule chakula, hawa watakusumbua kama hujawazoea" Mrs Samunge akamshtua Aretha

Macho ya Ed yalihama kwenye sahani na kumwangalia Aretha

"Aaaah sss..sawa mama! Ha...hhappy Birthday mama!" Alisema kwa kigugumizi huku akiinama chini.

"Asante, sasa kaa ule" akamgeukia Derrick

"Huoni unavyomsumbua mgeni.. badala ya kumuonesha ukarimu mnafanya vituko wewe na huyo dada yako"

Uso wa Ed uliokuwa umerudi kuangalia sahani ya chakula uliweka tabasamu jepesi ambalo isingekuwa rahisi kuliona..

Derrick akakivuta kiti nyuma na Aretha akakaa pembeni ya Ed huku yeye akichukua kiti kilichokuwa pembeni ya Aretha. Coletha akaenda kuketi pembeni mwa Li ambaye alikuwa akiongea na Allan. Meza ilipata watu wengine wawili na kufanya idadi ya watu kumi. Chakula kikaendelea

Edrian alifurahi kuwa na Aretha pembeni lakini bado maswali yalikuwa mengi kuhusu uhusiano wa Derrick na binti huyu.

"Edrian nilishakwambia usilete mawazo ya kazi nyumbani, huwezi kula hata kidogo... hapo unatugongea tu huo uma" mama yake akamshtua

Joselyn hakuacha nafasi ya kuongea impite...

"Ni kweli kabisa mama yaani anakuwa na mawazo, wakati mwingine unaweza kudhani hana watu wa kumsaidia"

"Mmmmmmm" Ed aliguna na kumwangalia Lyn

"Uwe unamkumbusha binti yangu" mama akamwambia Joselyn ambaye kwa kusikia maneno yale aliachia tabasamu

"Sawa mama, nitafanya hivyo"