webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · 現実
レビュー数が足りません
245 Chs

MFANYE RAFIKI

Alipomwachia mikono, Joselyn akageuka kwa hasira huku akimwangalia Ed "Sitoki Edrian na hiyo picha haitowekwa sehemu yoyote nitaichoma"

Macho ya Ed yaliyokuwa mekundu kwa hasira yalimwangalia Lyn. Akamsogelea

"Kuna namna mbili tu Lyn uondoke kwa ustaarabu au nikuondoe mwenyewe"

Lyn akamkazia macho pasipo na shaka kwa yale aliyosema, "kuondoka mwenyewe sitaweza ila kama unaweza kuniondoa jaribu ni_" kabla ya kumalizia sentensi Lyn hakujua saa ngapi alikuwa begani kwa Ed ambaye hakuzungumza chochote bali akapiga hatua kuelekea mlangoni

"Niweke chini Edrian" Lyn akalalamika huku mikono yake akimpiga ngumi mgongoni. Macho yake yalibaki mezani ilipokuwepo ile picha. Ed akafungua mlango na kumshusha kisha akafunga mlango na ufunguo kwa ndani. Alifanya hivi ili kujiepusha na hisia zilizotaka kumtawala ambazo zingepelekea kumpiga Lyn. Akarudi na kujitupia kwenye kochi huku kelele za Lyn aliyekuwa akigonga mlango afunguliwe zikimfanya asipate utulivu kabisa.

"Edrian nifungulie, nione huyo Anitha amekuchorea nini?" Kitendo cha Ed kutomruhusu Lyn kuigusa picha ile ilimkera lakini si tu kumkera bali alihisi kuna kitu cha siri Ed alikificha na sio picha tu. Bila kusahau baba yake alihitaji kupata ramani ambayo inasemekana baba yake Ed, Simunge Elvis alipata ramani ya maeneo yaliyokuwa na madini. Joselyn aliamini akiipata ramani baba yake na yeye watawekeza kwenye uchimbaji na sio kama sasa walibaki wachuuzi wa madini.

Ed aliyekuwa ofisini akainuka kwa hasira ili kuelekea mlangoni lakini kabla ya kufika mlangoni. Joselyn akaachia kuugonga mlango na sauti ya Li na Coletha zikasikika upande wa pili akajua ndugu zake wameingilia kati. Akshusha pumzi na kurudi pale mezani ili aone ile picha aliyopewa na Aretha.

Akafungua kwa utaratibu lile karatasi la juu akiogopa asije akaharibu kilichokuwa kimechorwa mule ndani. Alipomaliza, macho yake yalikuwa katika mshtuko uliomfanya awe kama mtu aliyepigwa na radi....

"What" akashtuka na kusema baada ya kugundua alikuwa amepotea kifikra kwa kile alichokiona

Picha Aretha aliyoichora ilikuwa ni ile siku ambayo alienda kule kwenye eneo lake la siri kwa mara ya kwanza. Kuanzia gari aliyoitumia siku ile ilikuwa imechorwa vyema na rangi yake ya bluu iliyoelekea kufanana na nyeusi . Mahali aliposimama, mazingira yalikuwa kama yalivyokuwa wakati ule.

Kilichomshangaza zaidi ni hadi nguo alizozivaa zilikuwa ni zile zile na mahali aliposimama palikuwa ni pale pale. Hakika kwa macho ya Ed alikuwa kama ndio kwanza yuko pale. Akamkumbuka baba yake ambaye asubuhi ya siku ile aliongea nae vyemakabla ya kupatwa na umauti mchana wa siku ile. Mkono wake wa kulia ukaipapasa ile picha taratibu

"Aretha you so talented" akanong'ona taratibu

Machozi yakabaki katika kona ya macho yake, mara mlango ukagongwa taratibu, akashtuka na kufuta macho yake. Akaelekea ulipo mlango, alijipanga ikiwa angekuwa Lyn basi asingeendelea na ustaarabu aliomuonesha. Alipofungua mlango, Coletha alikuwa mlangoni

"Big B, uko salama?" Akauliza huku uso wake ukionesha kuwa na wasi wasi.

"Am okay, samahani kwa usumbufu niliowapa" akaongea kwa taratibu

Coletha aliposikia hivi akajua kaka yake alijisikia vibaya kwa yaliyotokea..akaachia tabasamu kumhakikishia kuwa haikuwa kitu kikubwa..

"Brother wala hata hujatusumbua sababu sote tunafahamu Lyn na jazba zake"

"Ameondoka?" Akauliza huku akimuangalia Coletha

"Kaka Li kampeleka, tumemwambia akupe muda utulie mtaongea vizuri."

"Mmmmmm" akaguna Ed

"Aaah tuliona ni vyema asibaki hapa ndio tukamwelezea hivyo Bro naamini hautatukasirikia"

Edrian akajisikia vibaya kwa kuwa matatizo yake yaliwaathiri pia ndugu zake

"Hamna shida baby sisy, haitajirudia tena. Nataka nipumzike huku. Nitakuona asubuhi" Ed akamuashiria mdogo wake kuwa alihitaji kuwa peke yake.

"Oooh sawa kaka. Uwe na usiku mwema" Coletha akaaga na kugeuka kuondoka

"Baby sisy" Ed akamuita, naye akageuka

"Usisahau kumpigia Retha simu na umkaribishe hapa, mfanye rafiki unanielewa eeeeh"

"Aaaah sawa Bro, nashukuru maana hata mimi natamani niende tena kwao" Coletha akaachia tabasamu la furaha kusikia kaka yake akisema hivyo.