webnovel

sehemu ya 7:jini gani

Asubuhi, Asteria alikuwa kisimani anachota maji huku akiimba wimbo wa taifa.Akiwa pale ghafla akakoswa koswa na mshale.Akageuka haraka ambapo hakumuona mtu yeyote yule.Akapotezea na kuendelea na kazi yake.Ghafla mshale mwingine ukamkosa.

"Nani?"Akauliza Asteria akiwa amechukia.Utani gani huu.

Kumbe kuna jini alikuwa kando ambaye ni shoga.Yeye ndie aliekuwa akimchezea mchezo huo Asteria.

"Sitaki huo utoto wenu tafadhali."Akasema na kumfanya yule jini avutiwe na sauti yake.Haraka akamfuata na kumuingia Asteria.Pale pale Asteria akapoteza fahamu.

Muda mfupi baadaye, fahamu ndipo zikawa zinamrejea.Kichwa kilikuwa kikimuuma mno.Hakuelewa ni kwanini.Alipoangalia chungu tayari kilisha vunjika.Taratibu akarudi ndani.

"Namba kumi na nne ulikuwa wapi?"Abrenda Akauliza baada ya kumuona.

"Nilikuwa kisimani nachota maji."Akajibu Asteria.

"Sasa maji yako wapi?"

"Chungu kimepasuka kwa bahati mbaya.Nilipata ajali kidogo."

"Sawa .Nenda mapumziko."

"Shukran."Asteria akashukuru na kwenda ndani.Akakaa kwenye kioo akijifuta futa vumbi kisha akaanza kujiremba jambo ambalo siyo kawaida yake.Akiwa anajipodoa ghafla akamuona bibi kizee nyuma yake kupitia kioo kile.Akataka kugeuka lakini akagandamizwa asinyanyuke.

"Nani wewe.."Asteria akauliza akiwa na hofu.

"Mimi naitwa jini Jinaah."

"Unataka nini hapa."Asteria akauliza.

"Nataka nikuambie kitu.Hutamani kuwa malkia wewe.?"

"Malkia!!!!"

"Ndiyo.Utaki kuolewa na Arash?"

"Asa mimi ni mtumwa wa kawaida.Nawezaje kuwa malkia? Isitoshe mimi ni mtu mweusi."

"Unaweza kuw malkia Asteria.Kwanza hujawahi kulala na mwanaume.Si ndiyo?"

"Umejuaje?"

"Najua tu.Sasa una sifa kubwa ya kuwa malkia wewe."

"Namshawishije?"

"Wewe ni mwanamke na akikataa mbake tu."

"Eti!!!Nambakaje mwanaume mimi."

"Utaweza tu."

"Mh."

"Kwaheri...naenda kutembea tembea."Jinaah akasema na kutoka haraka eneo lile akimuacha Asteria mwenyewe.

Jinaah akiwa anazunguka zunguka akamuona Osman akiwa na watumishi wawili.

"Muje chumbani haraka.Musipokuja nawakata vichwa vyenu."Akasema Osman na kuwavutia ndani wale watumishi.Jinaah akatabasamu.

"Huyu ananyanyasa sana watumishi.Ngoja nimuonyeshe kazi."Akasema Jinaah na kuingia ndani pia.Osman alikuwa akijiandaa kuwala wale watumishi lakini ghafla, yule jini akamuingilia.Pale pale akaanza kuvua nguo na kutaka za wale wadada.Wakajua utani na kumpa tena magauni yao.Osman akavaa na kujipodoa kisha akatoka mbio eneo lile.

"Shahzad unaenda wapi jamani.Rudi."Wakaanza kumkimbiza maana ni kama anajidhalilisha.