webnovel

Sehemu ya 6:Tabasamu tamu kweli kweli.¹

Arash akamshika mkono Asteria

"Twende kwa daktari."Akasema lakini Asteria akakataa.

"Sijaumia lakini..."

"Ah!Twende huku huwezi kujua."Akamshawishi na kutoka naye taratibu.Arafa na watu wengine wote wakatoka isipokuwa Abrenda.

"Dada nisaidie kuinuka tafadhali."Akasema Osman lakini Abrenda akamtazama na kumsonya kwa hasira.

"Nyoo,nyanyuka mwenyewe mshenzi wewe mbakaji."Abrenda akaondoka bila utani hata kidogo.

"Walinziiiii"Akaita Osman ali wampe msaada.

Asteria alikuwa chumbani kwa Arash.Arash alikuwa akimfuta jasho taratibu.

"Pole sana namba kumi na nne."Arash akasema.Asteria alikuwa akitetemeka mno.sio kawaida kwa Shahzad huyu kumtendea mtu wema.

"Ni mshenzi sana.Alipaswa kuuawa kabisa."Arash akasema.

"Hamna, mbona kawaida tu.Hata hivyo nimekuja kama ulivyo taka."Akasema Asteria

"Umekuja ama nimekuleta.Bila mimi ungekuja kweli."Akasema Arash akitabasamu. Tabasamu lake lilikuwa tamu kweli kweli.

"Kumbe kutabasamu unaweza!"Asteria akauliza na kumfanya Arash akae kimya.

"Ndiyo ningekuja."Akasema na hapo Arash akatabasamu.Akasimama na kusogea kabatini kisha akatoa mkufu mmoja wa thamani kubwa sana enzi hizo na kumpa Asteria.

"Yangu!!!!!"Asteria akashangaa baada ya kuelezwa kwamba ni wake.

"Ndiyo ni wako.Mbona washtuka namba kumi na nne."Arash Akauliza.Asteria hakuwa na jibu lolote lile.

"Nashukuru sana."Akasema na kumfanya Arash atabasamu.

"Naweza kuondoka sasa?"Akauliza Asteria.

"Sawa ila kabla ya kuondoka..niandalie chai ninywe."Arash akasema na Asteria akatii haraka ambapo akaenda kwenye jiko binafsi ambalo lipo chumbani kwa Arash mule mule.

Akiwa anapika mawazo yakaenda mbali kwamba Arash anamuomba wafunge ndoa mbele za watu na atakubali bila kusita.

"Aah nawaza ujinga gani mimi."Asteria akajipiga kichwani kuondoa yale mawazo.Mtumwa ataolewaje na mtu mwenye hadhi kubwa kama Arash.

Ghafla akahisi uwepo wa mtu nyuma yake.Alipogeuka macho yake yakagongana na ya Abrenda.

"Hashima yako Sultana."Akasema Asteria lakini wala hakujibiwa.

"Unafanya nini hapa muda huu?"Akauliza Abrenda.

"Shahzad ameniomba nimpikie chai...."

"Sitaki kusikia.Ondoka na usirudi tena hapa."Akasema Abrenda. Asteria akatoka mbio eneo lile la jikoni.