webnovel

Sehemu ya 4:Siku yake

Hatimaye miaka minne ikapita..

Asteria alikuwa akitimiza umri wa miaka 21 tayari mdada alikuwa maeneo ya bustani akichuma mawaridi mekundu ambayo yangetumika kama mapambo.Akiwa anaendelea na shughuli ile,ghafla akaitwa.Alipogeuka akamuona Abrenda.

"Heshima yako sultana."Akasema na kumfanya Abrenda amsogelee.

"Unajua leo ni siku gani?"Akauliza Abrenda na kumfanya Asteria akae kimya ishara ya kutojua.

"Siku ya kuzaliwa ya kaka yangu.Arash."

Abrenda Akasema na kumfanya Asteria ashtuke.Huyu mwanaume anamuogopa vibaya mno.

"Umeteuliwa kuwa mnenguaji kwenye shughuli ya leo.Utamnengulia kaka yangu.Umeelewa?"

"Lakini..."

"Hakuna cha lakini wala nini.Au hutaki?"

"Sitaki ila sina namna.Mimi ni mtumwa napaswa kutii amri."Asteria akasema ingawa roho ilimuuma sana.Hakupenda kudhalilika Abrenda akatabasamu na kutoka haraka eneo lile akimuacha Asteria anahuzunika.

"Ipo siku nitakuwa huru.Nitafanya kila kitu kwa amri yangu."Asteria akajipa moyo.

Usiku sasa, Sauti ya vikuku ikasikika kuja ukumbini ambapo kila mmoja aligeuka kujua ni nani huyo anayeingia kwa mbwembwe.Asteria ndiye aliyeingia akiwa amevalia mavazi meupe.Mpasuo ulikuwa mkubwa na kuacha mapaja yake hadharani.

Bila kupoteza muda, Asteria akaanza kucheza mbele ya Arash tena kwa mapozi mengi.Hatimaye akamaliza kucheza.

"Sogea mbele namba kumi na nne."Abrenda akamuamrisha ambapo Asteria akatii.Sauti ya vikuku ikasikika kwa mtindo fulani ambao ulimvutia mno Arash.

"Safi! Napenda sana hiyo sauti ya vikuku."Arash akasema.

"Tangu lini kaka?"Arafa Akauliza.

"Tangu Leo, yaani imenivutia mno."Akasema Arash na kumfanya Arafa acheke kana kwamba kuna kitu ameelewa.

"Baadae unitafute nikupe zawadi yako namba kumi na nne.Sawa?"Arash akasema na kumfanya Asteria amtazame kwa aibu kubwa.

"Hapana Shahzad, hili ni jukumu langu.sipaswi kupewa zawadi yoyote."Asteria akasema.

"Baadae unitafute nikupe zawadi yako."Arash akarudia tena.

"Lakini...."Kabla Asteria hajasema lolote..

"Kimya!Hii ni amri yangu.Toka hapa haraka."Arash akafoka na hapo, Asteria akatoa heshima na kukimbia kutoka pale.Mlio wa vikuku ndio ukamfanya Arash asipepese macho popote zaidi ya kwa Asteria hadi alipopotelea gizani.Arash akavuta pumzi ndefu na kutulia.