webnovel

Sehemu ya 5: Mbakaji

Asteria akakimbilia kwenye chumba cha kulala na kukaa kando ya meza ya kioo akihema mno.Wenzake wakamuuliza nini shida lakini Asteria hakusema chochote kile.Ghafla,wakasikia sauti ya mtu akilia.

"Si sauti ya Zuleykha hii?"Hadija, rafiki wa karibu wa Asteria akasema na hapo Asteria na Hadija wakatoka kwenda kuangalia nini kinaendelea.

"Sauti inatokea humu mbona."Asteria akasema akionyesha bafuni.Bila kupoteza muda, Asteria akausukuma mlango na kuingia ndani.

"Aah!"Wakashangaa kuona Osman akijaribu kumbaka Zuleykha.

Asteria akamsogelea na kumsukuma mbali Osman.

"Unafanya ujinga gani wewe?"Asteria akafoka na kumfanya Osman amtazame kwa hasira.

"Tena wewe Asteria ndio unajitia unajua na kihele hele sana."Osman Akasema na kumfanya Asteria akae kimya.zuleykha akakimbia na kumuacha Asteria ndani na Hadija.

"Tuindoke Asteria."Hadija akataka kumtoa Asteria lakini Osman akamuwahi na kumsukuma nje kisha akabana mlango!

Ndani sasa wakabaki wawili, yeye na Asteria.

"Mbona unatetemeka? Shida nini?"Osman akauliza akimsogelea.

"Niache, Arash atakua anaitafuta."Asteria akasema na kumfanya Osman acheke kwa dharau.

"Kwa lipi hasa akutafute wewe.Hebu njoo!"Osman akamvuta Asteria.Hadija na Zuleykha wakaenda kwa Abrenda kutoa taarifa.Kwa bahati nzuri wakamkuta na arafa.

"Eti nini!!!"Arafa akastuka kusikia vile.Haraka akaongozana nao akiwa na hofu kwenda kwenye tukio.Abrenda akabaki anashangaa.sio kawaida ya dada yake kuwajali watumwa katika jambo kama hilo wakati anajua kabisa Osman anapenda wanawake.

"Niache,Arash!!!!!"Asteria akapiga kelele akitaka msaada.

Arash alikuwa anapita karibu na pale ambapo akasikia sauti ya Asteria kwa mbali.Haraka akaifuata.Osman alimziba mdomo Asteria ili asimuumbue.Arash hakusikia kitu chochote hivyo akageuka atoke lakini..

"Arash nipo humu ndani!"Asteria akasema baada ya kufurukuta.Arash akageuka na kuupiga teke mlango.Akamvaa mbakaji huyu bila kuuliza na kuanza kumpiga kwa hasira.Kina Arafa wakawasili na kukuta mtu akipewa kipigo takatifu.

"Kaka inatosha muache."Arafa akambembeleza Arash ambaye akatulia.Asteria alikuwa kajikunyata ukutani akilia.Arash akamsogelea kisha,akavua joho lake na kumvesha Asteria kumsitiri.

"Pole sana namba kumi na nne, Asteria wangu."Arash akasema na kufanya watu wote washangae.Sio kawaida ya Arash kumjali mtumwa kiasi hiki tena kamuita na jina badala ya namba.Mh