webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · realistisch
Zu wenig Bewertungen
245 Chs

UNISIKILIZE ZAIDI

Alipomuona Aretha akikimbia chooni, Edrian akatabasamu na kurudisha macho yake kwenye simu.

"I love her" akaandika kwenye simu yake kisha ujumbe akautuma.

Dakika kumi zikapita na Aretha hakutoka tangu alipoingia chooni. Edrian akapata wasi wasi akainuka na kusogea ulipokuwa mlango akaita

"Retha"

"Aaahmm" sauti yake ikasikika

"Unahitaji msaada?" Akauliza kwa wasi wasi

"Aah hapana.. nimemaliza" akajibu Aretha.

Ed akatabasamu, kisha akarudi kuketi akafungua simu yake akampigia Allan, wakati akiongea, akasikia kitasa cha mlango ukifunguka akielekeza macho kumwangalia Aretha ambaye alitokea kichwa chake kikiwa kimeinamishwa asiweze kumtazama Edrian usoni

"Basi nashukuru Allan. Nitakuwa ofisini hapo mapema kesho. Tutaongea. Jioni njema." Akamaliza Edrian kisha akainuka na kusogea alipokuwa amesimama Aretha, lakini yeye akamkwepa na kuelekea mlangoni

"Retha, please stop. Hakuna cha kuogopa, Dokta Brianna alihusika na kila kitu sio mimi" Edrian akamwambia

"Uumhh. Kweli?" Akauliza Aretha huku akiangalia pembeni isipokuwa kwenye macho ya Edrian

"Njoo Retha!" Edrian akamwambia huku akiachanisha mikono yake

Aretha akapiga hatua za taratibu hadi alipofika karibu naye, "ulimwambia mama?" akamuuliza

"Niliongea nae lakini sikumwambia tukio hili ila anajua kuna dharura tuko hospitali. Nataka nikaongee nae mwenyewe." Edrian akamwambia kisha akamshika mabegani

"Retha, sitakuacha, kwa sababu kuna watu wanataka nikuache. Na kuna watu wanataka uniache, niahidi hautaniacha"

"Eeehmm, aa... kwa nini unasema hivyo?"akauliza Aretha huku akijitahidi kumtazama Ed usoni lakini hakuweza sababu ya kuwa na soni nyingi kila alipofikiria hali aliyokuwa nayo kufahamika

Kwa sababu ndani ya siku mbili tumepata changamoto ambazo pasipo kutumia busara tungetofautiana. Ni ombi langu, kama ulivyoniahidi kunisikiliza sasa naomba unisikilize zaidi" Edrian alipomaliza hakusubiri Aretha aongee chochote akamvuta na kumkumbatia huku mikono yake ikimpapasa mgongoni.

"I love you Retha" akamwambia kisha akambusu kichwani

"Rian" Aretha akaita kwa sauti ya chini

Akamrudisha nyuma kidogo na kumwangalia, Aretha akainua macho yake yakakutana na yale ya Edrian

"I love you Rian. I really do" machozi yakatiririka kwenye macho yake. Alichojua katika maisha yake sasa nje na masomo yake ni kumpenda Edrian. Kwa Aretha ni ulimwengu mpya ambao aliuona wa pekee kutoka katika macho ya Ed.

Edrian alihisi damu katika mwili wake ilikimbia sana tofauti na awali. Akamshika shingo Aretha na akashusha midomo yake kwenye ile ya Aretha ambayo ilimpokea kwa furaha. Simu ya Edrian ikaita, wala hakujali alijiachia katika busu lile na Aretha. Mikono yake ilimshika vyema kiunoni na taratibu ilianza safari kuelekea ndani ya blauzi. Aretha muda huu aliachia miguno laini ambayo ilimchanganya zaidi Ed, mikono yake ilimshika mpaka pale alipohisi kuzidiwa na joto lilioanza kuumbika tumboni kwake

"Rian" Aretha akamuita kwa sauti dhaifu, mara Ed aliposikia akatoa mdomo wake uliokuwa ukimbusu shingoni, akashusha pumzi.

"Sorry Retha" akarudi nyuma kisha akageuka haraka na kuingia chooni.

Simu ya Ed iliendelea kuita, Aretha akasogea kuangalia kwenye kioo, akaona ni Derrick, akasogea pembeni akajiweka vyema huku akijiangalia namna nguo zilivyomkaa vyema hadi viatu

"Utadhani alinipima mbona kila kitu kimenitosha" akawaza.

Edrian alipofika chooni akainama kwenye karo la kunawa mikono. Akafungua maji na kujimwagia usoni kisha akainua macho na kujitazama kwenye kioo

"That was too close"

Akajiweka vyema kabla ya kusikia sauti ya Aretha ikimuita apokee simu. Akafungua mlango na kuelekea aliposimama Aretha akamkabidhi simu, akapokea na kuzungumza na Derrick ambaye alimfahamisha kuwa wameshampeleka Charlz nyumbani.

"Njoo nyumbani, utalala hapo kuna mambo ya msingi nataka tuzungumze. Baadae" akakata simu. Akampa ishara Aretha waondoke

"Rian, asante kwa kunistahi na kuendelea kunipenda" Aretha akamwambia alipokuwa akimsogelea

"Asante pia." Ed akatabasamu na kumuelekezea mkono ili amshike.

Aretha akampa mkono na kwa pamoja wakatoka mle ndani huku nyuso zao zikitabasamu.