webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Realistic
Not enough ratings
245 Chs

ALLAN NA RENATHA

Allan alipopigiwa simu na Edrian akimfahamisha kuwa yuko nje kiofisi, akainuka na kuelekea ofisini kwa Loy ili kupata taarifa ya ratiba zote muhimu zilizobaki.

"Bosi ameondoka kwa haraka hadi amenitisha unadhani kila kitu kiko sawa?"

Loy akamuuliza Allan

"Wewe ndio katibu muhtasi wake kwa nini haujui?" Akauliza huku akimtazama na kutabasamu

"Hahaha siwezi kujua ila alipotoka alikuwa anaongea na simu kwa wasi wasi na hasira. Huyo aliyemuudhi atakutana na kimbunga"

Allan akacheka kisha akarudi ofisini kwake baada ya kupewa ratiba iliyobaki ya Edrian.

Akabonyeza simu ya mezani

"Renatha, nakukumbusha saa kumi na moja, 'we have a deal" akaongea kwa furaha

Akakata simu na kuendelea na kazi mpaka ulipofika muda wa kutoka. Akachelewa kwa muda mfupi ili kumalizia mambo ya msingi ambayo yalitumwa kwenye barua pepe yake dakika za mwisho.

Renatha akamsubiri kama ambavyo alimuomba amsubiri kwenye eneo la mapokezi la kampuni.

Allan akatoka akiongozana na Loy, walipofika pale Renatha akainuka, mara zote hupenda kuvaa sketi, na leo alivaa sketi penseli nyeusi na blauzi nyekundu, kweli alipendeza huku miguu yake yenye ujazo mzuri ikipendeza kwenye kiatu cha kuchuchumia chenye rangi nyeusi.

"Pole sana utakuwa umenisubiri sana" akamwambia Allan huku akimsogelea

"Sio sana Mr Aĺlan ni kawaida tu" akajibu Renatha huku macho yake yakimuelekea Loy na kisha Allan

"Loy alipoona jicho lile akatambua alikuwa akiulizwa nini, aah bosi siku njema. Jioni njema Renatha"

Allan akatabasamu "tunaweza kwenda?" Akamuuliza Renatha ambaye akitikisa kichwa kukubali. Akainua mfuko uliokuwa pembeni yake wakaelekea kwenye lifti ambayo iliwashusha mpaka eneo la maegesho. Wakaingia kwenye gari ya Allan, na kuondoka jengo la Ashanti

Viwanja vya Don Bosco ambapo Allan alikusudia kumalizia makubaliano yake na Renatha vilikuwa nje ya mji mwendo wa dakika arobaini na tano.

Renatha akamuangalia Allan ambaye alikuwa makini barabarani,

"Mr Simunge alipata udhuru naona, vipi kuna usalama?" Renatha akauliza huku macho yake yakiangalia mandhari ya nje

"Alipata dharura nje ya ofisi. Yuko salama na atakuwepo kazini kesho. Unamjali sana brother." Allan akamjibu

"Kujali ni tabia yangu." Renatha akajibu

"Na mimi nisipoonekana huwa unaniulizia hivyo hivyo eeeh!"

"Aaahhhm" Renatha akashtuka na kumgeukia Allan ambaye alicheka baada ya kumuona uso wake katika kuchanganyikiwa kwa swali

"Unaweza kuniulizia na mimi kama unavyomuulizia Bro Ed!!"

"Naweza. Kwa nini nisiweze?" Akauliza Renatha na kurudi kutazama nje

"Basi nitafurahi kusikia ukiniulizia na kukosa raha usiponiona" Allan akamwambia huku tabasamu lake likichanua mdomoni kwake na kumfanya Renatha aliyegeuka kumtazama kumezwa nalo.

"Nitafanya hivyo" akajibu Renatha na kujiweka vyema kwenye kiti

"Usilale halafu nikakushinda ukasingizia usingizi sawa eeeh!!" Allan akamtania

Renatha akavuta kiti kwa nyuma kidogo na kuegama "mchezaji yoyote yule ushindi wake unategemea namna anajali afya yake. Nahitaji kupumzika kwa dakika kumi na tano" akamwambia Allan

"Ooooh basi sawa kocha!!" Allan akafungua radio kusikiliza muziki

"Tafadhali zima, siwezi kulala na kelele"

Allan akazima, "sasa unataka niongee na nani kama wewe unalala na redio hutaki niwashe eeeh!!" Akalalamika huku mdomo akiuweka kama mtoto aliyezira kula

Renatha akamwangalia kisha akarudi kulala kwenye kiti. Allan akaamua kuendesha gari huku akitabasamu lakini maswali mengi yaliendelea kufichika ndani yake kuhusu Renatha

Anataka nini kwa Brother.?

Anachokitaka ni kwa ajili yake au?

Allan akaendelea peke yake barabarani huku Renatha kama alivyosema alilala usingizi.

"Tumefika Renee" akamuita taratibu mara alipoegesha gari kwenye maegesho ya viwanja vya Don Bosco hapa A-Town.

Renatha akaamua na kujinyoosha. Akachukua mfuko wake na kushuka garini. Allan aliposhuka akapiga hatua mpaka aliposimama Renatha akamwelekeza sehemu za kubadilishia nguo za wanataka.

Renatha akaondoka huku akajinyoosha. Allan naye akaelekea upande wa wanaume kwa ajili ya kubadilishia nguo zake.

Baada ya dakika chache walikutana pale walipoachania.