webnovel

CHAPTER 9

Babra alifungua mlango kwa nguvu na kuingia ndani ya nyumba ya Leah. Ingawa jua lilikuwa kali nje, ndani kulikuwa giza kutokana na mapazia kutokufunguliwa. Alipatwa na wasiwasi mkubwa; kwanza, kutokana na kipindi kilichorushwa hewani masaa machache yaliyopita. Pili, Leah kutokuonekana kazini na tatu, Leah kutopokea simu zake. Alihofia kuwa bosi wake anaweza kuwa amejidhuru.

"Boss.", Babra aliita kwa pupa huku akipiga hatua mbele, "Ni mimi Babra.", alisema.

Akiwa anaelekea kwenye ngazi, alitupa jicho sebuleni na kumuona Leah ameketi kwenye kapeti, miguu akiwa ameikunja na uso wake ameulaza juu ya magoti. Bado alikuwa amevaa nguo zake za kulalia za tokea usiku uliopita.

Haraka, Babra alijongea sebuleni.

"Boss?", Babra aliita lakini Leah hakuitika.

Babra aliweka mkono wake begani kwa Leah na kumtikisa kidogo. 

"Boss?", aliita tena, kimoyomoyo akiomba bosi wake awe mzima, "Boss, it's me.",

"Najua.", Leah alijibu bila kumuangalia.

"Asante Mungu.", Babra alivuta pumzi, "Nilihisi umefanya uamuzi wa kijinga.",

"Why?", Leah aliuliza.

"Kipindi kilikuwa hewani leo kwa mara ya mwisho. Amekuongelea wewe.",

"I see.",

"Umesikia alichosema?",

"I don't care about that.",

"Sasa mbona upo hivyo? Umekaa kinyonge, kazini hujaja, simu zangu hupokei. Hujui kama umeniogopesha?",

Leah alikaa kimya.

"Ni kweli kwamba Paul amekupa talaka?",

Leah alinyanyua kichwa na kumtizama Babra kwa haraka. Uso wake ulivaa alama ya kiulizo, "Umejuaje?", aliuliza kwa mshangao,

"Kwenye kipindi, mtangazaji amesema hilo pamoja na vitu vingi zaidi.", Babra alijibu.

"Vitu gani?",

Ilibidi Babra amsimulie kila kitu kilichoongelewa redioni. Kilichomshangaza Babra ni jinsi Leah alivozipokea habari zile. Hakuonesha mshangao wala hasira. Alikuwa ni kama mtu asikiaye habari za kawaida sana. 

"I'm sorry, boss.", alisema Babra, akihisi labda Leah alikuwa akificha maumivu moyoni.

Lakini Leah alitabasamu na kutikisa kichwa.

Leah, Suzy, Janat na Annabella hawakuonekana ofisini wala nje ya nyumba zao kwa muda wa wiki moja. Ni kama walikuwa wamejificha mbali na macho ya umma.

Mtaani bado habari nyingi zilikuwa zikiongelewa kuhusu wote wanne. Kura zilikuwa zikipigwa na wananchi kuhusu nani asamehewe na nani aadhibiwe. Nchi ilijigawa kimakundi; wale waliosulubu na wachache waliotetea. Wengi walituma maombi kwenye stesheni ya Faraja kutaka kumtambua mtangazaji yule aliyeleta joto nchi nzima ya Tanzania, lakini maombi yao yote yalikataliwa kutokana na sababu za ulinzi na usalama wa mtangazaji yule.

Jumatatu asubuhi, mwezi November, tarehe 12, Leah alirudi kwenye macho ya umma. Tangia gari lake lipaki na yeye kushuka na kuingia kwenye jengo la ofisi yake, kila aliyemuona alisimama na kujiuliza kama ni yeye au utani. Walioweza walichomoa simu zao na kumchukua video kwa siri na kuzitupia mtandaoni. Leah aliona vyote hivyo.

Leah alionekana tofauti. Watu walitegemea angekonda na afya yake kudorora, lakini alirudi akiwa na mvuto zaidi. Alionekana mwenye nguvu, furaha, na amani. Ingawa aliona macho ya watu na kusikia minong'ono yao, hakutaka vimsumbue. 

Mchana kweupe, jua likichoma hadi utosini, redio zote na runinga zilipata habari ya ghafla;

"Mtangazaji maarufu aliyeweza kushika masikio ya kila mtanzania mwezi uliopita, hatimaye taarifa zake zimepatikana. Faraja station imeweka wazi taarifa za mwanadada huyu wa miaka 30 aliyeenda kwa jina la Montana Sabas.", aliongea mtangazaji kwenye runinga.

"Kwa habari zilizotufikia ghafla, Montana amefariki dunia usiku wa jana. Mwili wake ulikutwa leo alfajiri ndani ya chumba chake cha kupanga. Taarifa za hospitali zimethibisha kukuta sumu kwenye mwili wa marehemu na hivyo kuhitimisha kuwa Montana alichukua maisha yake mwenyewe.", habari iliendelea, "Salamu za pole ziifikie familia ya marehemu Montana na wote waliomfahamu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.",

Joto lilizizima. Nchi ilipigwa na butwaa. 

***