webnovel

CHAPTER 16

Cecy alisimama nje ya malango ya jela akiruhusu jua limchome. Upepo ulipalaza uso wake taratibu. Alikuwa huru. Miaka 20 ilipita. Sasa alikuwa huru kufanya chochote alichotaka. Hakuwa na mizigo mingi bali begi moja la mgongoni, simu na pesa kidogo ya kumfikisha alipotaka kwenda. 

Lengo lake la kwanza lilikuwa kuwasiliana na Leah ili amjulishe kuwa yupo huru. Alipowasha simu ujumbe uliingia chapu. Namba aliijua kwani alikuwa akiimba kila usiku kabla ya kulala ili asiisahau. Kwa hamasa kubwa alifungua ujumbe ule na kuusoma;

Finally upo free, ila unajua kwamba kuwa huru ni hatari zaidi? Zamani ulikuwa jela kwenye ulinzi wa polisi but now hakuna wa kukulinda. Be careful hasa ukiwa barabarani.

Cecy hakuelewa maudhui ya ujumbe. Alijaribu kuipiga ile namba lakini Leah hakupokea.

"Mbona simuelewi huyu?", Cecy alijiuliza,

Aliamua kwenda ofisini kwa Leah. Alijua ofisi ilipo na alijua daladala za kupanda hivyo alielekea kituoni. Akiwa njiani, Cecy aliingiwa na machale yaliopelekea kutazama nyuma. Kulikuwa na gari likimfata polepole. Gari ilikuwa rangi nyekundu na vioo vilikuwa vyeusi hivyo alishindwa kuona ni nani yupo ndani. Gari hiyo ilimfata bila hata kupiga honi.

Cecy aliongeza mwendo kwa woga. Kwa bahati mbaya njia nzima hakuweza kukutana na mtu wa kumuomba msaada. Alijua kusimamisha gari ile na kuuliza kwanini linamfatilia ilikuwa wazo baya. Alikamata vizuri begi na simu yake kisha kukimbia mbio. Gari ile pia iliongeza mwendo. Cecy aliongeza kasi na kukimbia bila kugeuka nyuma. Kwa mbali aliiona barabara. Alijua huko atakutana na watu na gari ile itamuacha. Matumaini yale yalimuondolea uchovu. 

Akiwa maili chache sana kufikia barabarani, gari ilimzidi nguvu. Cecy alisombwa kama kifusi na kurushwa kwenye kichaka cha pembeni. Alipotua chini alipoteza fahamu papohapo. Gari ilimuacha pale akivuja damu. 

Paul alipokuwa kazini alipokea simu iliyomjulisha kuhusu ajali ya Cecy. Alishindwa kusubiri na kufika hospitali mara moja. Mapigo ya moyo yalimwenda mbio akifikiria mambo mengi mabaya, kubwa likiwa kumpoteza Cecy kwa kifo. 

Hatimaye aliingia chumba alichokuwemo Cecy, na dunia ilisimama. Cecy alikuwa na ogo kwenye mkono wake na mguu wa kushoto. Japo kuwa hakuwa mahututi, hali yake haikuwa nzuri. Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Cecy kuwa kilema milele. 

Paul aliwahi kitandani na kuweka mkono wake kwenye paji la uso wa Cecy.

"Cecy!", Paul aliita, sauti ikitetemeka, "Ni mimi Paul.",

Cecy alifumbua macho yake taratibu na pale alipoiona sura ya Paul ni kama kitu kilifyatuka kichwani mwake. Macho yake yalifunguka kama ameona mzimu.

"Ondoka!", alisema Cecy kwa sauti ya kukwaruza,

"Cecy, siwezi kukuacha _",

"Unataka kuniua?",

"Kwanini unasema hivyo? Unaniumiza.",

"Maisha yangu yapo hatarini kwasababu yako.",

"Sijaelewa. Unamaanisha nini?",

"Mke wako, Paul, yeye ndiye kanifanyia hivi. Kanivunja mguu na mkono wangu. Mke wako anataka kuniua.",

Paul alishangazwa na maneno ya Cecy, "Unahisi Leah ndiye kakugonga na gari?",

"Sihisi, najua ni yeye. Alinitumia message leo asubuhi ya kunionya kuwa makini nikiwa barabarani. Kama unabisha chukua simu yangu. Utaiona message juu kabisa. Angalia na hiyo namba. Naamini utaitambua.",

Paul hakutaka kuyaamini maneno ya Cecy kwani kipindi hicho alikuwa na uhakika kuwa Cecy na Leah walikuwa timu moja yenye lengo la kumuumiza tu. Alihisi yale ni maigizo, mpango ambao Leah na Cecy walipanga. Lakini upande mwingine alimtazama Cecy na hali yake. 

Simu ya Cecy ilikuwa pembeni ya kitanda chake. Paul aliichukua, akaiwasha na kwenda moja kwa moja kwenye meseji. Hakukuwa na meseji nyingi, yeye alikuwa anaitaka ya juu. Kwanza aliiangalia namba na kweli ilikuwa ni ya Leah. Kisha Paul alifungua ujumbe ule na kuusoma. Ulimshtua, lakini bado alikuwa na hofu zake mwenyewe;

"Wewe na Leah mlikutana na kuongea kiundani.", Paul alisema, "Na ndiyo maana ukasema hutaki tena kuniona. Wewe na Leah ni timu sasa. Haya yanaweza kuwa maigizo.",

"Paul, embu niangalie.", Cecy alitamka, hasira ikimnyemelea, "Mkono na mguu wangu umevunjika. Maisha yangu yalikuwa hatarini, ningeweza kufariki. Ni maigizo ya aina gani hayo? Unahisi naweza kuweka maisha yangu hatarini ili mradi tu?",

"Cecy _",

"Mke wako aliniahidi kunipatia kazi na sehemu ya kukaa mara tu nitapotoka jela. Ila sharti lake lilikuwa ni mimi kuvunja mahusiano yangu na wewe, kitu ambacho nilifanya. Lakini mke wako ni muongo. Amenigeuka. Anataka kuniua!",

"Unasema ukweli au unanidanganya?", Paul aliuliza, "Kama ni kweli Leah amekusaliti mimi pekee ndiye nayeweza kukusaidia.",

"Paul, nipo serious! Mke wako ni shetani! Kaeni mbali na mimi, wote wawili!",

Moyo wa Paul uliumizwa na maneno yaliyotamkwa na Cecy. Chuki aliyokuwa nayo kwa Leah iliongezeka mara dufu. Sasa maamuzi aliyoyafanya yalikuwa ni kumporomosha Leah na vyote vilivyompatia jeuri.

Suzy aliangalia kila kona ya chumba kile cha mahojiano. Maisha yake yote hakuwahi kufika kituo cha polisi, hasa kuhojiwa kwa ualifu. Yeye alikuwa akiyaona kwenye filamu tu. Alipomaliza kuangalia chumba, aligeuza macho kwa Reuben. Alionekana tofauti na picha zote alizoziona. Tetesi zilisema kuwa ana macho ya kutisha lakini Suzy hakuona hilo. Alimuona Reuben wa kawaida sana na wala hakumtisha. 

"Suzanne, uliwahi kukutana na Montana katika pitapita zako?", aliuliza Reuben,

Suzy alitikisa kichwa, "No, lakini nilikuwa nina hamu sana ya kukutana nae.", 

"Kwanini?",

"Kwa sababu ya binamu yangu.",

"Unamaanisha Flaviana?",

"Yes.",

Reuben alihitaji ufafanuzi zaidi, "Kwanini ulitaka Flaviana na Montana wakutane?",

"Actually I just wanted my company back, so Flaviana aliniambia nikiweza kumkutanisha na Montana atanirudisha kazini.",

"Kwanini binamu yako alitaka kukutana nae?",

"Kumshukuru I guess. Montana ndio sababu ya binamu yangu kuwa huru.",

Sio Reuben tu bali hata Joy hakuelewa kwanini Suzy alikuwa akitamka maneno yale bila woga. Alikuwa huru, tofauti na wote waliohojiwa, na hilo lilimaanisha mambo mawili; hana hatia au ni muigizaji mzuri.

"Ulikuwa wapi tarehe 17, mwezi wa huu?", aliuliza Reuben,

"Kuanzia siku Montana alipotangaza habari zangu mpaka leo asubuhi, nilikuwa nyumbani kwangu, ndani. Nilitoka mara moja tu kwenda kumuona baba yangu na hiyo ilikuwa ni siku ya pili baada ya habari zangu kuwekwa wazi. ",

"Miss Suzanne.", aliita Joy, "Tumesikia mlifanya kikao baada ya Montana kutangaza ile vita. Unaweza ukatuelezea kikao kiliendaje?",

"Kikao?", Suzy aliuliza huku akijitahidi kukumbuka,

"Yes, kikao. Mlikutana wote wanne _",

"Oh, you mean that evening tea? Hakikuwa kikao per se, but yeah, unaweza ukakiita hivyo.",

"Nini kilijadiliwa?", aliuliza Reuben,

"Um, tulipeana kazi ya kumtafuta Montana na kumshawishi asirushe kipindi chake. Some of us tulikuwa tayari kumpa kiasi chochote cha pesa ili asitangaze mambo yetu, but ilishindikana. She was hard to track down.",

"Kwenye hicho kikao, wote mlionesha ushirikiano?", Joy aliuliza,

"Kusema ukweli I think only mimi, Janat na Annabella ndo tulikuwa na kihoro. Lakini Leah hakuonesha wasiwasi. Ni kama alikuwa hajali wala haogopi. Kwanza simu zetu alikuwa hapokei, alafu alikuja kwenye kikao baadae, chai ilikuwa imeshapoa nahisi.",

Joy na Reuben waliangaliana. Suzy alihakikisha kauli aliyosema Janat kuhusu Leah. Reuben hakutaka kufanya hukumu yake kabla hajawahoji wote wanne lakini mishale mingi ilikuwa imemgeukia Leah kwa sasa.

Askari alikuja kumsindikiza Suzy nje, na kuwaacha Reuben na Joy wakijadili.

"Unafikiria nini, detective?", Joy aliuliza,

"Nina swali.", alisema Reuben,

"Uliza?",

"Una siri yoyote nzito?",

Joy alifikiri kidogo kabla ya kutikisa kichwa, "Hapana.",

"Utajisikiaje nikikwambia ninajua siri yako kubwa?",

"Um, najua sina siri kubwa ila nitapata wasiwasi kidogo.",

"Why?",

"Kuna vitu taanza kufikiria ambavyo vitanifanya nihisi kuwa nina siri ambayo siikumbuki. Hilo wazo litanisumbua na nitakuomba uniambie hiyo siri ambayo mimi siifahamu lakini wewe unaijua.",

"Exactly!", Reuben alijibu kwa mkazo,

"Leah kutokuonesha wasiwasi ni kitu ambacho hakijakaa vizuri akilini. Kwanini alikuwa hana wasiwasi?",

"Na pia, kwanini Montana alifichua siri za wote lakini kwa Leah alisema vitu visivyo na msingi?", alisema Reuben,

"Mawili; either Leah knew she's innocent _",

"Au yeye ndio mastermind.",

Ghafla simu ya Reuben iliita na namba ilikuwa ngeni. Joy alikaa kimya na kumpa uhuru wa kupokea simu ile,

"Hello.", aliongea Reuben,

"Samahani, naongea na detective Reuben?", aliuliza mwanaume kwenye simu,

"Ndiyo, ni mimi. Nazungumza na nani?",

"Mimi Paul, mume wa Leah.",

Reuben alishangaa maana haikuwa kwenye karata zake kabisa. Haraka aliongeza sauti ya simu ili Joy pia aweze kusikia;

"Bwana Paul, nakusikia. Kwa nini umenitafuta?", Reuben aliuliza,

"Naomba tukutane kama hautojali. Nipo hospitali ya Muhimbili, MOI.",

"Kuna tatizo lolote?",

"Kuna mtu nataka uongee nae. Yeye atawaambia ukweli wote kuhusu Leah.",

Reuben na Joy waliangaliana kwa mara ya pili. Kuna kitu hakikuwa sawa;

"Paul, subiri kidogo; umesema wewe ni mume wa Leah, sio?",

"Ndiyo.",

"Na hapo umesema kuna mtu tunapaswa kukutana nae ili atuambie ukweli kuhusu Leah?",

"Ndiyo.",

"Ni ukweli gani unaozungumzia?",

"Ukifika na kumsikiliza utajua ni nini namaanisha. Nakuomba sana uje. Ni muhimu. Ukifika nipigie, nitakufata ulipo.",

"Sa-sawa Paul, nimesikia. Takujulisha.",

Reuben alikata simu na kukaa kimya kwa muda mfupi. Alijaribu kuichangamsha akili yake kuelewa ni nini kinaendelea maana ilikuwa kama mchezo. 

"Detective, inabidi twende.", alisema Joy, "Kuliko kukaa hapa ukijiuliza na kujijibu, ni bora twende tukasikilize.",

Japokuwa hakuwa na uhakika, Reuben alikubali.

***