DAR ES SALAAM TANZANIA.
Ilikuwa majira ya saa sita mchana katika jiji la kibiashara la da es salaam, katika wilaya ya temeke mitaa ya keko magurumbasi.
Nyumba zilizobanana, vichochoro vilivojaa wavuta bangi na wanaotumia madawa ya kulevya. Kama ungekuwa mgeni katika mitaa hiyo usingeweza kutofautisha kati ya mlango wa choo na mlango wa kuingilia sebuleni. Vyote vilikuwa Sawa sawia.
Watoto wadogo walikuwa wakicheza nje ya mlango uliotengenezwa na mabati ya aina ya msauzi na kuonesha kwamba umeunganishwa na vipande vingi vya bati visivopungua mia moja.
"Karibu sana kijana katika kilinge cha mzee mpitekule, hapa Umepika karibu sana kijana mizimu ya ndindile imekuongoza ninajua shida yako." Ilisikika sauti ya kukwaruza ndani ya chumba kimoja kilichopo ndani ya geti hilo la mabati.
"Ndiyo mzee nimekuja kwako nahitaji msaada wako katika hili linalonisumbua". Ilisikika sauti ya kike katika kile chumba chenye pazia nyeusi na nyekundu kilichokuwa na vibuyu vyenye rangi ya khaki vilivofungwa na vitambaa vya rangi nyekundu.
"Nipe kiganja chako cha mkono wa kuume" ile sauti ya kukwaruza ya mzee mpitekule Ilisikika
Kwa wasi wasi yule mwanamke alimpatia mkono wake wa kuume, uliokuwa mlaini kutokana na mafuta aliyokuwa akitumia. Kijasho chembamba kilikuwa kinamtililika, kiliambatana na woga uliokuwa ndani yake.
Alipitisha vidole vyake juu kiganja cha mwanamke yule. Na baada ya dakika chache mzee mpitekule alitikisa kichwa na kisha kutoa sauti yake ya mkwaruzo ya kutisha.
"Dada ninaona unachangamoto kubwa sana katika maisha yako, lakini usijali umefika kwa mzee mpitekule mwenye mizimu ya ndindile." Alijitapa mzee mpitekule kuonesha kwamba kipele kimepata mkunaji tena mwenye kucha za kuweza kukikuna hicho kipele.
"Ili kutatua tatizo lako inapaswa ulete kichwa cha Tai...tatizo lako ili usiweze kamatwa tena kama mwanzo ulivyokamatwa na yule kijana aliyekuacha uende alipokuweka mikononi mwake sasa amerudi tena kwa ajili ya kuhakikisha kuwa haufanikishi jambo unalotaka ufanye". Alisema mzee mpitekule kisha kumkazia macho mwanamke yule.
Alichukua karatasi nyeupe isiyokuwa na maandishi yoyote, kisha akatoa unga wenye rangi nyeusi na kuupitisha juu ya karatasi hilo. Yalianza kutokea maneno taratibu na baada ya kusambaza kwenye sehemu ya karatasi hilo alimpatia yule mwanamke asome nini kimeandikwa.
"M107" alisoma yule dada kwa sauti ya wasi wasi.
"Nini maana ya maneno haya mzee? Aliuliza huku akiwa na shauku ya kujua nini maan ya maneno yale.
"Dada kuwa makini katika siku zijazo utakutana na mtu ambaye atatambulika kwa jina la M107, katika mlolongo wa maisha yako inaonesha atakuja kuwa mtu wa hatari sana maishani mwako." Alisema mzee mpitekule
Akachukua kikombe kilichojaa maji na kutupia lile karatasi ndani ya kile kikombe.
Maji yaliyokuwa ndani ya kikombe kile yalibadilika rangi na kuwa nyekundu na wepesi wa maji ukabadilika na kuwa Damu nzito. Matukio yote yale yule mwanamke alikuwa akiyashuhudia kwa macho yake na yalikuwa si mazingaombwe kama alivozoea kuona katika matamasha mbalimbali ikiwemo ukumbi wa mlimani city unaopatikana katika wilaya ya ubungo.
"Mzee ni nini hiki? Aliuliza tena yule mwanamke na mzee mpitekule alicheka sanaa hahahaha hahahaha hahahaha kwa sauti kubwa iliyoongeza woga ndani ya mwanamke yule.
"Ni damu binti" alijibu mzee mpitekule kisha kuweka uso ulionesha kwamba jambo si jepesi kama anavofikilia.
"Sayansi ya mababu zetu haiwezi kushindana na sayansi ya mzungu, lakini hapa ni kwa mizimu ya ndindile hakuna lisiloshindikana hapa utageuka hata kuwa simba nyoka hata ukitaka kuwa kipepeo Basi utaweza kuwa mnyama wa aina yoyote". Alisema mzee ndindile na kumshtua binti yule
"Inawezekana kweli binadamu kuwa simba au kipepeo? Aliuliza yule mwanamke
"Binti hapa ni Kwa mizimu ya ndindile hivyo tambua hakuna lisiloshindikana...endapo utafata masharti nitakayo kupatia." Aliongea mzee mpitekulen na kisha kutoa kitambaa cheupe kilichokuwa ndani ya kibuyu kilichofungwa na kitambaa chekundu.
"Sharti la kwanza chukua hiki kitambaa cheupe nenda kwenye hifadhi ya Pori la kitulo, kachume Maua ya rangi ya zambarau na nyeupe kisha yafunge kwenye hiki kitambaa." Alitoa maelekezo huku akitoa dawa nyengine kwenye kichupa chekundu.
" changanya na hii dawa kwenye hii chupa uwe unakunywa kila inapotimia majira ya saa nane usiku ...kumbuka maji unayotumia lazima yawe yabaridi usitumie maji ya moto ama yenye uvuguvugu utaharibu dawa tumeelewana dada.? Aliuliza mzee mpitekule
"Nimekuelewa lakini vipi kuhusu hayo maua nitayofunga kwenye hiki kitambaa cheupe? Yule mwanamke aliuliza huku akiwa na wasi wasi.
"Kuhusu hicho kitambaa na maua utakayo yapata katika hifadhi ya msitu wa kitulo, hakikisha unaweka chini ya kitanda chako pale tu baada ya kunywa hii dawa utakayo changanya na majinya baridi. Fanya hivyo kwa muda wa siku saba siku ya nane utakachokipata chini ya Uvungu wa kitanda chako niletee hapa kilingeni". Alisema kwa sauti yenye mkwaruzo.
"Sawa mzee nimekuelewa , itanibidi niende katika hifadhi hiyo ndani ya wiki hii hii. Kesho ijumaa ntaanza safari ya kuelekea mkoa wa mbeya. Kufikia jumatatu nitarudi huku kuendelea na masharti ya siku saba nikikamilisha lazima nije kwako mzee mpitekule." Alijibu yule mwanamke na kutoa pesa nyingi katika pochi yake na kuweka ndani ya kibuyu kilichokuwa kimekatwa na kuwa na Muundonwa bakuli.
Like it ? Add to library!
Have some idea about my story? Comment it and let me know.