webnovel

wapi?

Taratibu akauweka mkono wake juu ya mkono wa Ecca.

"Unataka kufanya nini?" Akauliza Ecca.

"Kukutibia ."

Ecca akatulia lakini ghafla akajikuta akipata wazo.Vipi kama Alex atagundua kua Nora amemtibia ?Itakuwaje na wakati tayari ameshamwambia akae mbali na Nora?Kabla hata hajamaliza kuwaza,tayari Nora alishamtibia.

"Wakati mwingine akija uniambie.Na unieleze amekuumiza wapi tena?"

"Hamna."

"Amekugusa wap5i?"

Akauliza Nora na kumfanya Ecca alie.Akajikuta akimkombaTia akilia mno.

"Sijui nifanye nini labda.Nataka kuwa na furaha mno."

"Naelewa ."

"Lakini kaka yako alikuja hapa.....kweli ananinyima raha sana."

"Kwanini?"

"Hataki niwe karibu na wewe ndio maana sitaki uwe hapa.Anaweza kuniuwa kwasababu hiyo....."

Ecca akazidi kulia huku akimkombatia vizuri mno Nora.Sasa kumbe kuna mtu alikua akiwatazama.Isitoshe aliwachora baadhi ya matukio.Baada ya kuridhika akaondoka kwenda kupeleka taarifa kwa Alex.

"Ondoa shaka.Nimekuja kukuletea mwaliko kesho uje kwenye kasri kwaajili ya sherehe.

Nora akampa kadi Ecca ambaye akaipokea.Moyoni aliwaza namna ya kumuweka Alex mbali ya Ecca.Alitaka Ecca ammiliki yeye tu tena kwa amani.

Barua zilisambazwa kwa ufalme za mpaka ya Mesel.Tayari Mesel na Alicia waliongea na Kuyamaliza.

"Sasa utaenda au hutoenda?" Akauliza Alicia kwa upole mno.

"Labda unishauri."

'Unaweza kunipa historia fupi labda ya ufalme huo?Tukio la utekaji labda"

"Utekaji....." Mesel akawa anajaribu kukumbuka kama kuna tukio lolote la ubakaji lililo wahi kutok. ea.