webnovel

Sehemu ya 13:Kama mdudu

Fahamu zikawa zinamrejea taratibu Zebrana ambaye kijasho chembamba kikawa kinamtiririka.Matukio ya nyuma yakawa yanajirudia kwa kasi kichwani mwake na kumfanya akurupuke kutoka kitandani!

"Shida nini wewe binti?"Mtumishi akaingia ndani kwa kasi baada ya kusikia ukelele wa Zebrana.

"Wewe ni nani?"Zebrana akauliza kwa ishara akiwa mwenye hofu mno.

"Usiniguse.."Akafoka Zebrana kwa ishara baada ya kumsukuma alipo jaribu kumgusa huku akijivuta vuta kurudi nyuma.Akapepesa macho yake pande zote kujua kama yupo sehemu anayoitambua ama la.

"Usiogope upo sehemu salama hapa.Ila twende ukaoge alafu upate chakula.Najua una njaa.Au?"Zebrana akakaa tu kimya.Yule mtumishi akataka kumuinua lakini Zebrana akawa mkali mno.

"Tafadhali tulia bwana...."Yule mtumishi akajitahidi kumtuliza bila mafanikio.Ikabidi atoke nje kwenda kutoa taarifa kwa mtu aliye juu yake.

Zebrana akainuka na kuyatazama mazingira kwa umakini.Mbona kama yuko sehemu yenye Watu tofauti pia.Akasogea dirishani na kutazama nje.Falme ilikuwa kubwa mno kuliko hata ya kina Amarilla.

Ghafla akahisi kizunguzungu cha ghafla akiwa kasimama kwenye dirisha la juu!Akataka kudondoka lakini,Akashikwa mkono na kuvutwa kutoka pale.Akajikuta akilalia kifua cha mwanaume bila kutarajia.Akabaki ametulia kwa muda asijue cha kufanya.

Taratibu..akainua sura yake amtazame ni nani hasa.Hapo macho yake yakagongana na ya mwanaume aliyevalia kinyago usoni.Nani huyu? Zebrana akajiuliza moyoni na kutaka kurudi nyuma lakini yule mwanaume akambana vizuri asichomoke.

"Twende ukaoge."Akasema yule mwanaume yaani Zolan na kumnyanyua Zebrana hadi bafuni kibishi bishi.

"Aya uoge hapo haraka sana."Akatoa amri Zolan na kubana mlango.

Zebrana hakuwa na namna zaidi ya kukaa tu.Hakutaka kuoga kwa amri ya mtu.Akajitazama na kuhisi harufu kali mwilini mwake.

"Ila kweli nanuka inabidi nioge lasivyo nitakuwa kama mdudu."Akajisemea na kutazama maji.Yalirembwa sio kidogo.Hakupata tabu kujiongeza kuwa yupo kwenye kasri masikini kama yeye.Bahati gani hii?

Taratibu akaoga na alipotoka ndani akagundua tayari nguo na chakula chake kilishaandaliwa.Akavaa haraka na kuanza kula chakula hicho.Haikuwa rahisi ila akajitahidi kula kuyanusuru maisha yake.

Kwa upande wa Annia sasa....

Amarilla alikuwa kalala zake huku akinywa kinywaji taratibu kando ya mto mzuri wa kifalme.Akiwa pale ghafla akaja Annia akiwa amevimba kwa hasira.

"Amarilla, kwanini unanifanyia hivi? Kwanini unaninyanyasa kama vile mimi sio mtu wako? Lini utajali hisia zangu ah!"Annia akalalamika lakini Amarilla wala hata hakujali chochote.Akaendelea tu kunywa kinywaji chake taratibu.

"Mimi maongeA na wewe alafu unakunywa tu kinywaji.si dharau hizi."Annia akofoka na kuipuma ile glasi ya kinywaji mbali.Hapo mwanaume akavimba na kusimama alipo Annia.Akamkamata nywele kwa nguvu na kumvuta karibu yake.

"Unanijaribu sio? Unataka nikuonyeshe ukichaa wangu sio ? "Amarilla Akauliza.Annia akabaki kimya mdomo wote kwisha.

"Nakuuliza wewe!!???"Akafoka Amarilla na kumsukuma kando Annia.

Akasimama na kutoka akimuacha Annia mwenyewe akiwa analia kwa uchungu vibaya mno.Akajuta kwa nini alikubali kuolewa na Amarilla.Lakini..atakataje tamaa kirahisi hivyo?

Akainuka na kumfuata nyuma nyuma mpaka kieleweke Amarilla alikuwa karudi nyumbani na kwenda kulala maana alichoka hata hivyo.

"Amarilla,Leo hulali mpaka unipe heshima yangu kama mkeo."Akasema Annia na kumfanya Amarilla acheke kwa kutoamini.

"Inaonekana unataka sana eeh? "Akamuuliza na kusimama kumsogelea mkewe.

"Nisamehe mke wangu kwa kutokujali."Akasema Amarilla na kumsogeza Annia karibu yake kisha akamshika kidevu na kumpiga denda.

Akamsukumia kitandani na kilichosikika baada ya hapo ni kilio kwa Annia.