Zolan alikuwa karibu na dragona akihakikisha yupo salama mikononi mwake.
Siku zikapita,Zolan akarudi kwao akiwa na Dragona.
"Nani huyu?"Akauliza dada yake na Zolan.
"Utamjua akiamka tu."Akasema Zolan.
"Sitaki mtu yeyote aingie humu ndani bila ruhusa yangu."Zolan akasema na kutoka haraka eneo lile akimuacha dada yake ambaye ni Attif akimtazana Dragona.
"Mh,kuna kitu hapa sio bure."Akajisemea na kutoka nje.
"Baba umeniita."Annia akasema baada ya kupokea taarifa za wito kutoka kwa baba yake.
"Ndiyo mwanangu... kwanza hongera kwa ndoa."
"Asante sana baba."
"Nategemea kuwa muda sio mrefu nampata mjukuu."
Annia akaguna baada ya kauli ya baba yake.Laiti angejua kuhusu alichosema Amarilla wala asingefikiria mjukuu.
"Vipi Annia,kuna tatizo?"Akauliza firauni na kumfanya Annia acheke kana kwamba kuna kitu anataka kusema cha kuhuzunisha.
"Baba kuna jambo kuhusu Amarilla."Annia Akadokeza.
"Amarilla kafanyaje tena jamani?"Firauni Akauliza.
"Kusema kweli Amarilla...."Ghafra akaguswa bega.Alipogeuka akamuona Amarilla.
"Afadhali umekuja,mkeo alitaka kusema kitu kuhusu wewe."Firauni akasema na kumfanya Amarilla amtazame Annia.
"Ulitaka kusema kitu kuhusu mimi sio? Kitu gani hasa?"Amarilla Akauliza.
"Aah, nilitaka kusema kuwa Amarilla ni anakaa sana mbali na wanawake wengine.Ni mwaminifu kwa kweli."Annia akadanganya.Firauni akacheka kwa sauti kubwa baada ya kusikia hivyo.
"Mwanangu umenifanya nicheke.Asa hilo ndio unalijua leo.Amarrilla ni mwaminifu kwako tangu awali."
"Sikudhani kama itakuwa hivi baba."
"Ndo ishakuwa sasa."
"Ndiyo."
Amarilla akamshika mkono mkewe na kutabasamu kinafki.
"Nina zawadi ya siri kwaajili ya mke wangu kwa hiyo nataka kuondoka naye."Amarilla akasema na kutoka naye haraka mpaka chumbani.Akamsukumia ndani na kufunga mlango kisha akageuka kumtazama kwa macho ya kikatili kweli kweli.
"Amarilla..."
"Sh!!!!!!"Amarilla akamnyamazisha mdomo Annia.
"We ushaongea na baba yako kwa hiyo huu ni wakati wangu wa kuongea."Akasema Amarilla na kucheka kwa dharau kubwa.