webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

WIFE

Siku ya tatu, Aretha na Ed walielekea wote kwenye kongamano ambalo kiliendelea kwenye jiji la Sydney. Na leo Edrian alikuwa ni mmoja kati ya wawasilishaji kuhusu mabadiliko ya teknolojia na uendeshaji wa migodi.

"You look so great Rian" Aretha akamwambia wakiwa kwenye gari kisha akaushika mkono wake na kuegama begani

"Mhh thank you princess. You are more beautiful when you compliment my looks hahah" akambusu kwenye paji la uso..

Britney aliyekuwa ameketi mbele pamoja na dereva akawaangalia kupitia kioo cha ndani akatabasamu. Asubuhi hii aliamua kuja kumsaidia Aretha kujiandaa baada ya kumpa taarifa. Na kwa sababu yeye ni sehemu ya timu ya SGC aliongozana nao akiwa na furaha kuwaona wawili hao.

Edrian alivaa suti ya rangi ya bluu iliyoelekea kwenye weusi na ndani aliweka shati ya bluu mpauko huku tai ya rangi sawa na ile ya suti. Kiatu chake cha rangi kahawia. Kwa mwonekano wake ni mtu mwenye hila pekee angeweka dosari. Wakati huo Aretha alivaa suruali ya rangi ya kijivu na blauzi nyeupe iliyokuwa na mikono mirefu. Nywele zake zilifungwa kwa pamoja kati kati na huku zikizungushwa na kutengeneza mduara kisha kichuma cha rangi ya shaba kikipita kati mithili ya mrembo wa kijapani. Alipendeza sana.

Walipofika kwenye jengo ambalo lilitumika kuendesha kongamano hilo wakashuka na kuelekea mapokezi na kisha wakaelekea kwenye chumba maalum ambapo wawasilishaji walikitumia kufanya maandalizi na watu wa mawasiliano.

"Goodmorning Craig" Edrian akamsalimia mmoja kati ya wanaume wanne wenye asili ya magharibi waliosimama kwenye chumba kile

"Oooh Mr Simuge, goodmorning!" Akamsalimia katika lafudhi iliyodhihirisha kukosekana kwa "nge" kulifanya jina la Simunge kutamkwa tofauti, kisha na wale waliokuwa pamoja nae wakamsalimia na macho yao yakawaelekea Aretha na Britney.

"Goodmorning Britney" wakamsalimia na sasa wakaelekeza macho kwa Aretha kisha Ed

"Oooh let me introduce you to my wife, please meet Aretha"

Ni wazi utambulisho uliwashtua wao na kumshtua Aretha ambaye wakati Ed alipomwambia angemtambulisha kuwa ni mkewe alidhani anatania tu..

"Oooh this is amazing, we were not invited" Craig akaongea kwa niaba ya wengine ambao nao walikuwa kwenye mshangao

"Hahaha patience Craig, but not yet, better start preparing yourselves soon invitation will be knocking at your door!" Edrian akawaambia wakati huo akimvuta Aretha ubavuni mwake.

"Congratulations brother, with that I'll have million reasons to travel to Town A" wakampa pongezi kwa pamoja..

Wakasogea kwenye vifaa vilivyokuwemo mle ndani huku mwingine akipokea kompyuta ya Ed ambaye alikuwa na Aretha

"Craig ni mratibu wetu kwa upande wa Amerika na Ulaya yote, na yule pale ni Joel, yeye anasimamia Masoko yetu." Ed akamwambia Aretha

"Rian.... umenikomesha eeh" akamwambia taratibu huku akifinya kidogo mkono wake

"H ahahha I kept my word, didn't I?"

Edrian akaondoka nao hadi mahali ambapo wageni walitakiwa kuketi. Waliposhuka kwenye ngazi za umeme Aretha alikuwa na mshangao wa namna ukumbi huu ulivyokuwa mkubwa. Wakaelekea kwenye viti vilivyoandaliwa kwa ajili ya wageni. Huku akisalimiana na baadhi ya watu ukumbini pale Ed hakuacha kuwatambulisha kuwa Aretha ndie mwanamke ambaye hivi karibuni angefunga nae ndoa. .

Britney aliwafurahia sana na hasa kila mara alipoona Ed akimtambulisha Aretha. Wakaketi kwenye viti, kisha Ed akamuaga Aretha na kurudi kwenye kile chumba kingine.

Ratiba iliendelea kwa saa mbili yakizungumzwa mambo mbalimbali kuhusiana na usalama katika utumiaji wa teknolojia katika uchimbaji. Baada ya hapo muongozaji akawataarifu kuwa wangeendelea na uwasilishaji wa mada, na sasa ilikuwa zamu ya Edrian.

Wakati Ed akiinuka tayari Craig alikuwa ameandaa kila kitu kilichohitajika, aliweka kompyuta yake mahali ambapo alitakiwa kusimama.

"Goodmorning everyone! As you have heard, I am Edrian Elvis Simunge of Simunge Group of Companies. We run Simunge Mines in Western part of Country T. Some of you have heard or encounter one of our product in the market, so today I will present our discovery on the usefulness of technology in mining operations"