webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

USINGIZINI

Zoezi la kupanga picha liliendelea hadi usiku sana. Beruya alionekana kuchoka sana, msaada wa Aretha ulikuwa mkubwa sana kwake. Alipozidiwa na usingizi, akalala kwenye meza na shughuli iliyobaki ikamalizwa na Aretha kwa msaada mkubwa wa Edrian.

Walipomaliza kuweka picha pamoja na watu wachache waliokuwepo wakati huo, Edrian akamwangalia Aretha ambaye alionesha kuchoka sababu ya usingizi uliokuwa ukimnyemelea.

Wakamsogelea Beruya na kumwamsha,

"Samahani sana Edrian nimewaachia wageni hadi mmemaliza" sauti ya Beruya ilitoka ikiwa na mikwaruzo

"Una usafiri wa kukupeleka nyumbani?" Edrian akamuuliza

"Ndio.. ngoja nimpigie yuko hapo City Hospital....mnaweza kwenda ili Aretha apumzike"

Wakaagana na kukubaliana kuonana baadae muda mfupi kabla ya onesho..

Edrian akaongozana na Aretha hadi kwenye lifti. Walipoingia na mlango kufunga, Ed akamvuta Aretha taratibu na kumkumbatia.

"Pole princess" akainama na kumwambia sikioni kisha akambusu kichwani.

"Mmmh" akahema kwa uchovu na kutulia kwenye kumbatio lile macho yake yakiwa mazito kwa usingizi.

Walipofika kwenye gari Aretha aliegama kwenye kiti na kuacha usingizi umchukue taratibu.

"Am sorry Rian" akamung'unya maneno mara usingizi ulipoanza kumpitia

"Eeeeh" Edrian hakusikia vyema maneno yale na alipojaribu kumuita Aretha aliitika lakini mdomo ulikuwa nzito kuongea

Wazo la kutamani kwenda na Aretha nyumbani kwake likamtembelea kichwani akaangalia simu yake ili awasiliane na mama yake, akaamuru simu impigie

"Hellow mama"

"Edrian mko salama mwanangu?" Sauti ya mama ilimfanya Edrian ajue hakuwa amelala na huenda aliketi akiwasubiri

"Tuko njiani tunarudi" Ed akamjulisha huko moyo wake ukikata tamaa ya kumuomba mama yake ruhusa aende na Aretha nyumbani kwake...

"Sawa mwanangu, ninawasubiri. Frans atawafungulia geti" mama akamwambia

"Sawa mama" akamaliza na kukata simu

"Mmmmhhh" akashusha pumzi na kugeuka alipoketi Aretha aliyesinzia, akatabasamu mara mwanga wa taa za barabarani ulipommulika

"So peaceful"akawaza

Akaendesha gari mpaka nyumbani kwao Aretha. Akamjulisha mama mara alipofika, akajaribu kumuamsha taratibu lakini Aretha alimuitikia na kurudi kufumba macho..

Edrian akashuka na kuelekea upande wa pili wa gari alipoketi Aretha mara aliposikia sauti ya kufunguliwa kwa mlango mdogo wa geti. Akafungua mlango wa gari na kumuita taratibu Aretha, lakini alijikusanya kama aliye kitandani huku akilalama kwa usingizi..

Ed akageuka nyuma baada ya Frans kumuita ambaye naye alionekana kushtuliwa toka usingizini na aliegama kwenye geti akisubiri wapite..

Edrian akarudi na kutoa funguo ya gari, akaelekea tena upande wa Aretha, akambeba kama mtoto mdogo huku kichwa chake kikiwa mabegani. Asijue afanyalo, Aretha akazungusha mikono shingoni kwa Ed. Akarudisha mlango na kufunga gari kwa swichi iliyokuwa mkononi mwake

Frans aliyesimama pembeni alivyoona kilichoendelea, akazinduka kutoka katika weweseko la usingizi akapiga hatua haraka kusukuma geti kumuwezesha Edrian kupita

"Naona kazidiwa na usingizi" Edrian akamwambia Frans

Frans akatabasamu huku akirudisha mlango wa geti lakini hakupiga hatua bali akabaki amesimama pale pale.

Edrian akaendelea mbele kuelekea kwenye mlango wa kuingia ndani. Moyoni alishukuru mazoezi yake ya kila siku maana hakupata shida kumbeba Aretha. Alipokaribia alimuona mama amesimama barazani..

Mama akashangaa kuona Edrian kambeba Aretha ambaye alionekana kuchukuliwa na usingizi mzito

"Pole mwanangu" akamwambia huku akipiga hatua kufungua mlango wakaingia ndani. Edrian akataka kumuweka Aretha kwenye kochi lakini sauti ya mama yake ikamshtua

"Njoo umfikishie chumbani kwake mwanangu..akilala Retha huwa kama mfu vile"

Edrian akageuka na kumfuata mama ambaye alimuelekeza hadi chumbani kwa Aretha. Akainama kumuweka kitandani lakini mikono ya Aretha ilishikilia shingo ya Ed kama mtu aliyeshika boya kuokoa maisha yake..

Akamuweka na kuitoa mikono shingoni, Aretha akajigeuza kitandani taratibu na kujikunja kisha maneno yakamtoka katika usingizi mzito uliomkamata

"I love you Rian"

Edrian ambaye alisimama kumuaga mama akaangalia pembeni akajifanya kutokusikia maneno yale japokuwa furaha yake ilikuwa kuu sana