webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

USICHELEWE KURUDI

"Nimekutuma kuniletea taarifa muhimu na sio wuuu wuuu zako Renatha"

"Bosi, nimejaribu kutafuta namna ya kupata funguo ya ofisini kwake bado sijapata" Renatha akajitetea mbele ya TM ambaye alikuwa na sura iliyoonesha kutofurahishwa na mrejesho alioupata

"Na hizi taarifa za mapambano yako na mwanamke wake zinanisaidia nini?" Aliuliza TM

Renatha akamwangalia Bon aliyesimama pembeni ya TM, akashusha pumzi kuonesha alivyokerwa na namna baba yake alitaka kumuendesha

"Bab..aaaah..bosi kama huniamini na namna ya utekelezaji wangu wa kazi naweza kuacha. Sio lazima njia zangu uzijue, ila kama njia zangu zaweza kuleta matokeo, niache nifanye kazi"

"Renatha" sauti kali ya TM ikasikika na kumfanya Renatha akakamae kiasi lakini hakubadili msimamo wake akamwangalia baba yake usoni huku machozi yakikaribia kumtoka. Akafumba macho kuhakikisha hakuna tone la chozi kaka litaonekana mbele ya baba yake. Akainua macho yake na kumwangalia

"Usinifundishe, na usijione kuwa na uwezo zaidi ya vile nilivyokufunza"

"Am sorry Boss" akaomba msamaha japokuwa sauti yake haikuwa na hisia yoyote ya kujutia

"Renatha muda uliokaa na faili alilokupatia Simunge hukuona dalili zozote za taarifa inayoweza kutusaidia kupata ra_" akauliza TM sasa kwa sauti ya kawaida

"Boss, faili lilibeba taarifa yangu mwenyewe na nyingine zilikuwa za kawaida"

"Taarifa yako ipi?" Akauliza TM

Renatha akagwaya kidogo akijua kitakachofuata ikiwa akisema ukweli "taarifa za ukaguzi wangu kwa idara ya rasilimali watu"

"Vitu gani uliandika humo?" Akaulizwa

"Bosi....! taarifa ya vigezo vya ajira na utaratibu kufuatwa. Sikuona makosa yoyote nikaandika ripoti yangu na kumkabidhi kabla ya kuituma wizarani" akajibu Renatha akiwa ametulia

"Na kingine?"

Renatha akalamba midomo yake na kuendelea " Hakuna kingine zaidi Bosi"

"Wiki yote na tunaenda ya pili hujajua wala kupata tetesi ya hiyo ramani?" Kulikuwa na dalili za kukasirika kwenye sauti ya TM

"Bosi, unataka niende moja kwa moja nimuulize Mr Simunge?" Renatha naye akauliza kwa kuonesha kuchoshwa na mazungumzo yale..

"Toka humu Renatha kabla sijasahau kama wewe ni binti yangu" TM akaunguruma kwa ukali na kumfanya Renatha kutetemeka

"Am sorry" akainama na kugeuka kuondoka

"My last warning you stupid girl, do what I sent you to do" sauti ya TM ilitokea nyuma yake.

Akasimama kidogo halafu akapiga hatua kuendelea mbele hata akatoka mle ndani.

"Bon" TM akamuita

Bon akasimama mbele yake, "Tafuta hiyo taarifa aliyopewa Simunge na Renatha. Ninaihitaji."

"Sawa Bosi" akaitikia Bon na kuondoka

***********************

Edrian akamrudisha Aretha nyumbani huku akimuahidi kumchukua siku iliyofuata kwa ajili ya mambo machache ambayo alitaka kuyarahisisha kwa ajili ya maandalizi yake. Aretha akamshukuru Derrick na Edrian, wakaondoka.

Edrian akaendesha kuelekea Heaven Apartment kumshusha Derrick kabla ya kuelekea kwa Captain.

"Inawezekana Bro si Martinez pekee anayekuandama. Kwa tukio la G-Town kuna mtu mwingine anahusika japo sijajua ni nani moja kwa moja. Tumejaribu kudukua simu ya huyu bwana aliyekuwa msimamizi wa mazingira, mtu alikuwa akiwasiliana naye ambaye amekuwa akimrejea kama Face B." Captain alimwambia Edrian aliyeketi mbele ya kompyuta kwenye chumba maalum walichotumia 4D

"Face B" Edrian akarudia lile jina huku akimpa ishara Captain aendelee

"Mawasaliano yao yalikuwa kwa sekunde chache sana. Tumejaribu kuingia kwenye ile namba iko 'protected'. Meseji moja ilikutwa kwenye simu yake huyu mkuu wa Idara iliyoandikwa kwa mtu mwingine kuwa "anajua anachokifanya"." Captain aliendelea

Ed akashusha pumzi baada ya kusikia taarifa ile, "Tunamuwinda Face B sasa"

Tik. .Tik ujumbe ukiingia kwenye simu ya Edrian

"Rian, asante kwa msaada mkubwa ulionionesha leo. Nimejisikia vyema. Nakuomba usichelewe kurudi nyumbani. I love you"

"Vipi Bro, your face has become warm suddenly" Captain alimtania Ed baada ya kuona tabasamu laini usoni kwake

"You know what, naenda nyumbani kupumzika. Kuna miamala utaikagua kwenye akaunti, Moze ametuma. Enjoy." Edrian akainuka alipokuwa ameketi na akaaga na kuondoka.