webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

UMEPAMBA MOTO

"Allan tafadhali usipambane na__" ngumi ikarushwa kuelekea kwa Allan lakini Renatha akamvuta pembeni na haikuweza kumpata, akamsukuma kwa teke la mgongoni na kumfanya sense kuangukia meza ambayo ilikuwa na vinywaji

Kuanguka kwa chupa zile za vinywaji kukavuta macho ya watu kuwatazama na wakati huo walinzi wakasogea. Kabla hawajasogea tena kuwashambulia kina Renatha tayari walinzi walisimama kati yao

Lakini wale walinzi walipowaona wale wanaume wawili wakawalazimisha Renatha na Allan waondoke kuwa wanasababisha fujo. Allan akatoa vile vifaa masikioni, akataka kubishana nao lakini Renatha akamvuta waondoke

"Allan please let's go"

Wakatoka hadi nje, wakaelekea kwenye gari lakini walipofungua mlango kuingia wakashangaa wale wanaume wawili wamenakuja wakiwa na wengine watatu.

"Allan njoo ukae huku" Renatha akamwambia Allan kisha akaingia upande wa abiria na kuketi kwenye kiti cha dereva. Allan akazunguka nyuma lakini kabla hajaingia mmoja wa wale wanaume yule alipigwa ngumi akazuia mlango usifunguke

Akamrushia ngumi Allan lakini akaikwepa na kuinama huku akipata mwanya wa kumrushia ngumi ya tumboni..

Alipoinama kuugulia maumivu Allan akafungua mlango na kuingia

"Wanakimbia hao" mmojawao akasema na wote wakasogea kwa haraka, lakini walichelewa maana Renatha alirudisha gari nyuma kwa spidi kali na akageuka na kuondoka. Wale wanaume nao wakakimbia kuchukua gari...

"Nisamehe Allan" Renatha akamwambia huku akikanyaga mafuta kiasi cha kumfanya Allan amwangalie

"Sawa. Tutaongea" Allan akamjibu kisha akavuta mkanda na kufunga akaegama kwenye kiti mawazo yakimchukua juu ya yale aliyomwambia Renatha

********

"D bado nini kinatakiwa kwenye hilo onesho?" Li akamuuliza Derrick wakiwa sebuleni

"Kila kitu kiko sawa kabisa. Yassin anamalizia mambo machache ya mialiko" Derrick akamjibu

"Mna uhakika wa usalama eneo hilo" akauliza

"Bro vipi kwani unahisi kuna Al-Qaida wananyemelea eneo hilo???" Akauliza huku akicheka

"D acha utani, hatutaki mambo kama yale ya Southern Pole yatokee tena eeeh?" Li akamwambia

"Hahahaha usiwe na shaka tumehakikisha kila kitu kiko sawa"

"Vizuri"

"Bro naona ukaribu wako na Beruya umepamba moto" Derrick akamchokoza kaka yake huku akitabasamu

"Unanitafuta eeeh?" Li akamwambia

"Unamaanisha Beruya aliyeko kwa mama au mwingine!!" Sauti ya Coletha ikawashtua na wote wakaangalia mlangoni

"Eeeeh wewe nawe unakuja kama mchawi, ulikuwa unanielezea usikia umbea aisee" Derrick akamwambia huku akiinuka kupeleka glasi ya juisi aliyomaliza kunywa jikoni

"Ndio nimenyata nisikie umbea D, rudi umalizie huo umbea" Coletha akamwambia Derrick kisha akamsogelea Li

"Kaka Li yaani huyo Beruya amepatana na mama balaa basi kila saa ananisema natakiwa nijifunze kwake"

'"Mmmhm basi msikilize mama na ujifunze kwake" Li akamwambia huku akitabasamu

"Aaaarghhh hadi na wewe kaka unasema hivyo mbona mimi niko vizuri tu, napika, nafanya kazi za nyumb__"

"Hadi ujisikie kufanya la sivyo uombwe" Derrick akaingia na kumkatisha

"Aiseee wewe nimekufulia nguo mara kibao halafu unasema hadi nijisikie" Coletha akalalamika wakati huo Li akacheka kisha akamshika begani Coletha

"Uko vizuri mdogo wangu. Mama anasema hayo kukutia hamasa uwe vizuri zaidi"

"Hahahha bro anakutia moyo tu wala huwezi kumfikia Beruya" Derrick akacheka na kumtania

"D mwache dada yako, wewe unakula chakula chake mara nyingi kuliko hata mimi" Li akamwambia

"Ooooh basi sawa asije akaacha hisani yake buree"

Coletha akampa ishara ya kumzomea Derrick kisha akamgeukia Li "tuendelee mlivyokuwa mnasema kuhusu huyu Ber_"

"Naenda kulala Coletha kazi kwako" akamkatisha na akaondoka haraka akiwaacha Coletha na Li

Li nae akainuka

"Mbona kila mtu anaondoka jamani" Coletha akalalamika

"Ndio usipende kunyatia maongezi ya watu Coletha utasikia yasiyopaswa" Li akamwambia huku akipanda ngazi kuelekea chumbani kwake

"Aisshshhh sasa si nimeuliza tu jamani" akajitupia kwenye kochi

"Huyu Zey atakuwa kashalala sijui" akawaza kabla ya kuingia mlango wa jikoni ili kupasha chakula moto apate kula. Leo alichelewa kutoka chuo sababu ya maandalizi ya mitihani.