webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

UMEHARIBU 'SUPRISE'

Mazungumzo kati ya Beruya, Yassin na Derrick yaliendelea. Beruya alishangaa maelezo aliyopewa ambayo hayakushahabiana na yake yaliyotolewa na Damian.

"Sijui kwa nini alinidanganya, na anaendelea kunidanganya. Aliniambia kuwa wewe na Aretha mnanilaumu kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa wa mwisho kutoka ukumbini"

"Hata mimi nashangaa sana B, najua hakubaliani na mimi mara nyingi lakini sikudhani anaweza kunitungia uongo huo" alilalama Yassin

"Atakuwa na sababu zake za kusema alichosema" Derrick akamwambia kisha akaendelea

B, unaweza kuandaa picha ndani ya wiki moja? Au unaweza kuwa na picha za ziada ulibakiza?" Akaamua kuulizia picha ili kubadili mazungumzo baada ya kuona huzuni iliyokuwa wazi usoni kwa Beruya

"Aahmm D picha zangu bora ndio hizo zilizoharibiwa" akasema kwa huzuni Beruya

"Lakini B najua ndani ya wiki moja unaweza kuchora picha za kutosha kufanya onesho. Japo najua itakuchukua nguvu nyingi lakini nakumini B" Yassin akamtia moyo Beruya ambaye aliinama akitafakari nafasi hii adhimu ambayo aliipata

"Nitajaribu, lakini sijui kama nitaweza kufanya nikiwa hapa. Nahitaji sehemu tulivu Yassin, siamini kama naweza kuendelea mazingira haya." Beruya akawaambia

"Lakini unaweza kurudi kwako, kwani bado unajisikia vibaya?" Akauliza Derrick

"Niko vizuri lakini Damian anasisitiza kuwa nahitaji dawa zaidi. Nimemkubalia lakini sinywi kusema ukweli."

"Hahaha au atakuwa anajaribu kukuongezea ugonjwa" Yassin akamtania

"Yassin, acha utani, Damian kanikosea sana. Kwanza aliniambia kaka Edrian ndie amehusika kuharibu hizo picha sababu anataka kumkomesha Aretha" Beruya akawaambia

"Haaaaaa, huyu sio mzima kabisa" Yassin akahamaki kwa hasira aliposikia

"Lakini sikuamini kabisa sababu nilimuona namna ambavyo alijitoa kumsaidia Aretha. Tuachane na hilo, kwa hiyo Aretha naye atakuwa kwenye onesho?" Akauliza

Yassin akamuangalia Derrick ambaye aliamua kumjibu Beruya, "Hapana hili ni onesho ambalo litakusanya picha zako tu."

"Lakini ujue sina pesa kwa sasa mtaweza kukidhi mahitaji yote peke yenu?" Akauliza Beruya

"B, tumepata mfadhili lakini ametuomba tusimtaje. Atasimamia onesho lote" Yassin akamwambia huku akikumbuka maelekezo ya Aretha kuwa hataki Beruya ajue kama ni yeye analipia onesho lake.

"Nitatumia ile hundi uliyompa Damian kuchangia"

"Hapana B, hiyo pesa itumie kwa maandalizi yako binafsi" Derrick akamhakikishia

Walipomaliza, wakamsindikiza Beruya hadi nyumbani kwa Damian, wakamkuta akazunguka zunguka akifuatilia wapi wakaelekea. Hawakukaa mbali na mtaa ule, waliamua kuongelea mbali kidogo ili Damian asiweze kuwasikia.

Wakaagana na Beruya huku jicho kali la Damian likionesha kutowatarajia tena kurudi pale.

***********

Aretha alipofika Ashanti Tower hakutaka kuingia ofisini kwa Edrian. Alimsubiri kwenye maegesho maalum baada ya kuwa amepewa kibali cha kuingia huko kutoka kwa mlinzi ambaye alifanya hivyo kwa agizo la Edrian.

Mara mlango wa lifti ulipofunguka Edrian aliangaza ili kumuona Aretha lakini hakuwepo. Gari zilikuwepo chache tu hivyo haikuwa kazi ngumu kumuona mtu aliyesimama akisubiri. Akapiga hatua huku wasi wasi ukiwa wazi usoni mwake.

"Retha" akaita kwa sauti tulivu, hakukuwa na majibu yoyote

Akasimama na kuinua simu yake tayari kupiga, lakini kabla ya kupiga akasikia hatua za mtu ambaye alionekana kunyata taratibu. Akageuka kwa haraka

"Aishhh umeharibu 'suprise' yangu Rian" Aretha akasimama baada ya kugundulika

"Hahaha" akacheka Ed huku akisogea aliposimama Aretha

"Nilitaka niku__" kabla ya kumaliza sentensi yake Edrian alimvuta kwenye kumbatio lake na kumfanya ashindwe kujitoa

"Siku nyingine ukinifanyia 'suprise' kama hii nitakubusu mbele ya wafanyakazi wa SGC" Edrian akamnong'oneza sikioni na kumfanya Aretha ashtuke na kuinama

"Rian bado uko o_" Aretha akataka kuongea lakini akaktishwa na Ed

"Mbona hukuogopa kunifanyia 'suprise' eeeh" Edrian akamtania huku akimgeuza na wakaelekea kwenye lifti ambayo iliwapeleka hadi ghorofa ya mwisho ambapo walipanda ngazi chache na kutokea kwenye veranda ya juu.

"Rian, umeandaa kabisa?" Aretha akauliza baada ya kuona mazingira safi yaliyoandaliwa