webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

UKINIAMINI NITAKWAMBIA

"Renatha!" Edrian akamuita huku akiangalia glasi yake yenye mvinyo.

"Edrian, nashukuru kwa kukubali wito wangu" Renatha akamwambia baada ya kushusha glasi yake

"Mmmmm" Edrian akaguna

"Najua una maswali mengi ambayo unataka niyajibu" akaendelea Renatha

"Sio maswali Renatha, swali langu ni moja tu" akamkazia macho

"Sawa. Nami nitalijibu swali lako bila shaka" Renatha akamwambia Edrian ambaye alibaki kumtazama akitarajia jibu lake alipate lakini swali jingine likaongezeka..

"Kabla sijajibu swali lako, nitakuuliza swali"

"Ikiwa mama yako na mpenzi wako watapotea ni nani hasa utaanza kumtafuta?" Renatha akamuangalia Ed ambaye alishtushwa na swali lile akabaki akimwangalia usoni!

"Najua unataka kusema utawatafuta wote, fikiri tu umepewa dakika kumi utaanza kumtafuta nani?" Akauliza tena Renatha

Edrian akamtazama kisha akatabasamu, "ukweli ni kwamba nitamtafuta mama yangu sababu najua m__" Kabla ya kumaliza Renatha akamkatisha

"Sababu sio ya msingi Edrian ila utamtafuta mama pasipo kusita"

"Renatha, unataka nini kwangu?" Edrian akamuuliza hali uso wake ukikosa ustahimilivu kabisa

"Kuna mambo hautanielewa wakati nayafanya sababu hujui msukumo nyuma ya maamuzi ya__" kabla ya kumaliza Renatha alinyamaza ghafla, Edrian akamtazama usoni kwa mshtuko uliokuwa wazi kisha akafuatilia nini kilimshtua!

Akajaribu kufuatisha macho ya Renatha, lakini kulikuwa na watu wengi kwa upande ule. Alijikaza macho akaona mwanaume ambaye hakufanikiwa kuona sura yake sababu aliketi akimtega mgongo. Akataka kumuuliza kama mtu yule ndie alimshtua au la, lakini kwa kuwa hakutaka kubadilisha mazungumzo yao akaendelea

"Una maamuzi gani unayotaka kufanya ambayo yananihusu?"Edrian akauliza baada ya kurudisha macho yako kwa Renatha

"Ninataka kuaminiwa nawe lakini kwa nini nataka uniamini ni jambo ambalo siwezi kukwambia sasa!" Renatha akamwambia

"Mmm" Edrian akaguna kisha akafumba macho na kufumbua lakini kabla hajasema akawaza kwa nini Allan alichukua muda mrefu kurejea. Renatha akainama huku akimwangalia Edrian usoni akanong'ona

"Kuna kitu nataka uwe makini nacho lakini sitakwambia kwa namna gani, utakapo niamini na kuniambia kitu unachokificha ambacho hakuna mtu mwingine anajua zaidi yako, nami nitakwambia ufanye nini"

Edrian akamwangalia Renatha usoni huku akishangaa alikuwa akizungumzia nini. Akageuka kumuangaza Allan amwambie anaondoka akihisi hana tena uvumilivu wa kuendelea kumsikiliza Renatha. Alipoangalia angalia, macho yake yakashtushwa na mtu aliyesimama hatua chache kutoka kwenye mlango wa kuingia...

"Retha?" akajikuta akisema kwa sauti ya chini kitendo kilichomfanya Renatha aangalie mlangoni ambapo aliona mwanamke ambaye alionekana kumtafuta mwenyeji wake

Edrian akainuka na hatua zake zikamwelekea Aretha akihisi alikuja pale kumuona akizungumza na Renatha akihofia usiwe ni hisia za wivu. Kabla ya hatua za Edrian kumfikia, tayari kulikuwa na mtu alitangulia mbele yake akimwelekea.

"Allan?" Edrian akapunguza hatua huku akipata mshangao alipoona Allan akimuelekea Aretha

Edrian akasogea aliposimama Aretha ambaye naye alikuwa kwenye mshtuko wa kumuona Allan na yeye.

"Aretha samahani usije ukafikir__" Allan alijaribu kumwambia lakini alikatishwa na sauti nyingine iliyotoka nyuma yao.

"Aretha, karibu"

Allan na Edrian wakageuka kumwangalia aliyesema, wakati huo Aretha alibaki kwenye mshangao huku uso wake ukibaki kumtazama Ed.

"BM" Edrian akatamka taratibu huku akihema kwa nguvu.

BM akamsogelea Aretha akionesha kuwa yeye ndie mwenyeji wake na kumfanya Allan asogee pembeni

"Samahani naona kuna muingiliano umetokea hapa na watu unaofahamiana nao, karibu tuketi" BM akamwambia kisha akamgeukia Edrian huku akinyoosha mkono kumuelekea

"Mr Simunge samahani sikufahamu kama uko hapa. Habari ya kwako?" Akamsalimia Edrian ambaye aliupokea mkono na kurejesha salamu ile

"Salama"

Macho ya watu sasa yaliwaelekea wao, kwa kuona hivyo Edrian akamwangalia Aretha ambaye ilikuwa wazi kuwa yuko kwenye bumbuazi la kile kilichoendelea

"Ni mwenyeji wako?"Akamuuliza Aretha ambaye alimwangalia na kisha akatikisa kichwa kukubali