webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

TUTAKUSHANGAZA

"Rian" Aretha alimuita huku akimshika mkono asiendelee kutembea mara tu walipotoka nje ya mlango wa ofisi ya Meneja.

"Retha, nitakueleza baadae. Lakini unahitaji maandalizi kwa ajili ya jumapili. Twende princess." Edrian akamjibu huku macho yake yakitazamana na yale ya Aretha. Na kwa kuwa Edrian alikuwa mrefu, alikuwa akiangalia uso wote wa Aretha huku akizuia mikono yake ambayo ilitamani kumshika kidevu na kupata ladha ya midomo yake..

Aretha aliyebaki ameganda akimwangalia Edrian hakuelewa anaota au ni halisi hadi aliposikia mtu akikohoa kwa nyuma.

"Ooh samahani" akashtuka kumbe walisimama kwenye njia na Fatma sasa alifungua mlango kutaka kupita.

Edrian akacheka taratibu "Twende Retha tutachelewa appointment nyingine" Edrian akamshika mabega kumsaidia kuanza kutembea. Wakatoka wote na kuelekea nje ili kujiunga na kina Coletha ambao waliwaacha kwenye gari.

"Kaka Li unadhani Big Bro amekuja kufanya nini huku Golden?" Coletha akauliza

"Coletha, amekuja kutoa pesa yote na kumpa Aretha kumuonesha anampenda" Li akajibu kwa mzaha

"Aaargh kaka Li, unajua hawezi kufanya hivyo. Au anamtafutia mkopo wa shule eeeh!"

"Weweee, utanichosha Coletha. Wale pale wanakuja muulize sawa eeh. Nipumzishe jamani" Li akajitetea

"Eeeh heheheh waone wanavyopendeza, kaka Li huyu Aretha hana makuu. Ona anavyotembea kwa aibu." Coletha akaendelea kumsumbua kaka yake ambaye aliegama kwenye usukani...

"Sijui huwa unawaza nini tu" akawaza akilini.

Edrian akamfungulia mlango Aretha, kisha naye akaingia kwenye gari..

"Pole kukuchelewesha mwenye njaa yake" Edrian akamtania Coletha

"Hahahaha tumbo langu lina medali ya uvumilivu" Coletha akajibu huku akimgeukia Aretha akamnong'oneza

"Mmefanya nini huko mbona mmechelewa"

"Coletha" wote wawili wakaita kwa pamoja huku wakigeuka nyuma

"Hahahhaa haya brother" Coletha akasogea akimuacha Aretha akitabasamu

Wakaondoka, Aretha sasa alikuwa kimya sana akiangalia simu yake ambapo kulikuwa na meseji zilizoingia kama Meneja Chris alivyomjulisha. Ghafla macho yake yakabaki kwenye kioo cha simu kwa mshangao alipoona ujumbe wa kianzio kilichokuwa kwenye akaunti yake.

"Vipi Aretha mbona umeshangaa hivyo?" Coletha akauliza baada ya kumuona Aretha akishangaa macho kwenye simu yake

"Aaaahm, aa . hamna kitu nilikuwa nasoma tu kitu kimenishangaza" Aretha akajaribu kujitetea

"Kitu gani Aretha?" Coletha akauliza lakini sauti ya Edrian ikamkatisha

"Coletha baby sisy unajua tunaenda wapi?" Edrian akauliza ili kumpoteza mdogo wake kujua kwa nini Aretha alipigwa na butwaa

"Nope! Niambie Big Brother" Coletha akauliza kwa shauku..

"Victoria Style and Design" Edrian akajibu

"Kweli Big brother?" Coletha akauliza kwa shauku kubwa

"Muulize dereva" Edrian akajibu huku akimwangalia Li

"Kweli kaka Li au Big brother ananitania" akamuuliza Li

"Coletha toka lini umeniamini mimi zaidi ya bro Ed eeeh" Li akamjibu huku tabasamu la utani likiwa usoni...

"Aaaah, eeewhhh, Aretha ulishawahi kusikia Victoria Style eeeh?" Akamgeukia Aretha ambaye alitikisa kichwa kuonesha hakujua chochote

"Aaaiii leo nitakuchagulia kitu 'amazing', mimi ni mdau wake kabisa. Nimevaa gauni zake mbili lakini hadi leo picha zake watu wanazizungumzia" akaanza kumwambia na kumfanya Aretha apate kitu kingine cha kutafakari akiliweka lile la benki pembeni.

"Big brother ungeniambia mapema aiii ningemwambia Emmy aje" Coletha akamwambia Edrian

"Emmy yupi?" Akauliza

"Aaah umemsahau rafiki wa Derrick, anapenda zile gauni ulizoniagizia hapo. Ila tutakuja nae tena" Coletha akajibu

"Aaaah tutafanya hivyo wakati mwingine." Akajibu Edrian kisha akarudi kuangalia simu yake.

Wakasimama kwenye jengo la ghorofa ambalo juu kabisa liliandikwa Victoria Style and Designs. Edrian akapiga simu kwanza kabla ya kushuka..

"Tuko hapa V." Akaongea Ed

"Sawa" akakata simu

"Kuna mtu anakuja kuwachukua hapa ngoja tumsubiri" Edrian akawaambia

"Ah Big brother wewe hauji?" Akauliza Coletha swali ambalo lilikuwa usoni kwa Aretha pia.

"Hapana Coletha, tuna mambo ya kufanya na Li ila naomba msaidizane kuchagua kitu kizuri." Akajibu Edrian

"Sawa, tutakushangaza"