webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

TUFANI NDANI

Geti lilipofunguliwa gari ikaingia kuelekea sehemu ya maegesho. Kwa kuona gari ile wakajua nani atakayeshuka, Aretha akapiga hatua kuingia ndani hata kabla mlango haujafunguliwa....

Mlango ukafunguliwa Li akashuka na kuelekea mlangoni ambapo dada yake kasimama,

'Hey bro Li vipi big bro yuko wapi?" Coletha kauliza kwa wasiwasi

"Aisshhhhh, ameniagiza nimpeleke. Vipi mambo yakoje huko ndani"

"Nahisi Lyn amefanya makusudi, yuko wapi yeye?"

"Coletha relax. Hebu twende ndani" Li akamjibu huku akielekea ndani.

Aretha ambaye alitangulia ndani, alipofika akasimama karibu na kochi,

"Oooh mwanangu jamani pole sana, umenitembelea lakini umeishia kufanya kazi" mama akamwambia mara tu alipoingia

"H..Hapana shida mama, n...naomba niondoke maana muda umeenda sana" Aretha akaongea huku macho akiyakwepesha na yale ya Lyn

"Eeeh kweli muda umeeenda na kupata usafiri inak___" kabla ya Lyn kumaliza maneno yake ya dhihaka mlango ukafunguliwa. Aretha hakuinua macho kuangalia mpaka Li aliposalimia

"Mama naona unafurahi na wageni wako" Li hakuonesha hisia yoyote alipoingia japokuwa alifahamu hali ilivyo kama alivyosimuliwa na Ed wakati akija

"Eeh nyie si hamtaki kuja, ngoja nipewe watoto wengine wanaonijali" mama akatania

"Shemeji Li, unaendeleaje hatujaonana tangu juzi" mwili wa Li ulikakamaa ghafla aliposikia maneno haya ya Lyn lakini akarudi na kumjibu

"Vizuri, karibu" alipomjibu akageuza shingo kumwangalia Aretha aliyekuwa akamtazama huku mashaka yake yakionekana wazi usoni pake baada ya kumuona Lyn na sio Ed, akamsalimia

"Habari za siku Aretha"

"S.sa..salama" Aretha akayapeleka macho na kumwambia mwenyeji wake na kumwambia"mama, nashukuru sana, naomba niwaache sasa"

"Oh sawa mwanangu..nashukuru kwa kuja. Karibu tena na tena binti yangu. Hapa ni nyumbani kwako pia" akamgeukia Li "unaonaje mwanangu ukimsogeza binti yangu huko mbele apate usafiri kwa wepesi"

"Sawa Mrs Simunge" Li akaitikia kwa haraka

"Aah hapana mama usimsumbue tu nita__" Maneno ya Aretha yalikatishwa mara na mama yake Ed

"Mwanangu ah hapana, acha afanye hivyo, nitakuwa na amani ukirudi salama!

"Aretha msikie mama kaka Li akusogeze" Coletha naye akatia msisitizo

"Aa. .Sawa..mama nashukuru sana na jioni njema" Aretha akaaga kisha akaelekea nje nyuma akifuatiwa na Coletha na Linus.

Aretha alijaa maswali kichwani baada ya kumuona Li, akajiuliza Ed atakuwa wapi ikiwa ameona gari yake ikiingia ambayo ana uhakika ndio iliyomleta. Wakaingia kwenye gari huku Coletha akimuomba Aretha namba wawasiliane, baada ya kuwa wamebadilishana namba Li akaondoa gari getini.

Ed aliyekuwa amekaa kwenye gari ya Li iliyoegeshwa mita chache kutoka kwenye geti la nyumba ya mama yake, aliishuhudia gari ikiondoka akajua Aretha amekubali kupelekwa. Akashusha pumzi kwa nguvu halafu sura yake ikabadilika, akawasha gari na kumsubiri mlinzi amfungulie geti.

"Am coming for you Joselyn" mawazo ya Ed yakaongea ndani yake. Aretha kuondoka pasipo yeye kumpeleka kulileta maumivu moyoni kwa Ed. Aliamua kufuata ushauri wa rafiki yake ambao hata Li mdogo wake aliukubali. Hivyo Ed alipofika nje ya geti akaamua kumsubiri Li, na alipofika akaona vyema Li atumie gari yake ambayo aliona ilifaa kwa kuwa mdogo wake alikuja na gari ndogo aina Mitsubishi "Sports car". Akakusudia kutompatia mama yake wala Aretha shida.

Alipoendesha kuingia ndani ya geti, Coletha alikuwa nje bado akiangalia simu yake. Baada ya Ed kufungua mlango wa gari na kushuka muonekano wake ulimfanya dada yake kujua ujio wa kaka yake ni wa kushughulikia jambo na kulimaliza au kumaliza mtu. Akatamani afurahi lakini akaomba moyoni mambo haya yasimuathiri mama yake ambaye hakumjua Lyn vizuri wala hakumfahamu Aretha sana.

Coletha akamtazama kaka yake ambaye alipiga hatua kumuelekea, "Bro mbona hukum__"

Maneno ya Coletha yalikatishwa na mkono ulionyooshwa kumuonesha, Ed hakuwa tayari kuzungumza kuhusu hilo. Akamgusa begani kisha akapita na kuingia ndani akimuacha nyuma dada yake ambaye wazo moja tu lilikuja ndani yake.

"Tufani itavuma huku ndani" akawahi kumfuata ndani kaka yake ili kushuhudia mambo yatakavyokuwa.