webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

SUPRISE (3)

Mida ya saa nne Derrick aliendesha pikipiki yake kuelekea Moon Street, nyumbani kwao Aretha. Alikusudia kumshawishi kwa namna yoyote aweze kuongozana nae kwenda kwa Ed. Aliamini kuwa hatua hii itarahisisha mahusiano yao kuwa imara. Alipofika na kugonga kwenye geti la kuingia, alipokelewa na mama yake Aretha ambaye moja kwa moja alionekana kuwa na kazi as bustani. Alipokaribishwa ndani Derrick alikataa na akaongozana na mama yake Aretha mpaka bustanini.

"Mwanangu huku utachafuka, nisubiri ndani namalizia kumwagilia mboga hapa nakuja" mama Aretha alijaribu kumsihi Derrick.

Kabla ya kujibu chochote, Derrick alichukua birika mkononi mwa mama huyu na kuanza kumwagilia huku bila wasi wasi na kumuacha mdomo wazi mama Aretha. Wakati huo ikabidi achume mboga ambazo alikusudia kuzitumia leo.

"Eeeeh Derrick mwanangu mbona wajitesa jamani"

"Ha ha ha mama, mtoto wa kiume kuteseka ni sehemu ya mafunzo" Alijibu Derrick akiendelea kumwagilizia mboga na wakati huo raba alizovaa zilikuwa zimepata matope.

"Ooooh... basi nitakuiba huko ili uje uishi hapa, huyu binti yangu kalala hadi saa hizi, jumamosi huwezi muona huku. Nahisi alichelewa tena kulala!"

"Hahaha bila shaka nitahamia, nilitaka Retha anisindikize walau akabadilishe mandhari"

"Leo?" Aliuliza mama Aretha

"Ndio mama, lakini hajanipa jibu, nikaona nije nimshawishi"

"Mmh mwanangu huyu msichana Jumamosi ndio analala na kushinda kwenye uchoraji, mimi mwenyewe nilishamsahau siku za jumamosi... jaribu kuongea nae labda atakusikiliza." Alimueleza Derrick huku akimaliza kuosha mboga alizochuma.

Derrick nae alikuwa amemaliza kumwagilia wakaongozana kuelekea mlango wa nyuma ulioingia jikoni. Baada ya kuvua viatu na kuvifuta wakaingia ndani

"Ngoja nimwamshe muongee nae" alisema mama yake Aretha

"Aaah hapana mama, nisikusumbue. Ukinipa ruhusa nitaenda mwenyewe" Derrick alimsihi mama huyu ambaye aligeuka kumwangalia kisha akasema

"Sawa mwanangu ila usijaribu mambo yenu ya ujana. Ingia hapo sebuleni kuna mlango unaoelekea vyumbani kona ya kwanza mkono wa kushoto chumba chake utakiona." Alimuelekeza

"Haha mama wala usijali, mimi ni mwanao mwaminifu" Derrick alijieleza huku akichukua hatua kufuata maelekezo ya mama Aretha.

Baada ya kufika kwenye mlango wa Aretha, Derrick aliinua mkono kugonga lakini alisikia sauti ya Aretha akiongea na simu... Derrick akasogea karibu na kutega sikio vyema asikie.

Haikuchukua muda kusikia jina la kaka yake likitajwa na kujua hakika Aretha alikuwa akizungumza na Edrian.

Aliyasikiliza maongezi na alipohakikisha wamemaliza akagonga mlango.

Mlango ulipofunguliwa, macho ya Aretha yalipigwa na mshangao uliokuwa wazi na mara moja akafunga mlango. Derrick akatabasamu baada ya kuona kitendo kile, kisha akagonga tena mlango.

"Nisubiri sebuleni nakuja" alijibu Aretha huku mlango ukiwa umefunguliwa kidogo kuruhusu upande mmoja wa uso wake kuonekana.

"Sawa Retha, ila naomba nione picha unazochora?" Maneno haya yalisindikizwa na tabasamu ambalo lilionesha wazi kuwa hana mpango wa kuondoka hadi Aretha akubali...

Aretha akamwangalia na kumkubalia kwa kichwa ili aondoke. Derrick akampa ishara ya kidole gumba kuwa wamekubaliana. Akaelekea sebuleni na kumsubiri.

Wakati huo mama yake Aretha alikuja na kuendelea kuzungumza na mgeni wao ambaye sasa alikuwa na glasi iliyokuwa na juisi ya embe..

Aretha aliingia sebuleni akiwa amevalia suruali ya kaki na fulana pana ya rangi nyeusi iliyochorwa picha ya ndege tai.

Baada ya kumsalimia mama yake ambaye alianza kumshawishi kuhusu mwaliko wa Derrick...

"Lakini mama, siwezi leo, nina picha nataka niimalize kabla ya kesho. Usijaribu kunishawishi maana sitaweza" akamgeukia Derrick

"Derrick nisamehe kwa leo nitashindwa, siku nyingine nitakusindikiza"

Derrick alijua kwa nini Aretha hawezi maana alimsikia akimuahidi Ed kaka yake kuwa atampelekea hiyo picha.

"Retha... wewe hupendi kutoka hata kuona mazingira mapya na kukutana na watu wengine...aaaargh lini utaacha mambo ya kujifungia ndani" mama yake alilalamika

"Mama usimlazimishe sana, nina sehemu nyingine nataka anisindikize siku ya jumatatu."