webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

SUMU YA KUNIUA

Derrick alipomaliza kumsimulia kaka yake yale yaliyotokea kati yake na Lyn, alishangaa kuona tabasamu usoni kwa Ed. Alitegemea kusikia "mmmmm" lakini haikutoka mdomoni mwa kaka yake na badala yake kulikuwa na tabasamu kama la mtoto aliyekuwa akitafuta kitu halafu ghafla akakiona..

"Bro vipi...kitu gani kimekufurahisha?" Akauliza Derrick..

"Ah, ooh samahani, nimekumbuka kitu ndio nikatabasamu" akamwangalia mdogo wake ambaye alikuwa kwenye kitendawili cha kung'amua tabasamu la kaka yake..akaendelea

"Kwa mara nyingine...nisamehe. Sikujua kabisa mlifikia hapo, sikukupatia nafasi ya kujieleza. Naomba umsamehe kaka mkubwa kwa kukujeruhi."

"Hamna shaka bro, limepita hilo. Na hata hivyo naamini utafanya maamuzi sahihi." Derrick akamuwahi kaka yake asiendelee kuomba msamaha. Ulimwengu wa nje ulimfahamu Edrian kama mtu asiyetoa "samahani" yake haraka, lakini kwa Derrick anamjua kaka yake linapokuja suala la familia ni mwepesi kusihi msamaha kwa ndugu zake kuliko anavyotambulika.

"By the way..ikiwa utamsamehe Lyn nitakuelewa tu bro, liko kwenye maam____"

"Mdogo wangu nashukuru, nina swali nami nataka nikuulize" Ed alimkatisha Derrick

"Niulize tu bro"

"Kuna kitu kingine unachokijua zaidi kuhusu Lyn?"

Derrick akamwangalia kaka yake kisha akatikisa kichwa kuonesha kuna kitu bado hakuwahi kumwambia Ed

"Hata kama isingekuwa kilichotokea kati yangu na yeye, kuna hisia tu ilikuja tangu nilipomuona kwenye harusi ya bro Bri ambayo ilinitahadharisha nae, I felt it, more like a warning"

"Mmmhhh" Ed akaguna

"Bro... usinikasirikie lakini, kuna kitu Emmy aliniambia tulipokuwa harusini lakini sikumwamini mpaka uliporudi siku ya pili nyumbani ukiwa unalalamika unasikia mwili u dhaifu sana"

Macho ya Ed yakakaza kumuangalia Derrick usoni kwa mshangao uliobeba swali,

"Niambie D, tafadhali usinifiche tena"

Derrick akainua shingo yake iliyokuwa imeegemea kwenye kiti akamwangalia kwa sekunde kaka yake akijaribu kufikiri akisikia hicho anachotaka kusema atafanya nini. Akapiga mahesabu kichwani kisha akamwambia

"Siku ya harusi ya bro Brian, kumbuka tulikaa meza moja kitu ambacho kilitufanya sisi kumfahamu Lyn kama mtu ambaye uko na mpango naye wa kumvisha pete."

"Mmh" Ed akampa ishara aendelee...

"Wakati tumemaliza kucheza muziki tukiwa tunarudi, wewe ulikuwa unaongea na classmates wako. Mimi sikuwa naangalia kule mezani, lakini Emmy wakati namrudisha aliniambia alimuona Lyn akirudisha kichupa fulani kwenye pochi yake na kisha akatikisa glasi yako iliyokuwa na mvinyo.. akaniuliza kwa kiasi gani nakufahamu nikamwambia si sana"

Ed aliyekuwa akisikiliza kwa makini ni kama macho yake yalitaka kutoka kwa namna alivyoshtuka.."eehhh" akauliza kutaka kujua zaidi...

"Bro nilimwambia Emmy labda ameona vibaya, lakini alinihakikishia kuwa ameona kwa macho yake. Na tena Lyn alionekana kufanya kwa haraka asijulikane."

"Mmm" Ed aliguna na kumfanya Derrick ajue mazingira yamebadilika

"Bro alipomaliza kuniambia nilipiga simu yako haikupokelewa, nikampigia bro Li akaniambia mmeondoka na Lyn. Na nilipojaribu kumuuliza hali ya muonekano wako, akaniambia uko vizuri na inaonekana ulitaka privacy na Lyn so uliondoka na gari ukimuacha Bro Li arudi na Allan."

Ed akashusha pumzi na kumwangalia Derrick ambaye aliona taabu hata kupumua kwa jicho kali lililomwangalia....

"Bro relax kwanza...siku ya pili ulipompigia bro Li aje awachukue hoteli mlipolala nikataka kufuatana nae lakini akanizuia na kunihakikishia kuwa atanitaarifu ikiwa kuna shida... Aliporudi alikuja nawe na ulionekana uko vizuri japokuwa ulilalamika uchovu tu na ukaenda kulala. Nilijaribu kukuchunguza lakini sikuona jambo baya. Hata sasa bado naamini utabaki salama bro" Derrick alimaliza akiwa tayari kubeba ghadhabu ya kaka yake kwa kukaa kimya. ...

"Kwa nini hukuniambia mapema D, vipi kama ingekuwa sumu si ningekufa" Ed aliuliza kwa sauti ya chini ambayo ilibeba mitetemo ya hasira

"Kwa kweli nisamehe bro lakini kwa namna ulionekana baada ya kurudi na mlivyokuwa na Lyn nikaamini hawezi kuwa alikuwekea sumu."

"Na je kama ni sumu ya kuniua taratibu je?" Ed akamuuliza akiinua jicho lake