webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

SUBIRA RIAN

Nguo kadhaa zilikuwa juu ya meza, pembeni viatu vya kike na kiume na mikoba mikubwa na midogo.

V akainua nguo moja baada ya nyingine, akaitolea maelezo ambayo kuna wakati yaliwafanya wacheke. Katika nguo zile asilimia kubwa zilikuwa nguo za wakati wa baridi, masweta na makoti yaliyoshonwa vyema. Edrian akachagua makoti machache, suruali na viatu.

Aretha alivutiwa na suruali kadhaa za kike, masweta, viatu, ilikuwa ni jukumu la V kumshawishi vile alivyoona bora na vyenye kufaa..

"Chukua hivi Aretha, viatu vyepesi havifai kwenye maeneo yanayoanguka barafu"

Aretha akamwangalia Edrian ambaye alikuwa akitazama aina ya mikoba ya kike, akachagua miwili iliyomvutia na kumpatia

Baada ya muda wa kuchagua kumalizika, V akaita mhudumu akaondoa vile ambavyo havikuchaguliwa. Wakabaki na vile vilivyochaguliwa huku V akimuinua Aretha kwa ajili ya kujaribu nguo. Wakaingia kwenye pazia huku V akipangilia zile nguo na viatu.

Kila alipojaribu Aretha hakutaka kutoka kumuonesha Ed, alipomaliza akatoka akiwa amevaa kama alivyokuja. Edrian akamwangalia kwa kusikitika

"Hutaki nikuone" akalalamika

"Hahahaha kila mmoja ana 'suprise'. Subira subira Rian" Aretha akamwambia huku akicheka kwa kurudia maneno yaleyale aliyomwambia

"Hhahaha haya,Tafadhali tufungie V" akamwambia huku akitoa kadi yake na kumpatia

V akaita mhudumu ambaye alibeba vyote vilivyochaguliwa, wakatoka kuelekea sehemu ya malipo na kuwaacha Ed na Aretha.

Ed akafungua jokofu na kutoa maji akampatia Aretha huku yeye akibaki na mengine.

"Rian tunakoenda kuna barafu inaanguka?" Akauliza Aretha kwa shauku

Edrian akamuangalia huku akitabasamu, "Suprise"

Aretha akacheka "Tukitoka hapa tunaenda wapi?"

"Nako pia ni suprise hahaha"

*************

Derrick alikutana na Yassin katika harakati za kutafuta mahali ambapo onesho la Beruya lingefanyika. Wakiwa wametembelea moja ya ukumbi uliopatikana kwenye hoteli ya The Crest!

Baada ya kuelekezwa gharama na mambo yote yaliyohitajika wakajaribu kuwasiliana na Beruya lakini simu yake ilionesha Kutumika wakati wote. Yassin akamwambia Derrick

"Nina wasi wasi juu ya Beruya maana si kawaida yake kuwa 'busy' na hata asipokee simu zangu!"

"Mh..... unahisi kuna shida?, au nijaribu kumtafuta mimi?"

Derrick alipojaribu kumpigia simu Beruya akaambiwa namba haipatikani. Wakaamua kwenda nyumbani kwake lakini walipofika hakukuwa na dalili za kuwepo Beruya na hata baada ya kuulizia kwa jirani zake bado hakuna aliyekuwa na taarifa zake. Wakaamua kuondoka na kuelekea kwa Damian wakiamini wanaweza kupata majibu sahihi huko.

************

Safari ya Ed na Aretha iliishia nyumbani kwa Brian na Rose.

"Karibu sana Aretha" Brian akamkaribisha Aretha kwa furaha mara tu alipofika mlangoni,

"Asante" akashukuru huku akimtazama Ed kwa mshangao kwamba Brian alimfahamu,

"Hahaha usishangae Aretha, ulikuwa ni kibwagizo mdomoni mwa huyu 'senior bachelor' tangu akufahamu...." akamwambia Brian

"Ooouuch!" Brian akaugulia maumivu ya ngumi ambayo Ed alimpiga begani kumzuia asiseme

Aretha akamwangalia Ed akaimkataza asifanye hivyo

"Oooh asante Aretha, atanivunja mifupa huyu" Brian akalalamika

"Kwa hiyo hao wageni utabaki nao hapo nje hadi waondoke eeeh" Sauti ya Rose mkewe Brian ilisikika kutokea ndani akiuliza kwa utani na kumshtua Brian ambaye furaha yake ilikuwa kuu kumuona Aretha pamoja na rafiki yake...

"Ooooh nisamehe laaziz! Wageni karibuni ndani" Brian akawaelekeza kuingia ndani

Walipoingia ndani, Rose aliketi kwenye kochi huku akipata juisi akainuka na kuachia mikono yake ili kumsalimu Aretha.

"Asante sana Aretha, nimefurahi umekuja" akamkumbatia na kisha akamketisha kwenye kochi alilokuwa ameketi

Brian akaelekea jikoni, kisha akarejea na glasi moja ya juisi na kumkabidhi Aretha

"Aretha huyu bwana anakuhudumia vyema kweli" Rose akamuuliza Aretha, swali lililomfanya Ed kuangua kicheko

"Toka lini mimi ninawahudumia watu vibaya jamani, kwanza naona humu ndani mgeni ni mmoja tu!" Akainuka na kuelekea jikoni

"Aaahhh si umeona unajua kujihudumia" Brian akamwambia huku akiketi kochi lililotazamana na lile aliloketi mkewe na Aretha.