webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

NAKUAMINI

Wiki iliisha taratibu Ed akisubiri kuona kama Joselyn angefanya kitu cha kumdhalilisha kwenye mitandao ya kijamii lakini kulikuwa kimya. Hakumsumbua kwa kumpigia wala kufanya chochote. Akaamua kuamini kuwa huenda Joselyn ameelewa na kukubaliana na ukweli kuwa hawezi kuendelea na mtu ambaye hayuko tayari kuwa nae.

Mama yake Edrian alikubaliana na maamuzi ya mwanae kuamua kuweka mahusiano yake na Aretha wazi pasipo kuhofia kile Joselyn angeweza kufanya,

"Sawa mwanangu nakubaliana nawe, simuamini Lyn najua kwa namna yoyote atajaribu tu kuifanya jamii iwe na mkanganyiko wa uhalisia wako. Hivyo usilegeze ulinzi wako kihisia na kimwili." Mama yake hakuacha kumsihi kijana wake!

"Nitafanya hivyo mama. Naomba wikiendi hii nimlete Aretha" akamuomba mama yake

"Aishhhhh Ed, unaniomba kumleta binti yangu! Njooni tu mwanangu. Hata mje wote tunawakaribisha!"

Edrian wiki iliyopita alimuendesha Aretha hadi kwenye hoteli karibu na ziwa Dishan. Derrick alifanikiwa kumuunganisha na wachoraji mahiri wa kike wawili ambao walifahamika kwa kazi zao. Melissa na Beruya walimfahamu Derrick kwa sababu alihudhuria mara zote kwenye maonesho waliyoyaandaa. Edrian kuhusika ikafanya kwa rahisi zaidi kwao kukubali kuonana na Aretha kuweza kumsaidia kuipa muonekano kazi yake katika jamii.

Kwa kuwa Aretha hakuwa vizuri kwenye kuongea Edrian alimua kumchukua Derrick pamoja nao. Kabla ya hapo walikutana na Mr Singhran ambaye uhusika na minada ya picha akawaeleza masharti na vigezo vya kuzingatia. Na moja ya sharti ni kuwa picha itanunuliwa na kampuni ya Singhran na hivyo kama mchoraji hautakuwa na haki ya kupanga bei itakayouzwa kwenye mnada wala kudai iwapo bei itayaouzwa kwenye mnada itakuwa kubwa kuliko bei uliyolipwa na kampuni.

"Retha punguza hofu, ni wanawake tu kama wewe tena kuna vitu unawazidi ujue" Derrick alijaribu kumfariji Aretha aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma huku Derrick akiwa mbele na Edrian ambaye alikuwa akiendesha. Aretha alipofunguliwa mlango na Derrick akae mbele, aligoma akaketi kiti cha nyuma. Muda wote alikuwa akifinyanga vidole vya mikono yake

"Lakini Derrick unadhani hii picha wataikubali kweli ni ya kawaida sana ukilinganisha na zile umenionesha kutok_"

"Retha" Edrian akamuita huku akimuangalia kwenye kioo cha ndani

"Eehmm"

"Wakiikataa tutatafuta ambao wataikubali, uwe tayari kuitetea kazi yako mwenyewe. Sisi tunakuamini na tunaamini kipaji chako, hatuwezi kufanya zaidi ya wewe mwenyewe, umenielewa princess" Ed aliongea kwa upole huku akimuangalia wakati gari ilipoegeshwa kwenye sehemu ya maegesho ya hotel you iliyoko ufukweni kwa ziwa dogo la Dishan.

Derrick wakati huo alikuwa akitabasamu baada ya kusikia 'princess ikitoka kinywani kwa Ed. Akamwangalia kaka yake ambaye alimpa jicho lililobeba swali la "unatabasamu nini". Derrick akageuka na kufungua mlango tayari kushuka...

"Derrick" Aretha akamuita kabla ya kushuka

"Vipi Retha!" Akaitika Derrick huku akigeuka kumuangalia

"Unadhani lazima mimi niseme kit_"

"Derrick hebu tusubiri kidogo hapo nje" Edrian akampa maelekezo Derrick ambaye aliyafuata huku tabasamu lake likiwa dhahiri usoni hata kumfanya Aretha ashtuke nae akainama kwa aibu

Walipobaki peke yao, Ed akajigeuza vyema na kumwangalia Aretha aliyekuwa nyuma akiangalia nje kwenye jengo la hoteli huku mawazo yake yakionesha wazi alihofia mkutano huu.

"Retha sogea" Edrian akamwambia naye Aretha akasogea kumsikiliza na alichopata hakikuwa mazungumzo Edrian alimshika shingo kwa nyuma akakutanisha midomo yake na ile ya Aretha akimuacha na mshangao ambao ulimruhusu kupenya mpaka ndani ya kinywa chake. Aretha hakuweza kujizuia, aliyeyuka kwa mguso ule na mwitikio wake ukawa kumwacha Ed apate wepesi wa kumbusu sana huku naye akirejesha kile alichofanya Ed.

Sekunde chache baadae Ed alimwachia apate kuhema vyema. Akachukua kitambaa chake cha mkononi akamfuta uso Aretha aliyekwepa macho ya Ed. Akamuweka nywele zake vyema kisha akamwambia

"Nakuamini. Na niko nawe. Can you be confident, and let's do this together?"

Aretha akainua macho na kumwangalia Edrian, akatabasamu "Okay Rian"

"Then let's go"