webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

NAJUA KUZICHEZA KARATA ZANGU

Baada kuelekea vyumbani kwao, Joselyn aliyekuwa amekaa muda wote akiangalia Tv, aliinuka na kuizima. Akavuta hatua kuelekea juu ambapo badala ya kwenda mpaka chumba cha wageni alichofikia akaelekea chumbani kwa Ed, ghafla akakunja kulia na kuingia korido iliyoelekea chumbani kwa Derrick, alijua kabisa kwa muda huo shemeji yake hatakuwa amefunga mlango.

Akausukuma taratibu bila kupiga hodi na wakati huu maji yalisikika bafuni. Akajua Derrick anaoga, akakaa kitandani akimsubiri.

Baada ya dakika chache mlango wa bafuni ulifunguliwa na Derrick alitokeza akiwa amefunga taulo kiunoni. Alishtuka kumkuta Joselyn amekaa kitandani kwake, akainua macho kumtazama kwa dharau,

"Unataka nini?" Aliuliza

"He he sitaki kitu nimekuja tu kukuonya shemeji" alijibu Joselyn huku akimuangalia sana Derrick macho yaliyonesha unafiki

"Ondoka chumbani kwangu" alisema Derrick huku akichukua shati na kuvaa.

"Sikia D, chochote kibaya unachopanga kumwambia Ed, ahirisha." Alisema kumtisha shemeji yake.

"Unachoogopa nini kama hakuna jambo baya unafanya Lyn?" Alimuuliza huku akishika kitasa cha mlango na kufungua akimpa ishara atoke.

"Sina kibaya nachofanya ila najua unanichukia na unaweza nitungia uongo" alijibu huku akisimama na kumfuata Derrick

"Huna la maana nipishe nilale"alimjibu

Joselyn alionesha kukerwa na jibu hilo, akafika alipokuwa na kumgusa mashavuni

"Najua kuzicheza karata zangu usidhani ni mjinga. Unajiona sana kwa kuwa kaka yako anakupenda. Watch out D"

Derrick aliusukuma mkono wa Joselyn kisha akamkaba shingo kwa hasira lakini alipoona Lyn anatabasamu tu akamwachia, akamsukuma nje ya chumba chake na kufunga mlango.

Joselyn akacheka na kushuka ngazi taratibu akielekea mlango wa kutokea. Alikutana na dada wa kazi akimalizia kuiweka vyema sebule.

"Dada Lyn unaondoka?" Aliuliza Zena

"Nibaki nafanya nini wakati Ed hayupo, mliobaki hamnihusu" alijibu Joselyn na kutoka nje na mlio wa geti ulisikika kuashiria anatoka na gari yake.

"Mpheew! Kuringa tu utadhani kashaolewa" alijisemea Zena na kumalizia kuzima taa za ndani na kuelekea chumba chake kilichokuwa nje pembeni na mlango wa kuingia jikoni.

Usiku huu Derrick hakuweza kulala vyema, aliwaza namna gani atamshawishi kaka yake kumuacha Joselyn. Tangu mwanzo alikuwa na hisia mbaya juu ya nia ya Joselyn. Sasa anahitaji ushahidi kumshawishi. Lakini wakati akiwaza hivyo hakujua shemeji yake ameshamzidi hatua kwa kumsingizia kuwa alimkaba shingoni sababu ya kuingia chumbani kwa Ed. Kaka yake alishaamini kile kilichosemwa na mpenzi wake. Derrick aliumia kwa namna ambavyo kaka yake ambaye anamheshimu kumhukumu pasipo kumsikiliza.

Derrick aliazimu kumfuatilia zaidi Joselyn na kuhakikisha pete ya kaka yake haitaingia katika kidole cha mwanamke yule.

Aliondoka katika nyumba ya kaka yake na kuelea Heaven Apartment moja ya nyumba zinazomilikiwa na familia yake, alishukuru kuwa pamoja na kile kilichotokea bado ana uhakika kuwa kaka yake ni mtu mwema.

Karata alizozitupa Joselyn aliamini kuwa atazilipa kwa mafungu, kwa msaada wa kaka yake Li.

************************************