webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

MTUMBWI MMOJA

"Unadhani kama ukipata ushahidi unaweza kufungua mashtaka?" Li akamuuliza huku akimkazia

Allan akamtazama Li kisha akaegama kwenye kiti akashusha pumzi na kujibu "Siwezi"

"Umeshamwambia?" Li akamuuliza huku akiegama kwenye kiti tabasamu likiwa usoni kwake

"Mhmm sijui nawezaje kumwambia mwanamke ambaye anaonesha kuvutiwa na Bro!," Allan akauliza huku huzuni ikionekana wazi usoni kwake

Li akainuka na kuegemea meza "Nisikilize Allan, mwambie kwa sababu sina shaka hivi karibuni matarajio yake yatayeyuka yote. Si vibaya ukijaribu comrade"

Allan akashusha pumzi, "Li asante, ila naomba kwa sasa nijue kama ni yeye aliyehusika au la!"

"Usijali, Captain anakuja atashughulikia" Li akamtoa wasi wasi

"Naomba basi Alphonce asijue" Allan akamuomba

"Oooh tena kweli, nitamwambia mara akifika na __" mlio wa simu ya Li ukasikika, akaichukua na mara alipotupia macho kwenye kioo uso wake ukakunjuka

"Hellow" akapokea, upande wa pili ukaongea naye Li akajibu

"Leo au kesho?" Akauliza kisha akaendelea huku tabasamu likiwa usoni kwake..

"Lakini sio lazima kufanya hivyo Ber__" kabla hajaendelea ni wazi alikatishwa na akabaki akisikiliza huku akijaribu kuficha tabasamu usoni kwake.

"Basi sawa kesho nitafika jioni" hatimaye akahitimisha mazungumzo yake huku akiyakwepa macho ya Aĺlan

"Nawe pia Beruya" akakata simu na kuinuka

"Mtumbwi mmoja comrade hahah" Allan akamwambia

"Hahaha hapana kabisa Allan, mimi nafanya majukumu niliyoachiwa na Bro. Na wewe umempenda mfanyakazi mwenzio inakuwaje tukafanana!!" akauliza Li

"Majukumu yapi hayo?" Akauliza Allan huku akiinua nyusi juu

"Majukumu ya kila siku na___" kabla ya kumaliza Allan akamuwahi

"Kwa mfano hayo ya kesho jioni ni yapi?" Akauliza

"Comrade, hakuna kitu kinaendelea, ngoja nikaongee na Beno mara moja, Captain akifika nijulishe" akaelekea mlangoni

"Najua kwa kiasi gani unajua kuficha hisia zako bro lakini geuza ushauri unaotupatia ukufaidie pia" Allan akamwambia kiasi cha kufanya hatua za Li zisimame akainama chini kisha akaendelea mlangoni

"Ni kweli unanifahamu" akasema taratibu kiasi Allan hakusikia. . Akatoka mle ndani na kisha akasimama kuzungumza kidogo na Loy,

"Loy unatamani boss arudi eeeh" akamuuliza

"Aaaaahhh kaka Li, ila nimemkumbuka sana" Loy akamjibu hisia zake zikiwa wazi usoni kuwa alimkumbuka Ed

"Usijali, siku chache atakuwa hapa, upate kimuhe muhe ulichozoea" Akaelekea ofisini kwa Beno lakini kabla ya kufungua, mlango ukafunguliwa na Renatha ambaye alionekana kuwa na haraka akataka kuelekea ofisini kwa Allan lakini alipomuona Li akasimama

"Habari yako?" Akamsalimia huku akijaribu kutoonesha haraka

"Salama, Renatha?" Li akamjibu kisha akamuuliza

"Yes, Loy, Allan anapatikana ofisini?" Akajibu huku akimuuliza Loy

"Yupo lakin__" kabla ya kumaliza Renatha akavuta hatua kuelekea ofisini kwa Allan akiwaacha Li na Loy wakimshangaa

"Huyu ndio yuko hivi siku zote eeeh!" Akauliza Li

"Nadhani kuna kitu hakiko sawa leo" Loy akamjibu

Li akaondoka kuelekea ofisini kwa Beno.

**************

Allan akiwa ameegama kwenye kiti akayatafakari maneno ya Li,

"Natamani kile ninachohisi kisiwe kweli Renee" akasema kwa sauti ya chini akaangalia tena ile picha ya kamera za ndani aliyoituma kwenye barua pepe yake bado hakuelewa inakuwaje hakuonekana mtu kufungua mlango na bado mlango ulikuwa wazi.

"Hawezi kuwa amepita dirishani" Allan akawaza lakini ghafla mlango wa ofisini kwake ukafunguliwa pasi na hodi

"Renatha!!" Allan akashtuka na kumtazama, lakini Renatha alipoingia akaufunga mlango na ufunguo kisha akaelekea aliposimama

Hakuongea chochote zaidi ya kumvuta Allan kisha akambusu kwa nguvu hata kidogo Allan akose usawa wa kusimama..

Busu lilikuwa la kimabavu na Renatha hakumpa nafasi Allan aulize chochote zaidi ya kumbusu, alipomwachia Allan alikuwa akihema sana

"Uwe tayari saa mbili nitakujulisha wapi uje unichukue." Akapiga hatua kuelekea mlangoni

"Renatha unahitaji kuniambia ukwe___"

"Sshshhh" Renatha akamkatisha huku akiweka kidole mdomoni kisha akaendelea

"Fanya unachojua, ila kama nilivyokwambia saa mbili nitakupigia" akatoka