webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

MSAADA WA POLISI

Mara Inspekta Sunday alipoondoka, Edrian akarudi baada ya kufunga mlango, wakati huu Aretha akainuka mahali alipokuwa ameketi

"Rian" akamuita akiwa amesimama

Edrian akasimama mbele yake, "naam"

Aretha sasa hakuangalia chini bali akayakaza macho kumwangalia Ed kiasi cha kufanya mapigo ya moyo ya Ed kugonga kwa haraka huku kichwani akijaribu kujipa moyo kwa kuwaza fikra chanya

"Akiwa sio Joselyn?" Akauliza Aretha

Ed akamwangalia Aretha na utoto wake katika kuyaona mambo ukamvutia zaidi...

"Okay, tuseme sio Joselyn, unadhani nani aliyeleta hizo habari kwa wale vijana waliojaribu kukupa fedheha darasani?

Aretha akashusha macho chini akitafakari lakini mkono wa Edrian ukainua kidevu chake

"Ninaweza kumshughulikia sasa sababu najua ni yeye. Na ninaweza kumshughulikia pasipo msaada wa polisi. Jiandae tuondoke Retha"

Aretha akiwa na mshtuko kwa kile alichokisikia, Edrian akainama na kumuachia busu jepesi kwenye midomo yake na kisha akachukua mfuko uliokuwa na nguo akauweka kitandani.

Aretha akaufungua zilikuwa ni nguo mpya; suruali ya rangi ya bluu na blauzi ya rangi ya chungwa na raba nyeupe. Alipofungua mfuko mwingine mdogo macho yake yakawaka kwa mshtuko, nguo za ndani yaani chupi na sidiria huku kukiwa na kifuko cha taulo za kike. Aretha akageuka na kutaka kumuuliza lakini Edrian alikuwa makini kwenye simu yake akiandika pasipo kumtazama.

Akachukua ule mfuko na kukimbilia bafuni akafunga mlango. Edrian akatoa macho kwenye simu akashusha pumzi akakumbuka nini Dokta Brianna alimwambia mara alipomfikisha hospitali

**********

Njiani wakati Edrian akiwapeleka Aretha na Charlz hospitali kichwa chake kilijaa mawazo huku picha ile ya Aretha akiwa na Charlz ikikaa kichwani mwake. Kitu pekee alitamani kukiondoa kichwani kwake ni kumuona Aretha akiwa mtupu na asiye na fahamu wala msaada. Ilimuuma sana Edrian.

Mara alipofungua mlango alimuona Aretha akiwa amelazwa kifuani kwa Charlz wote wakiwa watupu. Kwa kuwa Derrick alikuwa nyuma yake hakutaka ashuhudie picha ile. Alikusudia saa ile abaki yeye, lakini sauti ya Derrick nyuma ikamshtua

"Brother kun_" kabla ya Derrick kumaliza akageuka kwa haraka akamsukuma nyuma

"Subirini hapo" akamwambia Derrick kisha akaingia ndani na kufunga mlango kwa haraka akiwaacha Derrick na Angle katika mshangao.

Akawasogelea akagusa mguu wa Charlz kuona kama kutakuwa na mjongeo wowote, akafanya kwa Aretha pia lakini hawakuamka.

Akamshika Aretha na kumgeuza, akashtuka baada ya kuona mchirizi ya damu ikitona taratibu mapajani mwake..

Mapigo ya moyo ya Ed yaliingia marathoni ghafla, akamuweka pembeni, ndipo akaona sehemu ya mapaja ya Charlz pia yalimwagikiwa matone hayo ya damu.

Akashusha pumzi 'tulia Ed, tulia na ufikiri" akaangalia nguo zilizotupwa chini hivyo hovyo akazitambua ni za Aretha na Charlz.

Pamoja na hizo harakati zake Aretha na Charlz walibaki vile vile hakuna hata aliyeinua kiungo chake chochote. Akajua hawako sawa. Akachukua kitambaa kilichokuwa kwenye mfuko wa suruali yake akamfuta Aretha kuondoa damu na kisha akamfuta Charlz. Akachukua nguo akamvalisha kwa haraka huku akishukuru kwa kuwa Aretha alivaa gauni.

Alipomaliza akashangaa kuona nguo ya ndani ya Aretha ikipata tena matone ya damu. Akachukua kitambaa alichowafutia akakikunja vyema na kukiweka kuzuia damu isiguse gauni.

Akachukua suruali ya Charlz akamvalisha, lakini akasikia kitasa kikiguswa na sauti yenye wasi wasi ya Derrick ikasikika akimuuliza

"Bro kuna shida, tafadhali fungua mlango"

Akaamua kwenda kufungua akimuacha Charlz pasipo kumvalisha shati. Alipopiga hatua akaona Charlz akijaribu kufungua macho kwa shida, akaelekea kufungua mlango ambao ulisukumwa na Derrick akiwa na wasi wasi

Akabaki akishangaa kile alichoona. Ed akachukua simu na kubonyeza kisha akaongea na Dr Brianna. Alipomaliza akamnyanyua Aretha na kuwapa maagizo Derrick na Angie wamsaidie Charlz kufika kwenye gari baada ya kuona anarejewa na ufahamu.

Njiani aliendesha gari akimtazama Charlz kwenye kioo, kichwani alitamani kutaka kujua imekuwaje.