webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

MDAU MKUBWA

Derrick" Aretha akaita

"Naam" akaitika Derrick

"Unadhani Ria. .aah samahani Edrian ana maadui wengi?"

Derrick akamwangalia Aretha kisha akatabasamu, "Retha, hebu niambie nini hasa unaogopa, maana kila mwanadamu ana maadui. Wengine ni waharibifu na kuna wengine la!"

"Aaaha..basi nawaza tu! Inawezekana unasema kweli najitia hofu" Aretha akatoa simu yake ambayo iliingia meseji muda huo.

Akasoma na kuijibu huku akimuacha Derrick katika tashwishwi ya kutaka kujua ni kaka yake au la.

Hadi muda ule Beruya alikuwa bado hajafika, wakaendelea kumsubiri huku wakiwa wameketi mahali pale walipoelekezwa. Walizungumza mambo mbalimbali ikiwa hasa yale yaliyohusiana na uchoraji,

"Oooh Aretha samahani nimekuchelewesha" sauti ya Beruya iliwashtua kutoka katika maongezi yao..

"Aahha hapana" Aretha akainuka ili kuweza kusalimiana

"Derrick karibu sana" Beruya akamsalimia

"Asante, tumekusubiri sana B aisee" Derrick akalaumu

"Hahaha pole sana rafiki yangu, majukumu ya kiofisi na maandalizi vilinikaba...aaha wamewahudumia kwa vinywaji kweli?" Akauliza Beruya

"Aaaah wapi, koo limekauka B, hawajui ukarimu watu wako" akaendelea kulalamika Derrick

"Hahaha wasamehe Derrick bwana, watakuwa wamekamatwa na majukumu wakasahau" akasema Beruya na kuelekea kwenye eneo ambapo kulikuwa na jokofu dogo na kutoa boksi la juisi kisha akachukua glasi nyepesi na kurudi nazo mezani.

Wakaendelea na mazungumzo huku akimpa Aretha maelekezo wakati wakipata juisi taratibu.

Wakainuka na kuelekea mahali ambapo Beruya alipaandaa kwa ajili ya picha as Aretha kukaa.

"Asante sana Beruya" Aretha alifurahi sana na kumshukuru akionesha kuridhika na eneo lile.

Derrick akaridhika baada ya kuona Aretha akifurahia

"B, samahani kuna kitu nataka nimuulize!" Derrick akamgeukia Beruya

"Uliza tu rafiki yangu" Beruya akamjibu

"Unamfahamu mtu aitwaye BM, maana tumemkuta humu ndani"

Aretha akageuka haraka kumwangalia Beruya usoni maana naye alitamani kumuuliza swali hilo hilo lakini alikuwa akisubiri muda watakapomaliza mazungumzo ya picha!

"Aaaaah Bon, alikuwa hapa?" Beruya akauliza kwa mshangao

"Kumbe unamfahamu?" Aretha akauliza nae akishangaa

Wote wawili wakabaki wakimuangalia Beruya ambaye alijaa tabasamu wakati akiuliza

"Ndio namfahamu Aretha, ni mdau mkubwa sana kwenye biashara ya picha, mara kadhaa amehudhuria maonesho tuliyofanya na Melissa" akaeleza Beruya kwa furaha huku akishangaa kama BM alikuwa mahali pale.

Derrick akamwangalia Aretha kuona mwitikio wake kwa taarifa ile

"Aretha, BM anapenda sana picha lakini mpaka anunue ni lazima hiyo picha iwe na mvuto anaoutaka" Beruya akamwambia

"Alishawahi kununua picha kwako?" Derrick akauliza

"Hapana Derrick, sio mimi wala Melissa tumefanikiwa kumuuzia picha lakini alitoa mchango mkubwa kutusaidia kuhakikisha tunafanikisha maonesho yetu mara zote tulizomwendea"

"Uliwahi kumwambia chochote kuhusu mimi?" Aretha aliyekuwa kimya akauliza

"Kuhusu wewe!!! Hapana. Hata sikujua kama yuko hapa" Beruya akaongea kwa shauku kubwa huku akimshika mikono Aretha

"Oooh kama atakuwepo huenda ukapata nafasi ya kuongea nae Aretha"

"Aaaahhh" Aretha akashangaa

Derrick alipoona mshangao wa Aretha akaamua kubadilisha muelekeo wa mazungumzo

"Hivyo, B kesho picha zinawekwa mida gani?" Akauliza

"Oooh kesho picha zinawekwa usiku saa sita Derrick japokuwa zinaweza kuletwa mapema na ukawepo kuhakikisha zinawekwa inavyotakiwa" Beruya akamwambia

"Oooh basi sawa. Tutafanya hivyo. Kuna ziada labda?" Akauliza Derrick

Aretha alikuwa katika dimbwi la mawazo mpaka mkono wa Derrick ulipomshika begani na kumfanya amgeukie

"Kuna maelekezo machache tu kwenye uwekaji wa picha natamani tuongee na Aretha" Beruya akamshika tena mkono Aretha na wakaelekea mahali ambapo kulikuwa na baadhi ya picha zilizokuwa kwenye majaribio.

"Unapoweka picha zingatia hadithi iliyo nyuma ya uchoraji wako" Beruya akaendelea na kumuelekeza Aretha ambaye sasa alijitahidi kumsikiliza

Wakaendelea na maelekezo yale kwa muda mrefu kidogo mpaka walipomaliza bado Derrick hakumuacha Aretha na alionekana kufurahia, mpaka walipomaliza na kuondoka.