Mlango ulipofunguliwa Edrian akawahi kuinua kichwa chake kilichokuwa kimeinama kuelekea uso wa Aretha, lakini walipogeuza macho yao yalikutana na mwanaume aliyavalia suti safi ya rangi ya kahawia. Kwa ule unadhifu wa mavazi yake, na mkato wa nywele zake, alionekana kuwa mtu mwenye hadhi ya juu.
Aliwaangalia kisha akatabasamu, macho yalimtazama Aretha kama mtu atazamapo kitu cha thamani mbele yake.
"Hello Aretha" akasalimia na kusogea pembeni kuwapisha waweze kupita, kitendo hiki kilionekana wazi kumshtua Edrian na Aretha pia. Wakiwa wamepiga hatua chache kutoka ndani ya lifti,
Aretha hakuweza kujibu zaidi ya kumwangalia huyu aliyemsalimia ambaye nae alishaingia kwenye lifti na kubonyeza mahali alipotaka kuelekea. Hali ile ya Aretha kupata kigugumizi cha kuitikia ile salamu kulimpa yule mwanaume tabasamu pana zaidi. Mlango wa lifti ukajifunga ukiwaacha Aretha na Ed wakiwa katika sintofahamu ya mtu huyo.
"Unamfahamu?" Edrian akamuuliza Aretha walipoanza kuelekea kwenye mlango wa kutokea.
"Sidhani kama nafahamu" Aretha alijibu akijaribu kuvuta kumbukumbu kama alimfahamu mtu huyu!
Edrian aliwaza maana sura ya yule mtu bado ilibaki kwenye akili yake na kwa namna alivyotabasamu akimwangalia Aretha. "Ni nani huyu" akajiuliza.
Wakaelekea mpaka gari ilipokuwa imeegeshwa, lakini Edrian akionekana kuwa kimya katika mawazo.
"Rian" Aretha akamuita
"Eeehm" akaitika Edrian
"Unafikiri nini umekuwa kimya" akauliza Aretha mara tu walipoondoka eneo lile!
Edrian akamwangalia Aretha usoni kisha akarudisha macho yake barabarani, moyoni mwake akifarijika kuona hali ya kujali iliyoonekana kwa mpenzi wake. Akaamua aweke wazi hisia zake
"Nina mashaka na yule mtu aliyekusalimia, kama wewe humkumbuki inakuwaje yeye anakufahamu hadi jina lako?" Edrian aliongea kwa utulivu
"Hata mimi sijaelewa Rian. Ila usiruhusu akufikirishe sana sababu naamini tutafahamu tu" Aretha akampa hakikisho Edrian
"Mhhhhm" akashusha pumzi, "sawa princess, usisahau kuwa makini iwapo utamuona tena" Edrian akamsihi Aretha
"Nitafanya hivyo Rian." Akajibu Aretha, kisha kimya cha sekunde chache kikapita kati yao.
"Rian, nina ombi moja"
"Aahm" akaitika Edrian huku moyo na masikio yake vikitaka kusikia ombi hilo
"Aaah. ..naona ninaingia sana kwenye ratiba zako za kazi Rian, kama leo karibia nusu ya siku umeimaliza nami. Natamani nisiwe sehemu ya kurudisha juhudi zako nyuma" Aretha akamwangalia Edrian kwa huruma
Akatabasamu, "kweli hajui kwa kiwango gani natamani kila muda angekuwa karibu nami" akawaza Edrian
"Retha, ukiona niko nawe fahamu nimemaliza karibia asilimia tisini na tano ya ratiba yangu. Na ikiwa sio hivyo uwe na uhakika kuwa nina mtu nimemuamini kusimamia jukumu katika kiwango kile kile kama nifanyacho mimi."
"Rian, usijaribu kuniridhisha_"
"Hapana" Edrian akamkatisha Aretha, "Please princess, hutakiwi kuwa na wasiwasi nami. Japokuwa ninatamani masaa yasimame niyanunue yote tuwe pamoja wakati wote"
Uso wa Aretha ukajawa na soni baada ya kusikia maneno yale ya Edrian, "Ninajua Retha, usiwe na wazi. Hata hivyo niko nawe hivi hii wiki sababu ni onesho lako la kwanza. Naamini utajifunza mbeleni kutembea mwenyewe"
"Ahhm..sawa Rian. Asante sana kwa kunipa muda wako. Nakupenda Rian" akamaliza Aretha kwa aibu huku akifinya vidole vyake
"Asante Retha" Edrian alipoyasikia maneno haya ya Aretha, moyo wake ukajawa na furaha isiyoelezeka na akajikuta akiegesha gari pembeni karibu na A-Town Memorial Hall.
Edrian akamwangalia Aretha, "I love you Retha" akasema na kuchukua mkono wake wa kushoto na kumbusu.
Hali ya hewa ndani ya gari ilibadilika, Edrian alimwangalia Aretha kwa mapenzi mazito ambayo yalifanya iwe rahisi kutambua alimaanisha kile alichokisema.
"I love you" akainama na kumbusu kwenye paji la uso kabla hajamuuliza swali lililomshtua Aretha karibia aruke kwenye kiti alichokikalia
Macho yake akayaelekeza moja kwa moja kwa Edrian, akawa kama mtu aliyeshtuliwa na taarifa asizozitegemea. Akatoa mikono yake na kuikumbatia tumboni mwake, bado alitamani asikie mara ya pili, alihisi hakusikia vyema
"Rian, umeniuliza sawa au nimesikia vibaya"