webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

KUNA MTU

"Sawa baba, lakini kuna kitu kinanipa wasi wasi" Joselyn akamwangalia baba yake ambaye alikuwa akifuta mikono yake na taulo baada ya kumaliza kifungua kinywa

"Nini tena binti yangu?" Akauliza Martinez

"Nina wasi wasi na Ed,....aahm... ni kama ana nia mbili kuendelea na pete na hasa tangu alipogundua yule mtu wako pale Boric amekuwa mbali na mimi"

"Eeehmmm..... wewe unatakiwa kumuonesha haujui chochote kuhusu mimi. Make him see your love is pure Joselyn"

"Lakini baba.... what if amepata mtu mwingine?" Joselyn alijibu huku akinawa mikono kwenye karo lililokuwa pembeni ya ukumbi huu wa chakula....

"Tutamuondoa....mpaka tufanikishe mpango wetu. Au umemuona mwanamke mwingine aliyekupa wasiwasi?" Akauliza Martinez ambaye sasa aliinuka kumsogelea binti yake ambaye alikuwa akifuta mikono..

"Aaah sijui baba ila jana kuna binti mshamba mmoja hivi alikuja na Derrick....lakini Ed alikuwa wa tofauti kila mara alipoongelewa huyo binti. Sina hakika lakini kuna kitu kinaendelea" akamueleza baba yake

"Mmmmmh... sawa. Fanya utafiti mdogo juu yake halafu nijulishe nitalifanyia kazi. Kwa sasa please play a part of a good fiancee...sawa binti yangu?" Akasema maneno haya huku akimbusu paji la uso binti yake.

"Haya baba. Nitajaribu" Joselyn akamkumbatia baba yake na wote wawili wakaondoka kuelekea kazini.

*****************

Edrian alikuwa busy na watu wa IT ambao walikuwa wakifuata maelekezo ya Captain ili kuweza kufungua kompyuta za kila idara. Hii ilikuwa baada ya Captain kumweleza Ed kuwa kuna mtu alitaka kudukua taarifa za SGC, lakini 4D walishaweka ulinzi wa kompyuta zile ndio maana zimejifunga.

"Mwambie Alphonce wasijaribu kuzifungua wala kupakua applikesheni kwa upya. Wasubiri muda mfupi nitaenda nao hatua kwa hatua" yalikuwa maelekezo ya wazi kutoka kwa Captain.

Saa moja lilipita na tayari karibia nusu ya kompyuta zilikuwa zimeshafunguliwa.

"Allan endelea hapo niko ofisini, nahitaji kucheck na watu wa site wanaendeleaje na maelekezo hayo.."

"Okay, bro" Allan alimjibu Ed ambaye alisimama kuelekea ofisini kwake.

"Boss nikuandalie kahawa?" Loy aliuliza mara baada ya Ed kuingia ofisini...

"Sawa.. andaa kikao cha dharura na wakuu wa idara wote.. weka maandalizi ya "Live meeting"....na pia cancel ratiba yangu ya nje kwa leo."

"Sawa boss... muda upi utafaa?" Loy akauliza akiwa amesimama tayari kwenye mashine ya kuandaa kahawa na wakati huo Ed alisimama kwenye mlango wa kuingia ofisini.

"Weka masaa mawili kabla ya muda wa kazi kuisha. Na tafadhali andaa mkutano na watu wa ulinzi, Allan atasimamia hilo."

Alipomaliza Ed aliingia ofisini, akatoa koti na kulitupia kwenye kochi. Akakaa kwenye kiti na kufungua kompyuta mpakato yake na kuendelea na kazi za ofisi. Taarifa chache zilimfadhaisha kutoka G-Town juu ya ukaguzi wa watu wa mazingira ambao waliwapa siku tatu watoe tathmini ya utunzaji wa mazingira ya mgodi huku wakitoa onyo kali la kusitisha uchimbaji hadi tathmini itakapomalizika kukaguliwa.

Ed akapiga simu kwa mkuu wa oparesheni na kuzungumza naye ambaye alimhakikishia kuwa hakuna makosa yoyote. Akaendelea kupiga akiongea na wakuu walioko kwenye oparesheni akiwaonya mambo ya kuzingatia maana ukweli alihisi kuna mtu anajaribu kuiharibia SGC..

Tangu alipoingia ofisini hakuwa ametulia hata mara moja. Ni saa nne asubuhi lakini alihisi kama jioni imeshafika..akaegama kichwa chake kwenye kiti.....simu yake ikaita... akafumbua macho kuangalia kwenye kioo....ghafla sura yake ikaonesha mng'ao wa tofauti...akatabasamu. ...

"Hello Aretha" kwa sauti ya utulivu akasalimia huku akirudisha kichwa chake kwenye kiti

"Hello Ed....aah busy na kazi?" Akauliza Aretha

"No... hapana. Siko busy tunaweza kuongea" Ed akajibu kwa haraka huku akijicheka mwenyewe maana alikuwa busy na kutatua changamoto za ofisi ila kumsikia Aretha kulimpa raha nafsini...

"Oooh... aaaah...samahani kwa kuchelewa kukujulisha mapema....aaah..nilitaka" akanyamaza Aretha kwa sekunde akifikiri asemeje..Ed akafadhaika moyoni kidogo akijua maneno yale yalikokuwa yakielekea lakini akajipa moyo akijua bado ana nafasi ya kumuona maana koti bado liko na Aretha.