webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

KUFUATILIA KITU KIZURI

Ed aliingia nyumbani mida ya saa nne usiku baada ya kushiriki chakula cha jioni na Joselyn katika hoteli ya The Crest. Alimkuta Linus amekaa sebuleni akiangalia mpira

"Hey bro habari ya kazi?" Li alimsalimia Ed alipohisi yupo hatua chache kutoka alipo

"Poa, vipi umerudi mapema leo?" Alijibu Ed na kuelekea kwenye kochi lililokuwa pembeni.

"Sio sana, nilitaka kuona mechi hii" Li alijibu.

Ed alinyamaza kimya akajitupia kwenye kochi na kuegama huku akifumba macho yake. Alikuwa amechoka lakini si kwa sababu ya kazi pekee, bado alikuwa ana vita ndani ya moyo wake na akili zake. Kwa muda mfupi moyo wake umevutwa kwa Aretha, na wakati ana ahadi na Joselyn.

Hakujua kuelezea kinachoendelea kwenye moyo wake kila mara anapotokea kumuweka Aretha katika fikra zake.

Alipoketi hapa alitamani kumuuuliza Li kama anamfahamu Aretha na kwa nini alimfuatilia. Akajiuliza namna gani ya kuanza lakini akakosa kabisa. Akiwa amefumba macho alitafakari jioni ya leo alipokuwa na Joselyn, alihisi kumsaliti mtu. Swali kubwa lilikuwa nani anayemsaliti, Joselyn? Mwenyewe? Au Aretha?

"Bro, vipi umechoka sana?" Li alimtoa kwenye masumbufu aliyokuwa akiyatafakari

"No!" Alijibu akiwa vile vile amefumba macho.

Li aliposikia jibu lile, na kwa namna anavyomfahamu Ed alijua kuna jambo linamsumbua. Kwa kawaida jibu hili humtoka anapokuwa akitafuta suluhu ya jambo gumu katika fikra zake.

"Sawa bro, ila nipo hapa in case unatahitaji kuzungumza" alisema Li kwa hisia za upendo na kumfanya Ed ajihoji kama alionekana mwenye kusumbuka zaidi!

Kikapita kimya cha muda mfupi kati ya hawa ndugu wawili. Li alitamani kuanzisha mazungumzo kuhusu kitu kile kile ambacho kilikuwa kinamsumbua Ed lakini hakutaka kumuonesha kaka yake kuwa anamfatilia.

Kimya hiki kilivunjwa kwa sauti nzito iliyotoka na mikwaruzo kwaruzo ya uchovu..

"Li" aliita Ed akiwa amefumba macho, kichwa kaegama kwenye kochi

"Yes bro" Li aliitika huku akiwa na shauku ya kusikia kama Ed atakuwa muwazi juu ya hisia zake.

"Ulimfatilia Aretha alipotoka ofisini kwangu?" Ed aliuliza kwa sauti ya chini

Looh! Swali lilikuja kama suprise kwa Li, na moja kwa moja akajua alionekana hakuwa na namna yoyote ya kuficha. Sasa alijua kazi imeanza ya kumuamsha kaka yake kwenye ukweli wa hisia zake.

"Ndio, nilimfatilia" alimjibu kwa ufupi

Ed alivuta pumzi ndefu kisha akafumbua macho na kumuangalia Li ambaye alijifanya yuko makini kwenye runinga lakini alijua nini anafanya.

"Unamfahamu?" Ed aliendelea huku akimkazia macho Li

"Hapana bro nilimuona pale ofisini?" Jibu hili la Li likatibua joto katika mwili wa Ed. Akanyamaza kidogo kutafuta katika kona gani aendelee. Li hamfahamu Aretha lakini kaamua kumfuatilia, je ametokea kumpenda? Mapigo ya moyo ya Ed yaliongezeka wazo hili lilipogonga fikra zake.

"Kwani kuna shida bro?" Aliuliza Li baada ya kuona kimya upande wa kaka yake.

Hii haikuwa rahisi kujibu, Ed akashusha pumzi

"No!" Jibu pekee lililomfanya Li ashindwe kujizuia kutabasamu, tabasamu ambalo halikufichika kwa Ed kugundua na kuuliza

"Mbona umetabasamu?"

Li akaona atumie mwanya huo kumchanganya zaidi kaka yake..

"Nimefurahi tu kuwa hapana shida kwako mimi kumfuatilia mgeni wako."

Uwhhhh Li, kwa jibu hili alipiga mshale kwenye eneo la hatari. Ed alijitahidi kutunza muonekano wa utulivu nje lakini ndani kulikuwa na mapambano yakiendelea. Hakuweza kuzuia ghasia katika hisia zake na akalipua swali kwa Li, ambalo mitetemo ya sauti yake ilimfanya Li ashangilie ndani

"Kumfuatiliaje Li?"

Mikono ya Ed aliikunja kuzuia kuonekana kwa hisia zake za wivu zilizoanza kutanda katika moyo wake.

"Hahaha bro vipi kwani, ni kufuatilia kitu kizuri ukikiona" Li alijibu kwa kicheko chepesi cha utani huku akijua athari ya maneno yale kwa kaka yake.

Ed alimuangalia Li kwa jicho lilionesha kuhitaji maelezo zaidi, wakati huo aliomba moyoni mwake isije ikawa Li amevutiwa na Aretha maana hakika hatoweza kuvumilia kumkatili mdogo wake.

"Usijali bro nilitamani kumfahamu tu kidogo lakini sikumuona. Let's hope for next time." Li aliongeza tena chumvi kwenye kidonda.

"Mmmm" Ed aliguna.

*******************