webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

IKULU IMEDUKULIWA

Please, I am _" Edrian akainuka mahali alipoketi, akamsogelea kitendo kilichomfanya Aretha asiweze kumalizia maneno yake. Ed akahakikisha yuko karibu kiasi cha kuhisi upumuaji wake, akamshika mkono taratibu huku macho yake yakimwangalia kwa upendo

"Retha, tafadhali tusizungumzie hilo kwa sasa. Nimekuelewa na ninajua nawe unanielewa, natamani uende ukapumzike utakapokuwa tayari tutazungumza mambo ya msingi. Nakupenda uwe na uhakika" Edrian akaacha macho ya Aretha yamtazame huku mikono yake ikipapasa viganja vyake

Aretha akahisi fukuto la upendo likibana kifua chake, macho yake yakalowa machozi, kwa haraka akavuta mikono yake kutoka kwenye ile ya Ed halafu akaizungusha kiunoni kwa Ed na kumkumbatia kwa nguvu akiacha machozi yalowanishe sehemu ya shati yake.

"Am so sorry Rian please.." akasema taratibu katikati ya kwikwi za kulia. Edrian alishtuliwa na kumbato lile, kwa ukakamavu wake aliweza kubaki amesimama la sivyo angeangukia mbele. Mkono wake ukatulia mgongoni kwa Aretha ukimpapasa taratibu wakati mwingine ukizipapasa nywele zake.

Akanyamaza kumuacha Aretha aondoe uchungu wote aliouhisi moyoni mwake.

"I love you Rian" Aretha akakiri katikati ya kwiki za kulia. Edrian akatabasamu aliposikia maneno hayo akajibu kwa sauti ya chini, "I love you too"

Dakika tano zilipita Aretha akiwa amekumbatia Ed huku akilaza kichwa chake tumboni kwake. Edrian aliendelea kusimama kwa ukakamavu akiacha uzito wa Aretha umuelemee huku akiendelea kucheza na nywele zake..

Aretha akaachia mikono yake ghafla alipokumbuka kitu,

"Ooooh Rian si unatakiwa kwenda kazini na mimi nakuchelewesha hapa"

Aretha akarudi nyuma akijaribu kupata namna ya kusimama, lakini Ed akamsogelea zaidi na kuziba mwanya wa yeye kuinuka. Kisha Ed akamuinua kidevu ili amuangalie usoni, akapiga hatua moja kurudi nyuma kisha akainama hadi usawa wa mdomo wa Aretha akambusu taratibu. Aretha akafumba macho akifurahia ulaini wa midomo ya Ed uliofanya tamaa yake iwake ndani akitamani kuendelea, sehemu ya juu ya tumbo lake ilipata joto ambalo hakujua limesababishwa na nini. Akajaribu kufungua mdomo wake ili kumruhusu Ed kumbusu zaidi lakini akakatisha kabla ya busu lile jepesi kugeuka kuwa zito. Akambusu kwenye paji la uso.

"Asante Aretha nitawapeleka nyumbani kisha nitaenda ofisini" kulikuwa na furaha moyoni kwa Ed alijiona kama mtu aliangusha ngome kwa ncha ya kidole..

"Rian please wahi kazini tutaondoka na "Safe Ride" Aretha akashuka kitandani akabeba mkoba wa mama yake uliokuwa juu ya kitanda waweze kutoka.

"Kwa nini nisikupeleke?" Akauliza kwa utani huku akimwangalia kwa macho yaliyomsihi

"Kwa sababu tunaweza kwenda, kisha wewe ukapata nafasi ya kuwahi kazini hata ukapumzika" maneno ya Aretha yalibeba msimamo ambao Ed alijua hatoweza kuubadili

"Na nikimwambia Li?" Akauliza kama mtoto

"No... naye anaenda kazini" Aretha akamjibu huku akipiga hatua kusogea aliposimama Ed..

Macho yao yakakutana, Edrian akatabasamu na kumvuta Aretha upande wake "Okay princess mtaenda na "Safe Drive nipe simu yako" alipompatia simu akainama na kumbusu kisha wakatoka huku yeye akiagiza usafiri kwa kutumia aplikesheni ya Safe Drive iliyokuwa kwenye simu ya Aretha.

****************

Baada ya kuhakikisha wameondoka hospitalini, Ed aliingia kwenye gari yake, tabasamu lake usoni lilimfanya Li ambaye alikamata usukani amtanie kaka yake,

"Bro umetungua ndege au vipi?"

"Hahahaha, nimedukua ikulu Li" Ed akaachia kicheko chepesi kisha akamwambia

"Asante Li"

"Chochote kwa ajili ya kaka mkubwa" Li akajibu kwa furaha

"Unajua kushauri mambo ambayo huna ujuzi nayo hahahaha" Ed akamtania

"Lakini wewe ndio shamba darasa langu" akajitetea Li

"Unahitaji kupata darasa lako hahaha" Ed akaendelea kumtania

Li akacheka sana kisha akamuuliza Ed, "Vipi umefanikiwa kuona chochote kwenye CCTV?

"Inaonesha hakuna mtu aliyeingia ukumbini baada ya Beruya na Damian kutoka. Lakini kuna kitu ninakitafakari, baada ya pazia kufunguliwa, watu walipatwa na mshtuko kuona picha zilivyoharibiwa lakini huyu BM haoneshi kushtuka bali alitabasamu"

"Eeeeh! Anaweza kuwa ni yeye? Li akahoji kwa mshtuko