webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

HAIKUWA LOVEBITE

Jumapili ilikuwa tulivu isiyo na mambo mengi kwa Ed, mida hii alikuwa nje ya nyumba ya Martinez, akimsubiri Joselyn kama ambavyo walikubaliana. Akiwa amekaa ndani ya gari yake aliendelea kugusa simu yake, Lyn alimuomba dakika kumi amalizie kubadili nguo baada ya Ed kumpa taarifa kuwa wataelekea ufukweni mwa ziwa Dishan.

Mlango wa mdogo wa geti ulifunguliwa na kumfanya Ed ainue kichwa kuangalia, Lyn alitokeza akiwa amevalia kaptula fupi ya jinsi na 'body top' nyeupe, miguuni alivaa raba nzuri nyeupe, alifunga nywele zake pamoja na kuwa kama mkia wa farasi. Muonekano huu ungekuweza kukausha pumzi ya mtu..

Ed alimuangalia mpaka alipoingia ndani ya gari, akikubali kuwa Lyn ni mzuri..aaah sasa alivutia kumwangalia.

"Ed come on..... uko kwenye mission ya kumuuliza don't let yourself be distracted" alijisemea moyoni Ed

"Eeeh Edrian pole kukuchelewesha" alisema baada ya kufungua mlango na kuingia.

"No problem" akajibu, wakati huo akawasha gari ili kuondoka lakini alishtuliwa na busu liloangukia kwenye shavu la kushoto....

"I miss you" Joselyn alisema akijiweka vyema kwenye kiti na kufunga mkanda, tabasamu la uchokozi lilikuwa usoni mwake.

"Asante" Edrian aliambulia kujibu. Kichwa chake kikaruka mbali kumkumbuka Aretha na uso wake ghafla ukakunjamana kidogo..

"Are you okay?" Alishtuliwa na swali kutoka kwa Lyn.

"I am" akashusha pumzi baada ya kumjibu na kujaribu kuweka tabasamu jepesi.

Wakaondoka, maongezi yaliendelea, Ed akijaribu kuweka ukawaida wake ili kutomshtua Lyn na mabadiliko yanayoendelea kwake.

Hakuwahi kuwaza kama angekuwa kwenye hali kama hii, njia panda ya mahusiano. Yuko na Lyn lakini anataka kumfahamu zaidi Aretha. Alimwangalia Joselyn ambaye sasa aliegama kwenye kiti akibofya simu yake.

Wakafika Dishan, kama kawaida ya eneo hili wikiendi huwa lina watu mbali mbali ambao hupenda kuangalia mandhari ya ziwa hili dogo kwa ukubwa lakini kina cha maji yake ni kirefu. Na moja ya maajabu ya ziwa hili ni mida ya jioni maji yake huwa ya moto kama yanachemshwa na kufanya jioni watu kusimama ukingoni mwake wakiweka miguu yao.

Pembeni kwa upande wa kushoto ilikuwepo hoteli iliyokuwa na sifa ya nyota tano iliyojengwa kwenye kilima. Ndani ya hotel hii muonekano wa ziwa Dishan ungekupa mshangao, hivyo wateja wengi walipenda kuja kwa sababu hiyo.

Ed alivuta kiti nyuma kumpa nafasi Lyn kukaa kisha akaelekea kukaa kwenye kiti chake. Haikuwa mara ya kwanza kwa Ed kuwa hapa lakini pamoja na Lyn ilikuwa mara ya kwanza. Walikaa kwenye baraza mojawapo ya hoteli hii ambayo ilikuwa maalum kwa meza moja tu. Walikuwa peke yao, muonekano wa ziwa na kuzama taratibu kwa jua kulileta mandhari safi machoni.

Akaja mhudumu na kuchukua oda zao, huku akiwaacha kuendelea na vinywaji alivyoleta.

Waliongea mawili matatu kuulizana hali zao na maendeleo ya shughuli zao.

"Lyn, kuna kitu nataka tuongee na nakuomba uwe mkweli, nami nitakuwa mkweli kwako" Ed alitupia mjadala mezani kitendo kilichomfanya Joselyn ashtuke na kuweka simu mezani aliyokuwa akipiga picha na kumwangalia..

"Aha.." Lyn aliitika na kuonesha kuwa anasubiri kusikia anachotaka kusema..

Ed akamwangalia usoni kisha akaendelea, "Ile stori ya love bite shingoni ilikuwa ya kweli au la?"

Joselyn hakuona hili swali likija akashtuka, "kwa nini umeuliza?"

"Nakuuliza tena sababu nataka kujua ukweli Lyn, ulisema Derrick ndie alihusika, ni kweli?"

Joselyn ni mjanja kuliko Ed alivyomfahamu, akajua kuna kitu kimeendelea na hajajua. Akamwangalia Ed

"Siku ile hukutaka nikumalizie lakini ni kweli alinikaba shingoni baada ya kubishana nae aliponikatalia nisiingie chumbani kwako, uliona alama ya vidole vyake haikuwa love bite Ed."

"What" Ed akashtuka

"Nisikilize, nilijaribu kuficha lakini naona ulitambua nadhani ile make up ilipungua" Lyn alijieleza huku akiweka uso wake kwa namna ambayo ungemuona ungejua anasema ukweli mtupu.

Lakini kama baba alivyo ndivyo binti alivyo, siku ile alipaka make up iliyotengeneza alama ya love bite shingoni mwake. Na alijua kabisa Ed hatokaa kusikiliza stori yote, alishatengeneza matukio yote na kuweka mizania kwa kila hatua.