webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

FURAHA TU

Edrian alitamani muda usimame aendelee kuwa na Aretha ofisini kwake lakini akakumbuka alitakiwa kumuona mama yake jioni, na bado alihitaji kufuatilia ukweli wa nani alihusika katika kuharibu onesho la Beruya.

Baada ya Aretha kumuelezea mpango wa onesho atakaloliandaa kwa ajili ya Beruya, Ed akampigia Derrick waonane hospitali lakini akawajuza kuwa Beruya amepewa ruhusa tayari hivyo atakuwa kwake.

"Sasa nisaidie namba ya Yassin nataka kuongea nanyi, unaweza kuwa na nafasi jioni ya leo tukutane The Lounge?" Ed akamuuliza Derrick kwenye simu

Alipomaliaza, akapiga hatua kurudi alipoketi Aretha, "Retha, Beruya ameruhusiwa tayari hivyo atakuwa kwake. Bado unataka tuonane nae huko?" Akamuuliza

"Aaaah sidhani kama itakuwa rahisi ninawaza kama ni yeye aliyetuma zile jumbe hatafurahi kutuona. Lakini kama ni mtu mwingine aliyetumia simu yake basi atajaribu kutuzuia tusimuone. Nafanyaje Rian." Aretha akauliza kwa huzuni

"Relax princess" Edrian akamshika mikono Aretha kisha akaendelea.

"Tutaonana na Yassin nina vitu vichache vya kuzungumza naye pamoja na Derrick, utakuwa vizuri twende wote?" Akamuuliza

"Niko tayari Rian, nimetoa ratiba yote leo kwa ajili___" ghafla akasita kuendelea macho yake yakiangalia mikono ya Edrian ikiminya ile ya kwake, hisia zilianza kuufanya mwili wake ushindwe kuficha matamanio yake akabaki akimtazama kisha akashusha pumzi kwa nguvu

Edrian ambaye hakujua kwa kiasi gani mguso wake ulisafirisha mawimbi ya mahaba kwenye mwili wa Aretha akamwangalia usoni akijiuliza nini kimemkatisha

"Retha" akamuita huku akihamisha mikono yake na kumshika mabega, lakini alipotazama macho yake aliona uhitaji wa Aretha na namna ambavyo alikaza kuangalia midomo yake, akatabasamu akainama taratibu ili kumbusu.

Kabla ya kukaribia midomo yake, alishtuliwa na Aretha ambaye aliwahi kuipeleka ya kwake na akawa wa kwanza kumbusu. Akampokea na wote wakazama kwenye mabusu moto moto.

Aretha hakuwa na uzoefu sana lakini aliweka moyo wake wote kumbusu Edrian. Njaa yake ilikuwa kubwa, na wakati huo huzuni yake ilimuweka kwenye uhitaji wa mguso wa faraja kutoka kwa Edrian.

Edrian akamnyanyua na kumketisha mapajani mwake macho yao kakakutana na kila mmoja akauona uhitaji wa mwingine. Akaanza kumbusu taratibu shingoni,

"Rian" sauti dhaifu ya Aretha ilisikika na kumfanya Edrian atabasamu kwa furaha kuona alimuathiri binti huyu kwa midomo yake. Akaendelea taratibu huku sauti ya Aretha ikizidi kuwa dhaifu akimuita Ed

Tone la maji likamwangukia Ed shavuni, akashtuka na kuinua kichwa chake kilichozama shingoni kwa Aretha. Akamwangalia usoni Aretha, ndipo alipogundua kilichomwangukia ni tone la machozi na si maji! Akatumia kidole gumba kufuta machozi kisha kwa wasi wasi akamuuliza

"Retha are you o_" Edrian akamuita lakini akashtuliwa na kumbato la ghafla alilopewa na Aretha. Akazungusha mikono yake na kumkumbatia pia akiwa na mshangao wa kwa nini Aretha alitoa machozi.

Baada ya kudumu kwa sekunde kadhaa kwenye kumbatio lile, Aretha akawa wa kwanza kumwachia Ed, kwa aibu akasimama na kujiweka vyema. Ed akainuka naye akamsogelea Aretha,

"Nitakuweka vizuri usiwe na wasi, lakini uko sawa Aretha?" Akauliza kwa kujali huku macho yake yakimtazama

"Aaa...ni..niko sawa Rian.furaha tu..aaargh" akakaa kwenye kochi na kuuficha uso wake kwenye mapaja yake

Ed alipoona hivi akajua Aretha aliona aibu," "it's okay Retha I understand." Akatabasamu na kuelekea alipoketi akanyoosha mkono kumuelekea "twende ukajiweke vizuri"

Aretha akainua macho na kuungalia mkono wa Ed kisha akaupokea na kusimama. Edrian akamuongoza mpaka kwenye mlango wa kioo uliokuwa pembeni karibu na kabati la lililobeba tuzo mbali mbali za SGC. Akauvuta huku akibaki ameshikilia kitasa, "jiweke vyema nakusubiri" akamwambia na kutabasamu.

Aretha akaingia ndani ya maliwato haya yaliyoonekana kuwa safi na mazingira yake ya kuvutia. Kioo kikubwa kilikuwa pembeni huku pembeni yake kukiwa na kabati dogo la ukutani ambalo lilinakshiwa kwa chupa za manukato zilizoonekana kuwa ghali.

Aretha akajitazama uso wake ulioonekana kung'aa, akijishika midomo yake akivuta hisia..