webnovel

Tafadhali, Nipende(Please, Love me)

Kuwa na kila kitu kizuri kwenye maisha haimaanishi kuwa una furaha. Ed ni kijana mwenye mafanikio makubwa  akiwa na umri mdogo. Wengi waliyatamani maisha yake, na kwa sababu hiyo alikuwa ni role model kwa vijana wengi wenye ndoto ya kufanikiwa. Akiwa kijana mdogo alijiwekea malengo ya kutoyaleta mapenzi kabla ya wakati wake. Alitumia muda mwingi kuweka imara msingi wa biashara zilizomilikiwa na Simunge Group of Companies. Aliogopa kuyapa nafasi mapenzi wakati alikuwa na mengi ya kufanya. Hakutaka kuona akishindwa pande mbili LAKINI baada ya muda kwenda na kwa msisitizo kutoka kwa mama yake, Ed anaamua kujitosa kupenda, lakini hakujua ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kukuchezesha kamari na ukabaki njia panda. Bila kujua yeye anapanga na wapo wanaopanga katika mipango yake. Martinez Kussah mfalme wa kupindua meza na kuyapanga matokeo anayotaka. Kabla Ed hajatweka ndoano yake kilindini kupata samaki, Martinez anamrushia samaki, Joselyn Martinez. Ajali ya kukutana uwanja wa ndege, inapelekea kuingia ndege moja. Haikuishia hapo, viti vinavyoambatana Business Class na mwisho hoteli moja. Coincidence? La hasha Mwanaume mmoja nyuma ya haya anahakikisha jambo lake lazima lifanikiwe. Baada ya Ed kufahamiana na Joselyn anaanza  taratibu kuyaonja mahusiano ya mapenzi, lakini haachi misimamo yake, na anaiweka wazi kwa huyu mpenzi wake. Hatojihusisha nae kimwili hadi atakapomtangaza kuwa mke wake, bila kujua kuwa Joselyn ni mlamba asali asiyeweza kuliacha sega. Ed anakuta amevunja kanuni ya kwanza, na kumbe nyuma ya haya mkono wa Joselyn ulihusika. Na kwa sababu he is a man of his word analazimika kuendelea na safari hii ya mapenzi. Wiki tatu kabla ya kumvalisha pete, anakutana na simple girl Aretha, mchoraji. Picha ya binti huyu inakamata ubongo wa Ed, anaanza kuona kiza katika maamuzi yake. Anapojaribu kuwa karibu naye, kumbe kuna makundi mawili ya watu yanamsogelea huyu binti. Wale wanaotaka kumtumia kubadilisha maamuzi ya Ed na wengine wanataka kumuondoa mbali na Ed. Sasa maisha ya Aretha yanakuwa hatarini zaidi ikiwa yuko on the badside ya Martinez.  Kabla ya haya makundi kupenyeza agenda zao, kundi la tatu lililo hatari zaidi linaibuka. Ed yuko njia panda ya kupambania moyo wake au misimamo yake, biashara au maisha yake. Amuokoe Aretha au aendelee na Joselyn. Let's wait as chapters unveil the desires of Edrian heart.

Evelyne_Buc · Hiện thực
Không đủ số lượng người đọc
245 Chs

ANAWAPENDA WOTE?

"Aretha usihofu....nitakuelewa tu. Please endelea" Ed akamtia moyo aweze kuongea hata kama atakachosema kisingemfurahisha..

"Aaah hapana...Ed..aaaa. mama...ameomba nisije sa.." kabla hajamaliza kulisika sauti za ajabu na kumfanya Ed kuita

"Aretha... Aretha" kisha sauti nyingine ikasikika

"Mwanangu habari ya kazi"

Mapigo ya moyo wa Ed yakaongezeka kwa ghafla.. akajua huyo atakuwa mama yake na Aretha... kuna nini! Akaogopa, akajikaza na kujibu

"Salama mama, shikamoo"

"Marhabaa mwanangu, sasa msamehe huyu binti yangu na kigugumizi chake" mama huyu akaongea na kumfanya Ed walau kutabasamu...

"Hapana shida mama" wakati anajibu Loy aligonga mlango ikabidi azibe simu na kumruhusu aingie..

"Kaniaga kuwa anakuja huko kurudisha koti lako, na mimi nikaomba uje ulichukue mwenyewe baba"

Ed akashusha pumzi na kumwashiria Loy aendelee baada ya kuwa ameweka kikombe cha kahawa mezani..

"Oooh basi sawa mama. Nitafika baadae kulichukua" Ed akamjibu mama yake Aretha huku moyoni akiwaza huenda mama yake hataki Aretha atoke kuonana na yeye...

"Vizuri mwanangu, saa ngapi nikusubiri maana huyu binti aweza kuwa bado chuo?"

Akammaliza kabisa Ed, maana alitaka kumuona Aretha na sasa atatakiwa kuonana na mama yake tu.. "am loosing" akawaza.

"Saa kumi na mbili mama nitakuwa hapo" Edrian akajibu kwa upole

"Sawa mwanangu.. nitakusubiri, kazi njema" mama akamuaga. Ed alitegemea angemsikia tena Aretha lakini simu ikakatwa.

"What a nightmare" Edrian akawaza. Jumanne hii aliiona kama ina kisirani na yeye. Kuanzia ofisini hadi kwa mtu aliyetamani kumfariji, akamfikiria mama yake na Aretha " Anamlinda binti mkubwa huyu daaah".

Akachukua kikombe na kunywa kahawa huku akiendelea na kupitia taarifa nyingine za kiofisi kwenye kompyuta yake mpaka Allan alipoingia na wakaanza kujadili yaliyotokea leo..

"Bro kesho tunahitaji kuandaa trip kuangalia site zote. Kuna mbinu nahisi kabisa inaandaliwa kuharibu oparesheni" Allan akamtahadharisha Ed

"Nimeshaiona hiyo Allan. Ngoja tumalize hicho kikao jioni, Loy anashughulikia. Tutaenda live na watu wa site. Captain anaendelea na kumtafuta aliyejaribu kudukua taarifa. Amesema hakuwa mbali na jengo hili. So anahisi huenda yuko kwenye jengo hili hata kama si ofisi zetu."

"Sure bro.... kwa ulinzi alioweka kwenye hizi kompyuta namna pekee ya kuzifikia ni uwe karibu nazo"

"Check na kampuni ya ulinzi, angalieni CCTV" akasisitiza Ed.

Wakaendelea kushughulikia mambo ya ofisi hadi muda wa chakula cha mchana. Ed akatamani kumtumia ujumbe Aretha amuulize kama kuna shida akaogopa isije ikawa simu imebaki na mama yake. "Aaaarrrgh" akaunguruma.

Loy akamletea chakula cha mchana ofisini baada ya kuona boss wake hana mpango wa kutoka

"Asante Loy.... umesumbuka tena kama sina miguu"

"Aaah hapana boss najua uko busy, na kikao kitaanza baada ya lunch usije miss chakula"

"Nashukuru sana Loy. Tuendelee na kazi" Ed aliinuka nakukaa kwenye kochi akiweka chakula chake mezani na kuanza kula. Akakumbuka jana alipokuwa akila pembeni akiwepo Aretha akacheka. .. "very shy" akajisemea.

*******************

"Mama mie naondoka" Derrick alimuaga mama yake ambaye alikuwa amekaa kwenye kiti chake baada ya kuwa wamepata chakula cha mchana...

"Kabla hujaondoka... jana nilitaka kukuuliza kitu lakini ukaenda na mjomba wako sijui wapi na ukarudi usiku" Mrs Simunge akamrudisha mwanae Derrick

"Mama nina kipindi saa tisa jamani..."

"Eeehshhhhhhh...nitauliza kwa ufupi.. huu ni uzembe wako umelala muda wote hata sikuweza kukuuliza"

Derrick akakaa pembeni ya mama yake

"Najua unataka kuuliza juu ya wanawake wawili wakaondoka na kaka"

"Mwanangu unajua kunisoma, haya niambie yule Aretha ni nani kwako na kwa kaka yako?" Akamuuliza huku akimfinya kwenye mkono

"Mama, aaargh!"

"Usinidanganye Derrick" akamuonya mwanae

"Mama yule Aretha alikuja na mimi... japokuwa alimfahamu bro kabla ya mimi" Derrick anyamaza

"Eeeh hebu elezea vizuri hilo tayari nalijua"

Mama yake akataka atoe maelezo zaidi..

"Mama jamani, ..... basi Bro anampenda" Derrick akamwambia mama yake ukweli

"Anawapenda wote wawili?" Akauliza kwa wasi wasi.