webnovel

usife

" Unahakika hajarudi kwenye kasri au?"

akauliza mfalme Blooden kwa hofu.

"ndiyo mkubwa"

"sawa,mtafuteni mtaani na yeyote yule atakayekutwa basi achinjwe ama la aletwe kwangu na apate mateso makali!"

mfalme akaagiza..

"sawa mfalme lakini nimepata taarifa kuwa jioni alionekana maeneo ya sokoni akiwa na kibinti fulani hivi.."

"unakujua kwao?"akauliza mfalme kwa shauku kubwa.

"ndiyo mtukufu"

"basi nenda na lolote baya likiwa limempata prince Mesel basi huyo binti ...unajua cha kumfanya."

"sawa mfalme"

"fanya haraka!!!!!!!" akafoka mfalme kwa hasira kali.

"sawa."mlinzi mkuu akaondoka haraka kwenda kwa Ecca.Yule mwanamke aliye msaidia Nora ni Ecca.Akampeleka mpaka nyumbani kwake na kumlaza kitandani.

"Nora!Nora!Nora!Amka tafadhali usife nakuomba"

Ecca akaita na haraka akaukamata mshale mmoja na kuuchomoa kwa nguvu.

"aaah!" akaweweseka Nora kwa maumivu makali sana.

"Pole jamani....pole sana" Ecca akaukamata mwingine tena na kuuchomoa pia.Hapo Nora maumivu ndio yakazidi.Kwa uangalifu..akaukamata mwingine na kuuchomoa.

"pole jamani.utakuwa sawa usijali.sawa?"

akamvua shati na kumuacha kifua wazi ambacho kilitapakaa damu nyingi mno.Haraka akakimbia kuelekea dukani kununua dawa za vidonda.

"umeumia na nini Ecca?"

muuza madawa akauliza akimkagua Ecca.

"Nipe dawa,maswali baadae tafadhali."

"sawa,chukua wala usijali."

"asante" Ecca akachukua dawa na kukimbia mbio kutoka pale.

Baada ya kufika tu akaanza kumtibia Nora kwa tahadhali kubwa mno tena sana.

"dada huyu nani?" akauliza mdogo wake ambaye ni Scan.

"huyu achana naye,utamjua akipona.sawa?"

"sawa." Scan akarudi ndani kulala lakini alikuwa na hofu kidogo.

asubuh Nora ndio akawa anapata fahamu sas...